Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Watumishi wa Afya walioajiriwa september 2013 na 2014 kwa sasa wana miaka takribani 6 mpaka 7 kazini na hawajawahi kupandishwa madaraja ya mishahara yao ambao ni Takwa la kisheria

Mnaahidi watapandishwa LINI? SABABU ZA MSINGI

KUWACHELEWESHEA HAKI YAO NI NINI?
 
Watakuwa hapa ila hawatajibu maswali magumu mf

Haki ya mtumishi kupanda daraja

Vipimo vya DNA
wingi wa vituo vya afya na ukosefu wa dawa

Bima ya afya kuendelea kupunguza dawa anazotakiwa kupewa mwanachama n.k
 
Poleni na kazi watendaji na watalaam wetu. Mi naomba ile namba ya Amana referral Hospital mlioweka kama contact number mnazoweka ziwe zinafanya kazi, mfano namba +255 22 286 1902 ukipiga unapata majibu " Sorry the call is not through, because the callee has not paid the bills" tunajua mnatumia namba za mkononi kwa ajili ya kazi za ofisi lakini hii ni kero kubwa sana

Karibu Idara zote za serikali wana tatizo hilo, Ila kwa muhimu wa TAASISI yenu tunaomba mtuwekee namba inayofanya kazi , maana kama ni bili hailipwi leo wala kesho. najua itachukua muda mrefu kutatua hilo ila naomba tu utujulishe kama huu ujumbe umeusoma na unashughulikia, itatosha, sisi tutasubiri hata kama mtarekebisha 2021/ - 2030 hatujali tumevumilia mengi sana.
 
Asante kwa kuwasiliana nasi.
Kupima Maambukizi ya Ugonjwa wa Homa ya Mapafu (Covid-19) kwa Raia wa Tanzania ni Shilingi 40,000, raia wa kigeni ni USD 50$
Asante kwa majibu mujarab sasa pale Mabibo ni wapi hasa wanapima na siku na muda wa kazi tafadhali
 

Nimekusoma ndugu mtaalam na mchambuzi mbobevu wa mambo ya kiafya, Wizara wanatakiwa kuhakikisha kunakuwepo na uhakika wa vipimo mhimu katika hospital zao maana ni aibu kubwa unakuta kila kipimo mhimu kutopatikana kwa mda wote kwa sababu ya mashine kuwa mbovu ama kutokuwepo kabisa vipimo hitajika kwa hospital ya ngazi husika ama wafuatilie kwa ukaribu zaidi uendeshaji wa hospital zao ili kupunguza vikwazo kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma kwao.

Jamii kubwa inategemea sana hizi hospital kwa sababu ya kipato duni lakini hugeuka kuwa kero kwao kuliko suluhisho kwa shida zao hivo kutafuta njia mbadala ambazo huwa si rafiki kwa afya zao.

Nakazia tena inatia aibu sana kukosekana kwa basic laboratory investigations kwa hospital ngazi ya rufaa mkoa, wizara inafanya kazi kubwa na nzuri usiku na mchana kujaribu kupanua na kuongeza juhudi ya kutoa huduma bora kwa wananchi lakini iwapunguzie mzigo kwa kuongeza vipimo na wataalam wa kada husika ili kuleta ustawi bora wa afya
 

Jonno sijui uko mkoa gani lakini huku kwetu naona wanaendelea kuboresha siku baada ya siku.

Ili kuongeza ufanisi na kupunguza au kubalance idadi ya wagonjwa kadri ya uwezo wa hospital, hospital zetu kubwa za rufaa kanda zimeendelea kuwezeshwa kuwa vipimo ambavyo ni vya gharama kubwa na vichache, na wakati huohuo hospital za wilaya na mikoa zikiboreshwa katika kuwa na wataalam, majengo na vitendea kazi vingine.

Kwa mfano kanda ya kaskazini ukiwa unatibiwa mount meru hospital unaweza kutumwa kufanya vipimo kcmc na kurudisha majibu na ukapata matibabu kama ilivyo kwa hospitali za mkoa kama kibaha ambapo mgonjwa anaweza kupelekwa mloganzila au amana kwa uchunguzi zaidi au muhimbili.

Mimi sio mbobezi kwenye sekta ya afya ila tulikotoka palikua pagumu jamani enzi zile unafikishwa hospitali hujitambui unalazwa chini hazikua na tumaini, tulipo pana ahueni na tunapoenda pana mwanga zaidi
 
Swali langu kwa wizara ya afya kwa nini hospital nyingi zinakataa volunters? Ikiwemo Benjamin Mkapa?
 
Hivi Tanzania kuna Corona ?
 
Hivi mbona siku hizi NHIF wanaendelea kupunguza dawa, nimeandikiwa dawa ya duphaston mara kadhaa, lakini ukienda dirashani wanakwambia imeisha nenda kanunue.

Kuna siku nilienda hospitali moja ya private wakaniandikia kwenye fomu ya bima nikanunue pharmacy wao hawana, nilitembea pharmacy zote kubwa zinazojulikana nikiwaonyesha ile karatasi ya bima wakaniambia hawana hiyo dawa.

Basi nikamtuma mtu akaninunulie kwa cash kwenye phamarcy mojawapo nilizotembelea, Basi yule mtu alipewa hizo dawa na ziligharimu 75000/ kwa dose. Sasa hii inamaanisha nini jamani, nini maana ya kuwa na bima sasa. Wizara tunaomba mtusaidie kwa hilo.
 
Ajirini na waphamacia jmn maana wengi wanaishia kuuza dawa za kutoa mimba mtaani
 
Suala la Wazee bado ni changamoto. Lile dirisha la Wazee ndani hakuna Daktari. Sera ya Wazee ya mwaka 2003 hadi leo hamjaitungia Sheria, hivyo kusema Wazee watatibiwa bure si kweli.

Ni lini mtawakumbuka hawa Wazee ambao masuala yao yapo ndani ya Wizara hii?
 
Asante kwa kaz yenu nzuri. Swali langu ni kuwa, mgonjwa anapoambiwa alete damu(watu wa kuchangia damu) damu anayoongezewa mgonjwa inakuwa ni ile iliyoletwa na watu wa mgonjwa?

Nina mgonjwa katika hospital ya litembo iliyoko wilayan mbinga mkoa wa ruvuma, mgonjwa wangu amefanyiwa upasuaj, baada ya upasuaj wakasema mgonjwa inatakiwa kuongezewa damu. Ili damu iongezwe ni lazima tulete watu wa kutoa damu. Hili suala lipoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…