Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Hivi kwenye Hiyo wizara
ile ya maendeleo ya jamii,wazee na watoto mmeifukia au?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz

Official Blog www.afyablog.moh.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfyaView attachment 1588107
Suula la NHIF katika huduma za saratani ni kero.Nimekata bima ya 1.5 amilioni ila naambiwa kamwe sitopata huduma za saratani
 
wekeni dawa za kutosha ktk Hospotali ya Mloganzila,pia Mhe. Rais alishaelekeza kuwa Madaktari bingwa wote wapatikane ktk hospotali hiyo muda wote.

Hospotali ya mloganzila ni tegemeo kubwa la wana Dsm na Mikoa yote ya Tanzania na hata nchi jirani hivyo tafadhali lindeni hadhi ya Hospotali hiyo maaana serikali imewekeza ktk majengo makubwa na ya kisasa hivyo lazima huduma iendane sambamba na muonekano, inaonekana bado wataalamu wamelundikana Muhimbili ya upanga wakati kuna nafasi ya kutosha ktk jengo la mloganzila, si haba ila mipango mizuri inahitajika zaidi.
 
Bado Kuna double standards kwenye hosp za govt. Hii inashusha morale. Work on this
 
Bado Kuna double standards kwenye hosp za govt. Hii inashusha morale. Work on this
Kwa kusema tu hawajambo ukija kwenye upande
Wa masilahi utasikia hapa kazi tu ukitaka Ng'ombe akupe maziwa mengi mlishe vizuri basi
Kumbuka hii kazi ngumu sana cha ajabu hilo
Hawalitambui kabisa kila ucheo ni hapa kazi tu
Madaktari wetu wanafanya kazi sana lakini ki
Maslahi wana hali mbaya mno
 
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kuna tatizo kubwa la dakitar bingwa wa masikio na koo ila sijui mnachukuwa jitihada gan maana kwa special clinic ya mwezi wa kumi hilo tatizo lilikuwa tatizo kubwa
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz

Official Blog www.afyablog.moh.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfyaView attachment 1588107
Hospitali ya mloganzila kuna urasimu sana ,watumishi hawalipwi stahiki zao, wapo waliohamishwa kutoka sehemu mbalimbali toka mwaka 2017 mpaka leo hawajapata stahiki zao, pia na stahiki zingine kama mda wa ziada watumishi wanada stahiki zao za miezi 10-12, serikali chunguzeni uongozi wa hii hospital
 
Hospitali ya mloganzila kuna urasimu sana ,watumishi hawalipwi stahiki zao,wapo waliohamishwa kutoka sehemu mbalimbali toka mwaka 2017 mpaka leo hawajapata stahiki zao,pia na stahiki zingine kama mda wa ziada watumishi wanada stahiki zao za miezi 10-12,serikali chunguzeni uongozi wa hii hospital
Hii ni kila sehemu watumishi wanapata tabu sana danadana ni nyingi mno hakuna moyo
Wakazi
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz

Official Blog www.afyablog.moh.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfyaView attachment 1588107


Naomba kufahamu jambo moja;
Mgonjwa akienda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kadi ya bima ya afya anatozwa gharama za kupimwa typhoid, akiwaambia mimi nina bima wanamwambia hawaruhusiwi kutibu kwa bima kwakuwa wao siyo hospitali inayoruhusiwa kutoa huduma hiyo.

Swali:
  1. Kwanini Wizara inaruhusu vituo binafsi kupima typhoid wakati wao siyo hospitali?
  2. Kwanini Typhoid inapimwa kwenye vituo hivyo kwa dakika chache wakati inasemekeana sampuli ya typhoid inatakiwa ikae kwa saa 24?
  3. Wizara ya Afya inalitambua suala la vituo vya afya kupima typhoid wakati sheria haiwaruhusu?
  4. Kwanini wagonjwa hunyimwa huduma ya baadhi ya dawa kwa kisingizio cha kwamba maduka hayo hayaruhusiwi kutoa dawa hizo wakati dawa hizohizo unazipata iwapo utatoa cash katika duka hilohilo?
 
HABARI natumaini mnaendelea na kazi vyema nilikuwa naomba kuuliza kuhusu AFYA najua imegawanyika katika vitengo vingi ili ikamilike neno afya kama maabara, famasi, udaktari n.k

sasa swal langu katika kutoa ajira serikalini kwanini uoande mmoja tyuu ndo huwa unaoata nafasi kubwa kuliko sehemu nyingne (UDAKTARI) kwa mtazamo wangu naona kama hiii inafanya kada zingne kuwa na vijana wengi mtaani hawana ajira na pia kuacha kukosa ajira tyuu wafanyakazi wengne wanazidiwa kazi mfano unaenda kupima maabara unakuta na foleni kubwa ukiangalia ndani ya hiyo maabara kuna mtu mmoja tuuu mfano wa pili unaenda katika dirisha la kuchukulia dawa unakuta kuna muhudumu mmoja tyuuu na nje kuna foleni zaid ya wagonjwa 15 wanasubili huoni hii ni kuwazidishia majukumu watu wengne

OMBI LANGU

Naomba wizara ya afya muangalie utoaji wa ajira kwa kada zote zinazohusu afya kama mnavyotoa ajira kwa madaktari

mfano hai

mimi nimemaliza diploma ya famasi yan phrm.technician na nina leseni yangu lkn hadi leo sijasikia chochote kuhusu ombi la ajira kuhsu kada ya famasi
naomba kuwasilishaaa
 
Hivi mnahabari jinsi gani wasafiri wanavyo taabika katika maabara ya taifa kwa covid certificate, watu wamesha cancel safari zaidi ya mara mbili vyeti havipatikani kwa wakati, wageni pia hawajasalimika, ni jambo la kutia aibu kama hata kutoa karatasi tu ya vipimo vya covid ni issue, hivi hili taifa mnalipeleka wapi?, mbona kila kitu kinakua ni opportunity ya kuadhibu badala ya kusaidia watu?, hakuna hata kiongozi mmoja anaepita kukagua utendaji wa maofisa wenu na kujionea jinsi watu wanavyo taabika kupata hiki cheti, mnaziwekea idadi ya watu hospitali binafsi ili maabara za serikali zipate pesa huku uwezo hawana, hii serijali lini itaachia watu binafsi wafanye kazi badala ya kutaka kushindana nazo kugombea kipato,?
 
HIVI MNAHABARI JINSI GANI WASAFIRI WANAVYO TAABIKA KATIKA MAABARA YA TAIFA KWA COVID CERTIFICATE, WATU WAMESHA CANCEL SAFARI ZAIDI YA MARA MBILI VYETI HAVIPATIKANI KWA WAKATI, WAGENI PIA HAWAJASALIMIKA, NI JAMBO LA KUTIA AIBU KAMA HATA KUTOA KARATASI TU YA VIPIMO VYA COVID NI ISSUE, HIVI HILI TAIFA MNALIPELEKA WAPI?, MBONA KILA KITU KINAKUA NI OPPORTUNITY YA KUADHIBU BADALA YA KUSAIDIA WATU?, HAKUNA HATA KIONGOZI MMOJA ANAEPITA KUKAGUA UTENDAJI WA MAOFISA WENU NA KUJIONEA JINSI WATU WANAVYO TAABIKA KUPATA HIKI CHETI, MNAZIWEKEA IDADI YA WATU HOSPITALI BINAFSI ILI MAABARA ZA SERIKALI ZIPATE PESA HUKU UWEZO HAWANA, HII SERIJALI LINI ITAACHIA WATU BINAFSI WAFANYE KAZI BADALA YA KUTAKA KUSHINDANA NAZO KUGOMBEA KIPATO,?
Salaam Ndugu Ali Isaac.

Kwanza pole sana kwani sio nia ya Wizara au Serikali kuwatesa wananchi wake ndiyo maana kwa waliofika Maabara siku za hivi karibuni wataona kuna maboresho yamefanyika ukiwemo utatuzi wa changamoto ya maliwato zilizokua hazitoshelezi, huduma ya watumishi maalum wa kusikiliza mteja mara ufikapo na kuelekeza hatua stahiki, n.k.

Lakini pia Wizara kupitia Mganga Mkuu wa Serikali tarehe 14.01.2021 katika kuendelea kutatua changamoto hizi kwa wananchi wake ilitoa mwongozo wa uchukuaji sampuli na upimaji wenye maelekezo yote muhimu. Aidha, vituo vya uchukuaji sampuli viliongezwa ili kuondoa kabisa kero hii hasa katika maabara hii ya Taifa.

Ni tumaini letu tuko pamoja na tunawashukuru sana kwa maoni, ushauri, malalamiko na michango yenu kwani inayusaidia sana kujua wapi pana shida na kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka. PAMOJA TWAWEZA, KAZI IENDELEE.
 
HABARI natumaini mnaendelea na kazi vyema nilikuwa naomba kuuliza kuhusu AFYA najua imegawanyika katika vitengo vingi ili ikamilike neno afya kama maabara, famasi, udaktari n.k sasa swal langu katika kutoa ajira serikalini kwanini uoande mmoja tyuu ndo huwa unaoata nafasi kubwa kuliko sehemu nyingne (UDAKTARI) kwa mtazamo wangu naona kama hiii inafanya kada zingne kuwa na vijana wengi mtaani hawana ajira na pia kuacha kukosa ajira tyuu wafanyakazi wengne wanazidiwa kazi mfano unaenda kupima maabara unakuta na foleni kubwa ukiangalia ndani ya hiyo maabara kuna mtu mmoja tuuu mfano wa pili unaenda katika dirisha la kuchukulia dawa unakuta kuna muhudumu mmoja tyuuu na nje kuna foleni zaid ya wagonjwa 15 wanasubili huoni hii ni kuwazidishia majukumu watu wengne

OMBI LANGU

Naomba wizara ya afya muangalie utoaji wa ajira kwa kada zote zinazohusu afya kama mnavyotoa ajira kwa madaktari

mfano hai

mimi nimemaliza diploma ya famasi yan phrm.technician na nina leseni yangu lkn hadi leo sijasikia chochote kuhusu ombi la ajira kuhsu kada ya famasi
naomba kuwasilishaaa
Wizara ya afya tunaomba pia mfanye tathmini juu ya bachelor ya medical laboratory science.
Lab scientist (degree) ni wengi lakini ajira hakuna na chache zinazotoka ni diploma na certificates tu.

isifikie mahala watu wakajuta kwanini walisoma bachelor wakaona bora wangesoma diploma ama certificate maana ndo ajira nyingi zinazotoka upande wa Kada ya maabara mpaka kwenye private sector Kwa siku hizi.
 
Muhimbili recently kumekuwa na suala la mtandao wa internet kukatika kila inapofika saa saba mchana na kuendelea,jambo ambalo linasababisha huduma muhimu kusimama.

Nimepeleka mgonjwa OPD kule almost two weeks ikifika saa saba mtandao unakata,wagonjwa ni wengi wanawaambia warudi kesho yake, ikifika kesho wanakudai tena 20k ya kumuona daktari, kama umepoteza risiti basi inakula kwako maana wanasingizia mtandao haukuwepo so registration haijafanyika.

Na mimi nilienda nikilipia cash, sijajua hao wa bima hali inakuaje maana wale ndio wanazungushwa hadi huruma yaani, mara mtandao,mara sijui bima hii haina coverage ya ugonjwa huu..mara hili..mara lile!

Mgonjwa yeyote ni binadamu anayehitaji huduma ya haraka, anapokutana na situation ya hivi, kukosa matibabu kwa zaidi ya saa 24 au wiki ni kumuumiza au kumpoteza kizembe kabisa.

Mpaka tunajiuliza pale mtandao unakatika kweli au kuna mengine yanalazimishwa kuendelea?!
 
Wizara ya afya ijikite zaidi kwenye kinga kwa njia ya kuelimisha jamii kwa kuitumia idara ya maendeleo ya jamii. Badala ya kujikita kwenye tiba na kuitenga idara ya maendeleo ya jamii.

Hii itasaidia kupunguza msongamano wa watu wanaougua magonjwa ya kijinga kwenye zahanati zetu.
 
Wizara ya afya ijikite zaidi kwenye kinga kwa njia ya kuelimisha jamii kwa kuitumia idara ya maendeleo ya jamii. Badala ya kujikita kwenye tiba na kuitenga idara ya maendeleo ya jamii. Hii itasaidia kupunguza msongamano wa watu wanaougua magonjwa ya kijinga kwenye zahanati zetu.
Salaam Tausi.

Ni wazo na maoni muafaka, tunayapokea na tuahidi tutaongeza jitihada zaidi katika utekelezaji wake. Wizara hii ni moja (Afya & Maendeleo ya Jamii) na tunashirikiana kwa karibu sana kama wizara maana Maendeleo ya Jamii kwa uasili wa kazi zake inakutana na jamii moja kwa moja kuanzia chini kabisa.

Hivyo tunatambua kuwa kuna sehemu ya maradhi ni ushauri na kuzungumza tu mtu anakaa sawa anakua hana uhitaji wa kufika Hospitali ambapo anaweza akafanyiwa vipimo na asibainike kuwa na ugonjwa wowote kumbe ni tatizo la kimsongo wa mawazo na hivyo kuhitaji msaada wa ushauri wa kijamii zaidi.

Tunashukuru sana kwa maoni yako.
 
Muhimbili recently kumekuwa na suala la mtandao wa internet kukatika kila inapofika saa saba mchana na kuendelea,jambo ambalo linasababisha huduma muhimu kusimama.Nimepeleka mgonjwa OPD kule almost two weeks ikifika saa saba mtandao unakata,wagonjwa ni wengi wanawaambia warudi kesho yake,ikifika kesho wanakudai tena 20k ya kumuona daktari,kama umepoteza risiti basi inakula kwako maana wanasingizia mtandao haukuwepo so registration haijafanyika.Na mimi nilienda nikilipia cash,sijajua hao wa bima hali inakuaje maana wale ndio wanazungushwa hadi huruma yaani,mara mtandao,mara sijui bima hii haina coverage ya ugonjwa huu..mara hili..mara lile!Mgonjwa yeyote ni binadamu anayehitaji huduma ya haraka,anapokutana na situation ya hivi,kukosa matibabu kwa zaidi ya saa 24 au wiki ni kumuumiza au kumpoteza kizembe kabisa.Mpaka tunajiuliza pale mtandao unakatika kweli au kuna mengine yanalazimishwa kuendelea?!
Ndugu Kerubi salaam.

Aksante sana kwa mrejesho wako. Tunalifanyia kazi. Usisite kutujuza tena mara utakapoona hali hiyo bado inaendelea kwani si mazingira rafiki katika utoaji huduma ingawa nyakati nyingine mtandao unakua na shida za hapa na pale. Wataalamu wetu wanalifanyia kazi.

Aksante.
 
Back
Top Bottom