Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Wizard ya Afya Special Thread mko vizuri sana mnajibu maswali na maoni ya wadau kwa muda muafaka, binafsi nawapa hongera na nawaomba endeleeni hivyo kwani changamoto kubwa kabisa kwa nchi maskini ni afya, maoni yangu
1. Wekeni pesa ya kutosha kwenye tafiti za madawa ya kienyeji mfano ni hii corona

2. Boresheni maslahi ya wafanyakazi wenu kweli kabisa rushwa itapungua na ufanisi utaongezeka

3.Wawezesheji wazalishaji wa ndani wa madawa na vifaa tiba kwa kuwapa ruzuku au kuondoa ushuru.

4.Boresheni bima zile rafiki kwa mtumiaji mfano kama hujatumia bima mwaka unafuata unapata punguzo au wanakupandi daraja

5. Vifo vya mama wajawazito na watoto wekeni kipaumbele hii ni mbaya
6.
7
8. Mambo ni mengi ila tumieni wataalam wa ndani na ikibidi wa nje kutatua matatizo na kufanya tafiti za tibabu
 
Matabibu wa kibongo wanataka mpaka mgonjwa aende hospitali yu hoi anatapika damu ndio wanashughulika nae haraka,ila ukiwa mgonjwa ambae bado unajimudu hawakuzingatii utapigwa kalenda na kusumbuliwa sana unless utoe hela za pembeni,in fact wanakugeuza dili mpaka upate huduma ushaliwa sana.

Tabia hii inasababisha watz wengi hawapendi kwenda mahospitalini mpaka wawe hoi,na tunapoteza nguvu kazi ambazo tungeweza kuziponya kwa kuwahi tiba mapema.

Wizara kemeeni tabia hii,kila mgonjwa ajae hospitali anastahili tiba haraka,awe mahututi,awe hatua za awali,wote wanapaswa kupewa huduma za haraka maana kuna maana kumponya mtu mahututi haraka,na pia kuna maana kumpa huduma ya mapema mtu aliyewahi ugonjwa kabla haujafika stage mbaya,vyote ni muhimu kwa maadili na taratibu za tiba.

Tuache kuwazungusha na kuwanyanyapaa na kuwageuza "dili" watu wenye hekima ya kuwahi kuja hospitali mapema mpaka tuwaone wanaanza kuumwa sana ndipo tunakuwa na attention,hii sio medical practice ambayo ni ethical.

Mnapenda taifa la wagonjwa mahututi?

Najua kuna changamoto ya vifaa tiba na wafanyakazi wachache sekta ya afya,ila hii sasa inakuwa ni kisingizio hata pale pasipo na changamoto,yaani ishakuwa utamaduni,mpaka mtu awe hoi ndio watu wanachangamka nae kwa haraka.

Mimi nimeshawahi kupigwa kalenda hospitali ya serikali nikiwa na jino lililotoboka nikazungushwa hadi lilipoanza kuwa na infection na kuvimba shavu ndipo nikapewa huduma kwa wakati,na mda napewa huduma jino lingine la upande wa pili nalo likawa limeshapata maambukizi ikawa shughuli ya kutibia magego mawili yote ya juu kulia na kushoto na yote yanauma yanastahili tiba ya haraka,ilikuwa patashika,hata ujui ufanyeje ili ubakishe moja la kutafunia msosi kwa mda.

Nilipochunguza na kuuliza jamaa zangu madaktari wazoefu wakaniambia siku nyingine ukiwa na case ambayo sio serious sana usiende hospitali za serikali mindset yao ni kujali mtu akienda hoi,kama bado mzima mzima bora uende private hospital,wao hawabagui mtu.

This is not good guys,wabaneni watu wenu waache utamaduni huu mbovu.

Mgonjwa ni mgonjwa tu,awe kwenye wheel chair,au aje ana drive mercedec benz yake mwenyewe,wote ni wagonjwa wanahitaji huduma yako YA HARAKA wewe daktari ili uponye nguvu kazi ya taifa,kwa mahututi unaokoa uhai,na kwa early stage ukimtibu unawahi kuzuia tatizo kuwa kubwa na baya zaidi,vyote vina maana kitabibu na kibinadamu.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
kitendo tu nyie kujiunga humu ni maoni tisha pitie Uzi mbalimbali kwenye jukwaa husika,mtapata maoni ushauri na mapendekezo
 
Na mimi nina swali hilo hilo. Ni dhahiri corona sasa imekuwa kitega uchumi. Nilikwenda Aghakan tarehe 15 Januari 2021 kupima. Wanakuambia ulipe Tsh 360,000 (au kiasi hicho kwa fedha ya kigeni) na baada ya malipo ndipo wanachukua sampuli za kwenda kupima. Majibu baada ya saa 48. Serikali nayo imepandisha kutoka US$50 hadi US$100. Jee, ni kitu gani kilichofanya gharama iongezeke mara mbili kama nyenzo zinazotumika kupima ni zile zile?
Kutoka 40,000 Oktoba 2020 hadi 300,000+ January 2021 ?
 
Salaam Ntwale.

Tunashukuru sana kwa swali lako. Tunaomba utambue kuwa hakuna dawa iliyoondolewa katika huduma ya NHIF katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika ngazi zote. Niwaombe tu, ikitokea wewe au mwanachama yeyote amepata au kukutana na changamoto yoyote juu ya huduma zitolewazo na NHIF tunaomba sana awasiliane nasi tuweze kumsaidia.

Tafadhali sana, utupigie tu kwa namba 0800110063. Tumeboresha Afya Nchini, na kazi inaendelea kuwasogezea zaidi huduma wananchi karibu na maeneo yao wanayoishi.

Aksante.
Hapa mmejibu kisiasa! Waambie wananchi juu ya utofauti wa vifurushi vya Bima, mf kuna NAJALI AFYA, TIMIZA na WEKEZA!

Je, mtu aliyelipia Tsh 192000 kwa kifurushi cha Najali atapada dawa zote sawa na mtu aliye na Bima ya Wekeza amelipa zaidi ya 500,000? Let us be open na tuepuke double standards!
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Waziri wenu kwa kweli aache u-Kangi Lugola na afanye kazi zake kulingana na Taaluma yake, Maigizo hayatakiwi kwenye nafasi hiyo...anaboa, akitumbuliwa asiseme hatukumuonya!
 
Wekezeni kwenye misingi ya Primary Healthcare..kinga mmeisahau kabisa wakati wataalamu wake wamejaa mtaani..kujenga hospitali kuongeza bajeti ya madawa sio suluhisho la afya kwa watanzania.

Primary Healthcare approach ni muhimu sana kutokomeza na kupunguza magonjwa nchini.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Walikuja humu wakijua kuna mazumbukuku. Maswali machache wamezimia kabla ya kutoa mmajibu. Serikali jipangeni kujibu maswali haya.

Msione watanzania wanatembea kama mabubu mkajua hawana hoja juu yenu. Wanakosa tu majukwaa ya kusemea. Huu ni mfano kwa wizara moja.

Kuna maswali ya wizara zote ila pa kusemea hakuna.
 
Poleni na kazi watendaji na watalaam wetu. Mi naomba ile namba ya Amana referral Hospital mlioweka kama contact number mnazoweka ziwe zinafanya kazi, mfano namba +255 22 286 1902 ukipiga unapata majibu " Sorry the call is not through, because the callee has not paid the bills" tunajua mnatumia namba za mkononi kwa ajili ya kazi za ofisi lakini hii ni kero kubwa sana

Karibu Idara zote za serikali wana tatizo hilo, Ila kwa muhimu wa TAASISI yenu tunaomba mtuwekee namba inayofanya kazi , maana kama ni bili hailipwi leo wala kesho. najua itachukua muda mrefu kutatua hilo ila naomba tu utujulishe kama huu ujumbe umeusoma na unashughulikia, itatosha, sisi tutasubiri hata kama mtarekebisha 2021/ - 2030 hatujali tumevumilia mengi sana.
Madaktari na manesi nawashukuru na kuwapongeza kwa kazi ngumu mnayoifanya kutuhudumia sisi.Watanzania.Japo Wizara ya Afya imewasahau kwa muda mrefu bila kushughulikia masilahi yenu iko siku.

Swali langu Wizara ya afya,katibu mkuu,kila siku Watanzania wanaambiwa kuwa matibabu ya wazee ni bure.Kiuhalisia wazee ndio waliotufikisha hapa tulipo.Inakuwaje kuwaongopea kuwa matibabu yao ni bure kumbe wakienda hosipitali wanatelekezwa hapo.

Naomba wizara ya afya ituambie kwa wazi na kina,wazee wanapatiwa matibabu bure kama mnavyosema?

Kama ni ndiyo kwenu,lakini kwa wazee sio.Wazee wanakwisha kwa kukosa matibabu.Huo ndio ukweli wenyewe.Tafadhali tujulishe.
 
WIZARA YA AFYA KUTUMIA UVUMBUZI WA CHUO KIKUU CHA SUA KWA KUTUMIA PANYA WENYE UWEZO WA KUGUNDUA VIMELEA VYA KIFUA KIKUU

Na Emmanuel Malegi-Morogoro

Wizara ya Afya imeshaanza kutumia teknolojia ya Panyabuku katika kubaini ugonjwa wa Kifua Kikuu (Tuberculosis ) kwa sampuli za wagonjwa wenye dalili hizo ili kuongeza uwezo wa kutambua vimelea hivyo hasa pale ambapo njia zingine zimekuwa zimeshindwa kubaini.


Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi ambaye alitembelea kitengo hicho cha APOPO katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Morogoro amepongeza mapinduzi kutoka kwa Wanasayansi Wazalendo ya kuwawezesha Panya buku wa Chuo Kikuu hicho kunusa na kubaini vimelea vya Kifua Kikuu katika sampuli za makohozi yanayoletwa hapo kwa ajili ya vipimo vya Kifua Kikuu, na ameelekeza kufikia mwaka huu huduma hii iweze kuzifikia zaidi ya Hospitali 100 nchini.


“Nawapongeza sana watafiti wa SUA kwa hatua ambayo mmefikia, kituo hiki baada ya kukitembelea tumeona kuwa kimekua kikifanya ugunduzi wa vimelea vya kifua kikuu kwa kutumia hawa Panya. Lakini pia wameweza kuwafundisha na kusambaza hiyo Teknolojia katika nchi mbalimbali kama vile Msumbiji na Ethiopia ambako wanafanya kazi ya kupima ugonjwa wa Kifua kikuu, na kwenye nchi za Cambodia na Angola ambako wanafanyakazi ya kutambua mabomu ya ardhini”. Amesema Prof. Makubi.


Prof. Makubi amesema Panya hao wana uwezo mkubwa wa kugundua vimelea vya Kifua Kikuu hata kwa mtu ambaye alifanya vipimo Hospitalini kama vile vya hadubuni (microscope) na mashine za kupima vinasaba mfano GeneXpert na vipimo vingine na vikatoa majibu kuwa hana TB, lakini panya hao wana uwezo wa kubaini vimelea ambavyo mashine za Hospitalini zinaweza zisibaini. Hii inaonyesha utumiaji wa panya hawa unaweza kusaidia kuongeza ugunduzi wa wagonjwa wengi zaidi. Panya mmoja anauwezo wa kugundua kama sampuli ina vimelea vya kifua kikuu kwa muda wa sekunde moja, na hupima sampuli za makohozi 100 kwa dakika 20 hivyo teknolojia hii inaweza kutumika hata kwenye upimaji wa sampuli nyingi kutoka kwenye kundi kubwa la watu (mass Screening) kwa muda mfupi.


Mganga Mkuu wa Serikali aliweza kushuhudia Panya ajulikanae kwa jina la Justine aliyeweza kupima sampuli 60 za makohozi ndani ya dakika tano na kugundua sampuli sita zenye vimelea vya Kifua Kikuu.


Mpaka sasa huduma hiyo inatolewa katika Hospitali 74 na kuweza kubaini wagonjwa 14,680 ambao hawakuweza kugundulika kwa njia za kawaida. Hii imesaidia wagonjwa 8,119 kuanza matibabu ambayo yamezuia maambukizi ya kifua kikuu kwa wanachi 81,190 hadi 121,785 ambao wangeweza kuambukizwa kutokana na mgonjwa mmoja ambaye hajatibiwa anaweza kuambukiza ugonjwa huu kwa watu wa karibu naye 10 hadi 15 kwa mwaka.



“Hatua hii inanipa faraja sana kama Sekta ya Afya kwa sababu dhumuni la Sekta hii ni kulinda afya za watu wake. Tunapopata kipimo kama hiki kitasaidia wananchi wengi kuweza kujua afya zao na matokeo yake tutaokoa wananchi wengi kwa kupata tiba na kufanya maisha yao yaweze kuwa marefu zaidi lakini pia tunapunguza uwezekano wa kusambaza ugonjwa huo kwa watu wengine”. Ameongeza Prof. Makubi.


Aidha, Mganga Mkuu huyo aliahidi kulifanyia kazi ombi la Mkuu wa Mradi wa kutambua Kifua Kikuu kupitia Panya Buku Dr. Georgies Mgode la kuitambua Teknolojia hiyo ya Panya katika Mwongozo wa Kutibu Kifua Kikuu hapa nchini.


Pamoja na hayo, Mganga Mkuu huyo wa Serikali ameelekeza Chuo cha SUA kuendelea kushirikiana na Wizara ya Afya na NIMR katika kuboresha huduma za Sekta ya Afya katika maeneo ya kubaini magonjwa, kuanza kutengeneza chanjo, kuimarisha tiba asili, kupanua tafiti za magonjwa, kutoa mchango katika kuboresha lishe za wananchi na kushirikisha sekta mbalimbali katika kuboresha huduma za afya nchini (One Health Approach).


Kwa upande wake Mkuu wa Mradi wa kutambua Kifua Kikuu kutumia Panya Buku Dr. Georgies Mgode amesema kuanzia mwaka 2007 mpaka Desemba 2020 mradi huo umeshapokea na kupima sampuli za makohozi 559,428 kutoka kwa wahisiwa wa kifua kikuu 315,476 huku wakiongeza utambuzi wa wagonjwa wa kifua kikuu kwa asilimia 40 katika maeneo ya mradi. Huduma hii ikisambaa maeneo mengi nchini basi Tanzania inaweza kuondokana na janga la ugonjwa huu kwani tayari Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma unatambulika duniani kuwa mfano katika mapambano dhidi ya kifua kikuu.


Nae Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA Prof. Raphael Chibunda amemshukuru Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi kwa kuonesha nia ya Wizara ya Afya pamoja na SUA kuweza kushirikiana kuzalisha wataalamu na kufanya tafiti mbalimbali ambazo zitaweza kusaidia sekta ya afya. Aidha Prof. Chibunda, ameahidi kuwa SUA itaendelea kutoa mchango wake katika tafiti mbalimbali za kuboresha huduma za afya nchini. Ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuimarisha chuo hicho katika uboreshaji wa miundo mbinu, vifaa na mafunzo kwa watalaamu.


MWISHO
IMG-20210225-WA0038.jpg
IMG-20210225-WA0041.jpg
IMG-20210225-WA0042.jpg
IMG-20210225-WA0040.jpg
IMG-20210225-WA0043.jpg
IMG-20210225-WA0039.jpg
 
Naisihi wizara ya fya iangalie kwa upana swala la korona. hao wanaolazimisha tuchukue chanjo n=wana tamaa ya hela na pia wanatataka yubaki na madhara makubewa ili ajenda yao ya depopulation itimie.

Tukumbuke tanzania ni nchi yenye maklighafi nyingi sana. nahisi chanjo itakayoletwa Tanzania itakuwa ina deadly effects,...ili kuhakikisha watanzania wanpukutika haraka.

Wazungu wanaitaka tanzania. washauziwa rwanda sasa wanataka tanzania by all means.

Wanaendeleza ukoloni wao hukuu afrika kwa mgongo wa chanjo...mikopo..msaada...nakadhalika, Tanzania fungueni macho.

Mkataeni mkoloni mamboleo...angalieni na mchambue kwanza jambo kabla ya kukubali. Mnadhani wazungu wantupenda sana eeh...africa ndiyo imeshililia uchumi wa ulay na america ndiyo maana wangependa kwa njia yey=ote ile tusisonge mbele...wametuletea magonjwa na mengien hayatibiki sasa wakaona hatuiahi wakaamua kuja na kitu ambacho wangependa kaulazimisha kila mtu achukue...ili lengo lao litimie...tusiwe wajing Mungu ametubariki sana Tanzania na tusijifanye ni wakarimu sana...kukubali kila kitu
 
Tozo za kupokea matibabu wangojwa wanafika hospital PF3 ziondolewe zinaleta usumbufu sana kwa wagojwa wanafika kupokea matibau Katika hospital zetu ila usumbifu mkubwa Sana
 
MALALAMIKO: KUHUSU KUCHELEWA KWA MAJIBU YA COVID TEST.
Mbali na gharama kuwa kubwa, Majibu ya covid test yanachelewa sana. Wanasema ni baada ya saa 24 lakini siyo, ukipima leo unapata Majibu kesho kutwa.

Naomba wizara tubadilike jamani, tuongeze maabara zingine. Tuko nyuma sana ukilinganisha na nchi zingine. Ambazo kuanzia saa 3 haizidi saa 12 unakuwa umepata Majibu.

Inatuletea shida sana kwa tunaosafiri na hasa ukipata dharura, au ukitoka mbali kijijini na inatakiwa kusafiri nje ya nchi.

Na muda ukiwa tunasubiria Majibu unakosa amani kama utayapata kwa wakati au lah. Kwa ujumla inatuletea shida sana.

Sioni what is the big issue maabara zinazo aminika zisiongezwe kusaidia. Kama vile CLINA LANCET LABORATORY.
Tunaomba mlifanyie kazi tafadhali sana.
 
Habari za wewe ..? Natumaini uko salama na unaendelea kupambania haki za raia wa Kitanzania.
Sisi ni wanafunzi wa kitengo cha usingizi (Anesthesia)

MNH six months course tuliopo chini ya ufadhili wa MOHSWGD wakishirikiana na TAMISEMI, Wametugawa kwenye hospitali mbali mbali zikiwemo BMC, BMH, IFAKARA, MNH, MOI, KCMC kutegemeana na kanda tunayotoka,
Tumetokea makazini na wengi wetu tulioajiriwa mwaka 2015. Mchakato wa kutuselect haukua rafiki yani niseme tu wengine hawakua wamejipanga kusoma hii couse ila kwa vile boss kakuchagua huna budi kwenda huku unaambiwa gharama zote utagharamiwa.

Kiufupi wengi hawakua wamejipanga kwa jambo hilo sema sababu kama attractive packages na kubadili mazingira , nadhani unaelewa watumishi wa vijijini tunakua sawa na sehemu tuliyopo.

Tumeripoti mwanzoni mwa Dec2020 tukitegemea in btn that month and jan2021 tutakua tumeshapewa stahiki zetu. Tumeendelea hivo huku tunapewa ahadi nzuri nzuri mara watuambie nyie ni watumishi kwo hamna shida, sawa ni watumishi lkn hiyo salary yangu sikua nmeipangia niitumie huku na pia tayari tuna familia plus ndugu zetu vijijin , nadhani unaweza kuona ni kiasi gani tunavyoishi maisha magumu tena tuko kwenye miji mikubwa.

Tumeendelea hivo kuwakumbusha mpaka mnamo mwezi wa march2021 tukalipwa laki sita out of 2160,000/- katika mchanganuo wa matumizi 10k per day, yaani tumekaa miezi mitatu ila tunalipwa miezi miwili haikumake sense bt kwa vile tulishavua nguo ikatubd tuoge tu.

Tumeendelea kufuatilia kwa Ntuli na Mwenzie Bakari bila mafanikio zaidi ya kupewa vimaji na kuwasubiria afu wanakuja kukupa sababu zisizo na vichwa as if sio haki yetu.

Leo tumebakiza miezi miwili kasoro lakini bado hatujalipwa fedha za kujikimu na dalili iliyopo ni kudhulumiwa, wamefuatilia TAMISEMI tangu saa 2 asubuhi wanakuja kuingia ofisini kwa Ntuli sa8 mchana umechoka unajibiwa mtandao mbovu kesho mambo yatakua mazuri.

Wakumbuke mpaka kufika hapa tumekopa,tumeuza mifugo,tumeuza mashamba na wengine wameiba pia. wengine wameshindwa kuwalipia ada watoto wao na ndugu zao kisa utapeli huu uliofanywa na TAMISEMI wakishirikiana na MOHSWGD.
 
Hivi wizara ya afya haioni wagonjwa wanaohangaika kutokana na kukosa gharama za matibabu? Watoto wanahangaika na kuteseka kwa maumivu baada ya kukosa gharama za kutibiwa. Serikali angalieni hili.

Kweli bilioni 4 au 10 iwe sababu ya kuteseka kwa mtoto wakati pesa mnatumbua ovyo
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe mawasiliano@afya.go.tz

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
Tiba ya kimeo ni nn?
 
Hivi Wizara ya Afya huwa mnalenga kufikisha Ujumbe gani kwa Wananchi wa Tanzania pindi Mnapomtumia Msaniii MRISHO MPOTO kuwa balozi wa KAMPENI zenu mbalimbali za Kiafya ikiwemo hii inayoendelea NYUMBA NI CHOO.

Msanii MRISHO MPOTO sote tunajua FALSAFA YAKE anatembea PEKU PEKU na anapingana na UVAAJI WA VIATU/MALAPA hali ambayo Kiafya haikubaliki na Hata Wizara ya Afya ilipaswa iiipige VITA.

Lkn Inashangaza, kufikirisha, kughadhabisha na kuona kama mnafanya mchezo wa kuigiza na Upumbavu kwa Watanzania Wote kumsimamisha Msanii akiwa pekupeku kusimama jukwaaani kuhamasisha watu wazingatie Usafi wakati yeye Falsafa yake pale jukwaaani inapingana na kile anachokuwa anahubiri.

Watanzania wa Sasa sio wa mwaka 1970, kama Kuna 10% huyo Mpoto anawapa pindi mnampa hayo Makampeni acheni, Mnaitia aibu Wizara ya Afya na mnachofanya kinafedhehesha Watanzania wenye akili timamu. Wapeni kazi Wasanii kulingana na Wasifu wao na kile mnachofanyia kampeni.

Kwa Ujinga huu Ipo siku mtatuletea Wasanii akina Rayvann wenye kashfa za akina PAULA kufanya kampeni za Mimba za Utotoni au NIACHE NISOME. Badilikeni na Mfanye VETTING za Wasanii kabla ya kuwapa Ubalozi wa Kampeni husika, mnachemka sana.
Am over
 
Back
Top Bottom