Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Heheh, ila bwamdogo wacha umbeyaa
 
Hahaha ila bwamdogo wacha umbeyaa
 
Magufuli alimaliza hayo
 
Wizara ya afya upokeaji wa matibabu wa watoto chini ya miaka 5 bado ni.changamoto watoto wa umri wa chini ya miaka 5 bado upokeaji wa matibabu ni changamoto kwao hata mama mja mzito bado kuna changamoto.namna.ya upokeaji wa matibabu
How be specific
 
Naomba nijue hivi kama mtumishi anangazi ya cheti, akatumikia ile ngazi akapanda daraja kuchukua mshahara wa ngaz ya diploma,

badae akaenda kusoma akapata diploma ya secta yake ,akapnda daraja tena kabla ya kubadilishiwa muundo , swali langu je baada ya kubadilishwa cheo cha muundo inatakiwa ashushwe mshahara?

naomba kwaanaye jua anisaidie ndugu.
 
Hongera Serikali ya Tanzania kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta ya Afya.Serikali ya awamu ya tano na sita,imejenga hospitali nyingi za wilaya,vituo vya afya kwenye kata nyingi na zahanati kwenye vijiji vingi kwa lengo la kufikisha huduma Karibu na wananchi.

Ushauri
1.Serikali ipeleke madaktari, matabibu, wauguzi , wafanyakazi wa maabara na wafamasia ili kutimiza lengo la Serikali kupeleka huduma za afya kwa wananch, vinginevyo, majengo yatabaki kuwa white elephant.

2.Serikali ipeleke vitenganishi na dawa kwenye vituo vyetu.

3.kadi za Bima ya afya ziwe zinapokelewa kwenye vituo vya afya.
 

Ndio anatakiwa kushushwa!
 
Wizara ya afya simamieni wizara yenu ipasavyo hasa hospitalini, madaktari wanatorosha sana madawa na kwenda kuuza kwenye maduka binafsi. Huo ndio ukweli, tunalalama kila leo dawa hakuna ila wahujumu wakuu ni madaktari.
 
Kituo cha afya karume wilayan
Rombo hakina dawa saa 24/7
Ukiwa mgonjwa uandae na pesa ya kununua
Dawa sasa hii hospital ya kuna haja
Gani kuitwa ya government??
 

Wizara ya afya mimi kama mtanzania wa kawaida naomba ufafanuzi kuhusu Suala la ndugu wa mgonjwa kuchangia damu. Natambua Sera ya afya inayohusu damu salama inatamka ama imetoa mamlaka kwa kila hospitali kuweka utaratibu wa kukusanya damu.

Naomba huu ufafanuzi kutokana na tukio lilojitokeza hospital ya Musoma. Kuna mgonjwa ambaye alitokea wilaya ya Musoma vijijini kwa ajili ya matibabu, kama Familia tulijitahidi kwa kadili tuwezavyo ili ndugu yetu apate huduma, pamoja na changamoto za vifaa tiba katika hospitali ile, hospitali haina hata gloves, kanyula kila kitu nikununua madukani nje ya hotel.

Shida yangu kubwa ni kuwa ndg yetu aliongezewa damu chupa nne, Sasa amezuiwa kutoka hospitali akidaiwa damu chupa 12. Kwamba kila chupa inatakuwa kurudisha chupa Tatu. Je endapo watu wa kutoa hiyo damu hawatopatikana huyu ndugu hatotoka hosp?

Ajabu ni kwamba mimi na kijana huku Dar tumekuwa tukichangia damu bila kujali tumemchangia nani na mpaka kadi za uchangiaji damu tunazo.
 
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya,wiki iliyopita, imetoa tangazo la watumishi wa afya wakiwemo madaktari 10 wa kujitolea kwa kipindi Cha mwaka moja na watalipwa posho ya kijikimu wakati huo.

Ni suala zuri, ili kufanya huduma za afya kwa wananchi ziendelee,
-jambo la kujiuliza,ina maana Tanzania tuna madaktari wengi kuzidi mahitaji yetu, -Vituo vya afya vyote vina madaktari wa kutosha ,na Zahanati zetu Zina matabibu wa kutosha

-au serikali haikutenga bajeti ya kuajiri watumishi na dawa.

-Kama tatizo ni bajeti ya kuajiri watumishi na dawa,basi kuna tatizo la planners wetu.

-Ni sawasawa na kupanga kununua magari 200 bila kuweka provision ya ajira za madereva au gharama za uendeshaji.

Ushauri:
1). Serikali inapopanga kujenga miundombinu mbinu,ni vema wakapanga na suala la rasilimali watu na gharama za uendeshaji.

2). Serikali,(kama imejitosheleza na Madaktari), izungumze na nchi jirani (Kama south Sudan, Botswana au Comoro) tuanze ku-export huduma.

3). Serikali itenge bajeti ya kutosha kuajiri madaktari ,wauguzi,wafamasia ambao wamehitimu na kufaulu mitihani ya bodi zao (bodi ya madaktari (MCT),wauguzi na Famasia)
 
Swali langu mmsema kuchanja chanjo dhidi ya Corona ni hiyari mbona kuna baadhi ya kliniki zinazohudumia magonjwa sugu pale Muhimbili wanalazimisha wagonjwa kuchanja tena wanawapigia simu na kuwataka waende kuchanja hata kama sio tarehe yake ya kuhudhuria kliniki.
Imekaaje hii?
 
Hivi humu hata hawa maadamin wa huu uzi wapo kweli au wamshauterekeza.

#MaendeleoHayanaChama
 
Rushwa na uchafu umerudi KWA Kasi Sana mahospitalini!!je WIZARA hii inahitaji jpm Mwingine ILI irudi kwenye mstari!!?maana upigaji umerudi vituoni vya afya Sana tu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…