Wizara ya Afya yadaiwa kuhusika katika ufisadi wa bilioni 4.8

Wizara ya Afya yadaiwa kuhusika katika ufisadi wa bilioni 4.8

Sasa shida iko wapi hapo ? Wazungu wameleta Pesa za bwelele zimepigwa na watanzania kimkakati we unalia lia nini wacha wafaidi ili siku nyingine hao mabeberu wapungunze shobo juu ya bara la Africa.
Mara nyingine ukinyamaza utaficha mengi. Kwa akili yako hiyo pesa ilitolewa bure? Ni kodi yako, watoto na wajukuu zako itakayotumika kuilipa.
 
Rais Samia alithibitisha kwamba ndani ya serikali kuna mtandao mkubwa ambao unaiba fedha za umma. Nafikiri sasa Rais asilalamike tu, achukue hatua za kushughulika na mafisadi hao serikalini.

Mashirika ya kimataifa yanadaiwa kutoa fedha kwa ajili ya kufanya kampeni kuhamasisha wananchi wajitokeze kuchanja kwa kuwa baada ya chanjo za awali za COVID-19, watu waligoma kujitokeza kuchanja.

Wizara ya Afya chini ya Waziri Ummy Mwalimu inadaiwa kupokea kiasi cha TZS 4.8 bilioni kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kuchanja. Taarifa zinadai Clouds Media Group na E-Media (EFM & TVE) walipewa zabuni ya kuhamasisha.

Kwa kuwa kampeni ile haikuwa na maana tena isipokuwa kutafuta uhalali kwa wafadhili wa pesa hizo kupitia “uhamasishaji” ili kuzitafuna, wanadaiwa walilazimika kuzipelela fedha katika taasisi ‘well-known’.

Ni kama utakatishaji fulani hivi. Kwamba pesa zionekane zimefanya kazi ya kuhamasisha, na baadae wataandika vyeti feki na kutuma jumbe fupi za maneno kwa watu ambao hawajawahi kuchanja.

Taarifa zinadai E-MEDIA (EFM na TVE) walipewa kiasi cha TZS 1.9 bilioni ili kuandaa kampeni ya kuhamasisha kuchanja kupitia tamasha la muziki linaloitwa (Muziki Mnene). Wasanii wa muziki walitumika kama SHILOLE.

Wasanii hao wa uigizaji na muziki wakapewa kazi ya kuhamasisha na kutoa elimu ya afya na chanjo ya COVID-19 (wao waliita UVIKO-19). Tazama ukurasa wa Instagram wa SHILOLE, November 24, 2022.

Clouds Media Group (CMG) wanadaiwa kupewa TZS 800 milioni Via Benjamin Mkapa Foundation (chini ya Dkt, Hellen Senkoro Mkondya) kufanya kampeni. CMG walianzisha kampeni inaitwa ‘Ujanja ni Kuchanja’.

Benjamin Mkapa Foundation wanadaiwa kutoa TZS 800 milioni kwenda Clouds Media Group (CMG). Wao (BMF) walipokea fedha hizo kutoka wizara ya afya. Dr.Ellen Mkondya-Senkoro (CEO) ni rafiki wa UMMY.

Kampeni ya kuchanja ‘ikafariki kifo cha mende’ fedha zikatafunwa. Wizara ya Afya inadaiwa kuchukua taarifa za watu waliochanja awamu ya kwanza na kutengeneza vyeti feki kwamba wamechanja awamu ya pili.

Ukweli ni kwamba watu hao hawajawahi kukanyaga hospitali yoyote kutafuta chanjo ya COVID-19. Vyeti hivyo binadaiwa kusainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dr, Seif Shekalaghe (hayupo ofisini sasa)Kampeni haikufanikisha lengo la wafadhili. Watafanya nini kuonesha kwamba kampeni hiyo ilizaa matunda?

Taarifa zinadai Wizara ya Afya ikaamua kutoa ‘certificate of COVID-19 vaccination’ batili (feki).Wizara ya Afya wakaunda Bulk SMS Automation (mass text messaging) kupitia namba 199. Bulk SMS ni ni huduma inayowezesha kutuma idadi kubwa ya SMS kwa hadhira kubwa - mara moja.

Lengo la namba hiyo (199) ni kutuma ujumbe kuwajulisha kwamba wamefanikiwa kupata chanjo ya UVIKO-JANSSEN na unatumiwa na link ya cheti chako feki.

Wizara ya Afya inadaiwa kutoa ‘certificate of COVID-19 vaccination’ kutumia data za waliochanja awamu ya kwanza. Unapokea taarifa upo Makambako, Njombe umefanikiwa kupata chanjo Hanang.

Tatizo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wakati huo, Dr. Seif Shekalaghe atueleze watanzania, hiyo saini aliyoweka katika cheti feki cha COVID-19 ambacho watu hawakuchanja alipata maelekezo kutoka kwa nani?

Wizara ya Afya, kwanini mliwapa taarifa za uongo Shirika la Afya Duniani (WHO) kwamba watanzania wamechanjwa (full vaccinated) wakati sio kweli na serikali imeghushi nyaraka chini ya UMMY Mwalimu?

Wizara ya Afya kutoa vyeti feki (fake certificates) ambavyo vimewekwa saini ya Katibu Mkuu wizara ya Afya kuhalalisha wizi wa fedha za wafadhili linatosha kukueleza dhamira mbaya ya WAZIRI wa AFYA.

WIZARA ya AFYA inatoa nyaraka feki ili kuhalalisha wizi wa fedha za wafadhili na kuwadanganya watanzania itashindwa kuruhusu dawa zilizokwisha matumizi (expire) kutumiwa na watanzania?

Source: Martin Maranja Masese

Kama Samia akiwa Serious na kuacha Ushosti, Ummy anatakiwa kukaa pembeni immediately. Ufisadi umerudi kwa kasi, na Ummy anatajwa kwenye maeneo mengi yanayohusika na Ufisadi. Kuna jambo halipo sawa kwa Ummy na anatakiwa kuchunguzwa. Hata ishu ya NHIF na kitita chao…… kuna viashiria vya rushwa na ndio maana wizara chini ya ummy inapiga kampeni ya kuhamasisha kuwa kitita kipo sawa. Fuatilia viongozi wa wizara kwa makini kwenye media , Tv na redioni…….:

Ummy ameunda tume ya kupata maoni ya kitita. Kimsingi maoni yalitakiwa kuwa collected kabla ya kitita kuwa approved

Ipo shida Mahal tena kubwa chini ya uongozi
Wa Ummy ;

Mama anatakiwa awe serious na maslahi ya vinginevyo asigombee tena , anazidi kudidimiza nchi. Nchi imekuwa ya kihuni kila mtu anajipigia , ule uangalizi wa resourves za nchi haupo tena . Ni siasa hadi kwenye mambo ya msing

Ummy
Has to
Step
Down
 
Anajua sana kusukuma kete na ufisadi

Vyombo vya ulinzi na
usalama, mkiachia nchi hawa wanasiasa bila ya action

Tunarudi kwenye UFISADI MKUBWA zaidi ya ufisadi wa JK
Kinga yao hawa mafisadi ni kumsifia sn maza na kurudisha return kwa maza walichochuma
 
Wapigaji wa aina hii ndio wenye kuchukia hata kutajwa tu jina la magufuli. Eti januari makamba anaorodhesha mambo makubwa kumsifu samia ni pamoja na vita vya covid 19 kwa kukubali mikopo na kuletwa chanjo. Hao beberu wa kutengeneza pandemics feki wenyewe wanajua ni ujinga kuwakubalia uhuni wao uliyopangwa vizuri sana maana wanalofanya ni ubeberu wa kisasa.
Uzuri watu walimuamini magufuli nakujua covid ni uhuni mkubwa wa kimataifa kwa hivyo hawakujihatarisha kuchanja waligoma. Sasa madawa yanaozea kwenye bohari na hela zilizokopwa zinaliwa na magufuli haters. Mama mwenyewe aliwabariki wapigaji kwa kuwapa nguvu kwa kusema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake ya malisho. Sasa mama anatoa machozi ya mamba bure huku akijua mpango wake umefeli. Amelikoroga tembo basi alinywe.

Ila Biteko kamjibu ,

Jamaa hataki unafika. Kila kinachoonekana sasa ni nguvu ya JPM . Na mama hadi sasa hajaweza kukamilisha project nyingi za JPM.

JPM meant a lot kwa watanzania na alimaanisha mengi sana HASA ukiangalia uelekeo wa nchi kwa sasa.

JPM kaacha nchi petrol one liter ni 1700 now ni 3160.

JPM kaacha dola ni 2200 , now ni 2700

JPM kaacha hakuna shida ya upatikanaji wa dola, now kupata dola ni dili na utoe shiling nyingi

JPM kaacha miundombinu inakaribia kumalizika. Mwaka wa 3 sasa hakuna barabara hata moja iliyofunguliwa

JPM kaacha nchi haina tozo za miamala, now tozo ni kila kwenye muamala wa simu

JPM aliwapiga burn DP world kwasababu hawaku meet term za recruitement , JPM alitaka nafasi za ajira ziwe 60% by 40% na some of the highest positions za management zishikwe na watanzania; mama
Kawapokea bila terms zozote kuweka maslahi ya taifa Mbele. Tangu DP world waje, wametangaza kazi ngapi? Moja tu tena kama geresha

Huu upuuzi wa kuingiza mchele wa virutubisho pasipokuwa na msingi JPM asingeruhusu. Hatuna shida ya mchele wala virutubisho



JPM alimaanisha mengi kwa watz na hamuezi kuburial legacy yake, that man was a great man kuwahi kutokea and he will always be remembered
 
hapa ngoma droo! machanjo ya kiujanjaujanja yakakutana na maofisa wa wizara wajanjawajanja.
 
Back
Top Bottom