Wizara ya Afya yafafanua juu ya gharama za Mradi wa Hospitali za Rufaa Mawenzi

Wizara ya Afya yafafanua juu ya gharama za Mradi wa Hospitali za Rufaa Mawenzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuhoji juu ya Mradi wa Serikali kupewa fedha nyingi kuliko bajeti iliyopangwa na kuripotiwa kutokamilika, ufafanuzi umetolewa

Mdau alitoa mfano kwa kupitia Bajeti ya Wizara ya Afya 2024/25 iliyosomwa bungeni Mei 14, 2024 ambapo Mradi wa Uimarishaji ya Hospitali za Rufaa – Mawezi, ilisomeka Mradi ulihitaji Tsh. Bilioni 7 lakini ukapokea Tsh. Bilioni 12 na kwamba umefikia 86%.
Afya Wizara.png
Ufafanuzi umetolewa na Wizara ya Afya ambayo imewasiliana na JamiiForums na kueleza kuwa nyaraka ya awali ilikuwa na dosari na taarifa rasmi imerekebishwa na inapatikana pia katika Tovuti ya Bunge.

Wizara imeeleza kuwa gharama za Mradi wa Uimarishaji wa Hospitali za Rufaa Mawenzi utakaohusisha Ujenzi wa jengo la huduma za afya ya uzazi (Maternity block) ni Tsh. 17,423,559,565.00 na kiasi ambacho kimeshatolewa ni Tsh. 12,609,352,188.81

Ujenzi huo umefikia 86% ambapo sakafu ya chini na ya kwanza zinatoa huduma.


Hoja ya Mdau - Inakuwaje mradi unapewa hela zaidi ya walizoomba na haukamiliki?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bado kuujenga uwanja wa mabingwa wa muda wote Young Africans
 
Back
Top Bottom