Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Amesema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni 1.148 ambazo ni sawa na asilimia 64 ya bajeti iliyotengwa zinaombwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, amesema kuwa kati fedha hizo, fedha za ndani ya nchi ni shililingi Bilioni 789.45 na kiasi cha shilingi Bilioni 358.56 zinatoka kwa washirika wa maendeleo.
Mhe.Mchengerwa ameliambia Bunge kuwa, Wizara ya Afya imepanga kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 652.236 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambayo ni sawa na asilimia 36 ya bajeti iliyotengwa. Amefafanua kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi Bilioni 516, 323 ni kwa ajili ya mishahara ya Watumishi wa Afya na kiasi cha shilingi Bilioni 135, 913 zitatumika kwa ajili ya matumizi mengineyo.
“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali Watanzania na kuiwezesha Wizara ya Afya kupatiwa fedha nyingi katika miaka mitano iliyopita ambapo Nchi yetu imeendelea kuwa miongoni mwa nchi chache afrika zinazotoa matibabu kwa gharama nafu”amesema Mchengerwa.
Mwisho, Mohamed Mchengerwa Waziri wa Afya ameliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha jumla ya shilingi Trilioni 1.8 katika mwaka wa fedha 2026/27,amesema kupatika kwa bajeti hiyo kutasaidia kutekeleza shughuli mbalimbali zilizopangwa ikiwemo vipaumbele vyote 11 ambavyo vimelenga kuiweka Tanzania kuwa mfano kwa utoaji bora wa huduma za afya kwa Wananchi Barani Afrika.