Nadhani kuna mambo mengine ya hovyo yanafanywa na Serikali, wengi tukiamini yamekubaliwa au ni maelekezo ya Rais, kumbe ni maamuzi wa baadhi ya watendaji wenye akili ndogo ndani ya Serikali.
Kuwazika marehemu usiku, kwa kificho, bila kuwashirikisha ndugu, ulikuwa ni uhayawani.
Siamini kama kuna sababu yoyote ya maana inayoweza kueleweka. Mtu amekwishafariki. Mmetoa maelekezo kuwa msiba usihudhuriwe na watu zaidi ya 10, sasa kumzika usiku kuna maana gani? Hao virus nao huwa wanahitaji muda wa kulala, kiasi cha kusema watu wazike wakati virus wamelala usingizi?
Wati wengi tulilalamikia jambo hilo. Lakini majitu majinga kama yule Bia Yetu, yaliendelea kushabikia. Niliwahi kusema pia, mashabiki wajinga kama Bia Yetu, hawana msaada kwa Rais, nchi, Serikali wala CCM.
Tunampongeza Rais kwa kusitisha ule uhayawani wa kuzika watu usiku. Waliopoteza ndugu zao wana majonzi ua kuwapoteza ndugu zao, lakini pia kutokuwa na uhakika kama makaburi waliyoambiwa ndimo ndugu zao wamelala, ndimo kweli walimolala.
Tupunguze tutofautiane kwa fikra katika kuutokomeza ugonjwa huu lakini tusimame pamoja katika lengo kuu la kulitakia mema Taifa letu.
Sent using
Jamii Forums mobile app