Wizara ya Afya: Zimetimia Siku 41 hakuna mgonjwa mpya wa Marburg

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760


Wizara ya Afya imetoa taarifa kuhusu Ugonjwa wa Marburg kuwa hadi kufikia Machi 10, 2025, zimetimia siku 41 bila kuwa na mgonjwa mpya.

Ikumbukwe Januari 20, 2025, Serikali ilitoa tamko kuhusu kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa Virusi vya Marburg Mkoani Kagera ambapo Wizara imeeleza mwenendo wa udhibiti wa ugonjwa huu unaendelea vizuri.

Januari 2025, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuhusu mlipuko wa #Marburg Wilayani Biharamulo na kudai kuna vifo vya Watu 8, siku chache baadaye Serikali ikatangaza mtu mmoja kukutwa na maambukizi hayo, ambapo Januari 24, 2025, Serikali ikasema mtu mmoja amefariki kati ya wawili waliokuwa na maambukizi.

Pia soma:
~
Mlipuko wa Marburg Tanzania: Serikali yatoa Mwongozo wa Wasafiri wanaoenda na kutoka Mkoani Kagera

~ Mtu mmoja kati ya Wawili waliobainika kuwa na ugonjwa wa Marburg afariki Kagera

~ Rais Samia athibitisha mmoja kugundulika na maambukizi ya virusi vya Marburg nchini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…