Wanajamii forum nawasalim,
Naiomba wizara ya Ardhi na Maendeleo Ya Makazi waumulike Manispaa ya Mtwara. Mimi ni mhanga katika ufisadi ambao unaendelea pale ofisi ya ardhi jirani ma BOT. Nilikuwa nahitaji kulipia kiwanja changu. Lakini kila nikipewa control number inasoma jina ambalo silo la kwangu. Nimefuatilia zaidi ya mara nne naambiwa mpaka wizarani wawezeshe ndipo mtaa wetu eneo la ligula ndipo litaweza kuhudumiwa vyema.
Juzi nilipofika ofisini nikaambiwa ya kwamba kuna mfanyakazi wa ambaye ndiye alikuwa mtaalam lakini ametumbuliwa. Kwamaana bila yeye maeneo mengi waliobaki hawawezi kuyatambua.
So kinachotokea ni kwamba pale nje ya ofisi yao kama unaenda shule ya rahaleo huyo jamaa hukaa. Ukiwa pale ndani wanakuambia umuone huyo jamaa umpeleke site, kisha akirudi anatoa data za site yako ndipo unapewa control number. Unalazimika kumlipa 10,000/= posho na usafiri juu yako. Juzi nilisita nikataka nisome mchezo. Jamaa yuko very busy. Anachukuliwa anarudi anaenda anarudi kiasi imekuwa biashara yake. Mfano mtu site unadaiwa 16,000/= unalazimika kumlipa jamaa 10,000/= plus 1000*2 bodaboda kwenda site na hawabadilishi chochote kwenye data ya kiwanja. Mwaka ujao process itakuwa the same.
Wakuu nimejaribu kuwauliza takukuru mtwara it seems ni mchezo ambao wanaujua kwani wanasema baada ya jamaa kutumbuliwa, hajaajiriwa mtu mwingine kwenye nafasi husika. Issue ni kwamba kwanini mwananchi aingie gharama hii?
Waziri Lukuvi na makamishna wako Mtwara, tutatulie hii kitu kwani wapo wanaotaka kuchukua nafasi ya kuvunjwa kwa bunge na focus ya uchaguzi kuwaumiza wanyonge.
N i hayo tu....