Wizara ya Ardhi yatwaa ubingwa wa Darts Shimiwi 2026

Wizara ya Ardhi yatwaa ubingwa wa Darts Shimiwi 2026

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
47c7c135-f010-44d3-bc7c-200f6ecf3b53_D701A389-9CC2-41B6-9C16-96797D19CDC7.jpeg


KILIMANJARO

Timu ya mchezo wa Darts ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya SHIMIWI 2026 yanayoendelea mkoani Kilimanjaro, baada ya kuifunga timu ya Wizara ya Maji kwa jumla ya pointi 5–3 katika mchezo wa fainali.

Mchezo huo wa fainali uliojaa ushindani na mvutano mkubwa umechezwa Septemba 2, 2026 katika Uwanja wa Magereza, ambapo wachezaji wa Wizara ya Ardhi walionesha umahiri, umakini na ustadi mkubwa katika kurusha mishale, hali iliyowawezesha kupata ushindi na kutwaa nafasi ya kwanza.

Ushindi huo ni matokeo ya maandalizi na juhudi za timu hiyo, huku ukiwa chachu na hamasa kwa timu nyingine za Wizara ya Ardhi zinazoshiriki mashindano hayo kuongeza ari na kufanya vizuri katika michezo iliyosalia.

Katika hatua za awali za mashindano hayo, timu ya Darts ya Wizara ya Ardhi ilipangwa Kundi A na kufanikiwa kushinda michezo yake yote ya hatua ya makundi, kabla ya kuendeleza ushindi huo katika hatua za mtoano.

Katika robo fainali, timu hiyo iliifunga TAMISEMI kwa pointi 3–0, ikafuatiwa na ushindi wa pointi 4–0 dhidi ya RAS Ruvuma katika hatua ya nusu fainali na hatimaye kuichapa Wizara ya Maji kwa pointi 5–3 katika mchezo wa fainali.

Akizungumzia mafanikio hayo, Mwenyekiti wa Ardhi Sports, Bw. Swagile Msananga, amesema ushindi huo umetokana na mafunzo, maandalizi na mikakati iliyowekwa na timu, akieleza kuwa juhudi za wachezaji zimechangia kufanikisha matokeo hayo.

Aidha, akielezea mafanikio ya Wizara katika michezo mingine, Msananga amesema mwakilishi wa Ardhi Sports katika mchezo wa kurusha tufe, Bw. Kelvin Mamku , ameshika nafasi ya tatu, huku timu ya Wizara ya Ardhi ikishika nafasi ya tatu katika michezo ya riadha na mbio za vijiti.
 
Back
Top Bottom