Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Jana nilipata nafasi ya kukutana na Kiongozi mmoja wa Ubalozi wa New Zealand nchini Tanzania, tulipata wasaha wa kula chakula cha jioni yeye pamoja na familia yake. Tulikuwa kwenye hoteli moja maarufu sana haa Dar es Salaam, na baada ya kupata chakula tulizungumza mambo mengi na kupiga stori mbili tatu, na tukiwa kwenye stori nikapata mshawasha kuwa nimuulize kuhusu suala la scholarships haswa kwa wanafunzi wanaotoka Afrika hususani Tanzania.
Nilimuuliza mengi kuhusu hili ila malengo yangu yalikuwa ni kwenye kufahamu haswa je mchakato wa kupata wanafunzi unakuwa ni mchakato wa namna gani? Lakini pia ushirikiano wao kama ubalozi na nchi husika unakuwaje linapokuja suala la ufadhili wa masomo (scholarship). Yule mzee alibaki kushangaa sana kuwa sifahamu namna mifumo ya Afrika ilivyokaa kihasarahasara tu.
Wanapokuwa na wazo la kutaka kuchukua wanafunzi waende nchi yao huwa wanalazimishwa maombi yapitie Wizara ya Elimu na sio njia nyingine, Wizara ya Elimu ndo inabeba dhamana ya kutafuta watu wenye vigezo ambavyo Ubalozi husika inakuwa inahitaji. Lakini ajabu ni kuwa Tangazo la scholarship la Ubalozi linabadilishwa mwanzo mwisho na kutengenezwa tangazo jingine kabsa ambalo linakuwa na upungufu wa taarifa au taarifa zisizo sahihi.
Halmashauri huwa zina utaratibu wa kuweka matangazo kwenye mbao za matangazo ambazo mara kadhaa zinakuwa nje ya ofisini husika, lakini ukisoma matangazo ya scholarship mara kadhaa taarifa na maelekezo yake sio sahihi kwani zinaweka vigezo vingine visivyotakikana kwa ubalozi. Mfano, huweka kigezo cha muombaji awe mwajiriwa wa serikali ilihali tangazo halisi la ubalozi linadai waombaji wawe watanzania, unakutana na kigezo cha Mwaka wa kumaliza chuo au shule ya Sekondari.
Hizo pesa za kuwasomesha wanafunzi zinzotolewa na serikali husika za huko Ughaibuni sio pesa zenu, kwanini mnaweka ngumu hivyo watu kupata ambao mnataka nyie, sio sahihi. Pia alizunguzia suala la kujuana na kubebana sana. Binafsi nashangaa sana kuona nafasi ya kwenda kusoma nje kwa watanzania wanaoweka vikwazi ni watanzania, sijui tuna roho gani?
Kuna kiongozi mmoja mwaka fulani aliwahi kusema “Mnakwenda kusoma kwenye nchi za Ughaibuni ili iweje, Wakati tuna vyuo vingi bora hapa Tanzania? Kwanini uende Ughaibuni? Je ukipata matatizo? Na ajabu ni kuwa kiongozi huyu amesoma Shahada yake UDSM na viwango vingine vya elimu amesomea Japani pamoja na Uingereza. Ni wivu gani wa kijinga huu kiasi kwamba unaweka ngumu kwa Mtanzania mwenzako kwenda kuosha hata macho?
Sikatai kuwa Tanzania kuna vyuo bora ila hivyo vyuo bora vipo vingapi? UDSM, Muhimbili, Sokoine, UDOM, Mzumbe na SAUT, NELSON MANDELA vilivyobaki sidhani kama vinaingia kwenye orodha ya kushindana na vyuo vikubwa vya nje. Lakini wapo wanaotamani kusoma nje ya nchi na kupata nafasi za kuzuru maeneo kadha duniani.
Kwa hakika nimeumia sana kuona watu walio na roho za ajabu sana kwenye maendeleo ya watanzania wenzao. Baadhi ya balozi wameanza kukataa kutumia mfumo ambao Wizara wameuweka kwani ni mfumo kandamizi sana na usiotoa nafasi kwa watu. Ni kawaida kukutana na majina ya walimu wa vyuo wakipelekwa kwenye usahili na kupewa endorsement za kila aina. Tanzania yangu tunarudishana nyuma mwenyewe.
Rai yangu:
1. Wapatie nafasi balozi wenyewe wafanye usahili na kuwafadhili watu kulingana na utaratibu wao, nyie kama Wizara ya Elimu mbakie kama washauri tu kwa wale ambao wamepata nafasi ya kwenda kusoma. Msiwe madalali wa kuonesha yupi ni bora na yupi sio bora kwa viongozi husika ndani ya balozi zilizopo ndani ya Tanzania.
2. Walimu na wakufunzi sio lazima wawe miongoni mwa watu watakaopewa ufadhili, kwa sababu moja, kila chuo kina mahusiano mazuri na vyuo vingine vya kimataifa duniani kote wanaweza kubadilishana watalaamu hivyo sio lazma wakabanane kuchukua nafasi za vijana ambao hutamani kwenda kusoma elimu nje ya nchi.
3. Waajiriwa ambao ni wazawa (watanzania) acheni chuki wajameni, kumkazia mtanzania mwenzako asipate nafasi sio faida kwako bali ni uchoyo wa kipuuzi sana. Kuna dada yupo Ubalozi wa Uswisi, aisee mbinguni sidhani kama utaingia. Dada ana roho mbaya utadhani anaishi Uswisi. Sio kitu kizuri kabsa.

SIO KWA UBAYA! SIO KWA UBAYA!