Vituko vya kwenye sherehe, na vihoja vyake huishia hukohuko kwenye sherehe. Kwani maneno mengi yanayosemwa na MC si ya kweli na wala hayalengi kumchafua mtu yoyote lakini yanalenga kuwaburudisha na kuwafanya maharusi na familia yao, waone ile ni siku yao muhimu na kwa siku ile anakuwa wa muhimu na wa heshima kuliko wote. Ndio maana hukalia viti vya kifalme na kimalkia na kuvikwa mataji. Lakini baada ya hapo taabu na dhiki zinaanza. Mwenye matatizo ni wewe unayeleta mambo ya harusini hapa. Ninyi ndio mnakuwa mnaangalia mikanda ya harusi ya watu wengine baada ya harusi unakuta limtu linasema ona hapa nimependeza, nyambafu harusi ilikuwa yako? hata kama ulialikwa kwenye kamati, mkanda wa harusi waachwe maharusi waangalie siku wanatimiza jubilei ya miaka 50 ya ndoa