Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,355
- 2,736
Nisijue walioko wizarani wanafikiria nini ila ukifuatilia mijadala mbalimbali kuhusu matokeo ya kidato cha nne, utaona wazazi na wahitimu wana sintofahamu nyingi na zenye kuumiza akili za watu.
Hoja ya kwanza inayolalamikiwa ni kuwa, mwaka huu alama zimebadilikia ukilinganisha na miaka ya nyuma. Katika tovuti ya Wizara wametangaza nafasi za masomo ya Ualimu. Kwa upande wa kidato cha nne wazazi na wahitimu wamekuwa wakiuliza mara kwa mara kuwa ina maana tukiomba ualimu hata kama una division 1,2, au 3 hutapata nafasi ya kwenda form five?
Kwa nini wizara isiweke wazi? Kama matokeo yalitangazwa february leo hii mwezi wa 5 kwa nini wizara isiweke wazi. Maana yake kuna implication mbili. Moja Shirika la Posta lineemeke kwa watu kutuma maombi japokuwa hawataenda ualimu au Watu walazimike kuomba ualimu na kupelekwa kwa nguvu ili hali nia yao ni kwenda form five ili wapelekwe ualimu wasichaguliwe kwenda kidato cha tano, wazazi wapeleke vijana wao shule binafsi serikali ikwepe majukumu au lengo ni nini?
Watu wamefaulu vizuri ila wamelazimika tu kuomba ualimu lakini si kwa kupenda bali ni kujaribu kukabiliana na usiri wa Serikali yetu hii. Inakuwaje serikali inashindwa kustrategize kuvutia watu waende ualimu hata kama wana alama nzuri ili wapatikane walimu wenye kupenda kazi hiyo na badala yake tuache kuviziana?
Mtu ataingia gharama atume kuomba ualimu then anyimwe nafasi apelekwe form five hata kama hawezi kumudu gharama yake hasa kwa wale ambao wao na wazazi wao wamepanga asome ualimu apate kazi kwanza aisaidie familia yake. Mtu huyu kuna hatari ya kukosa vyote. Kama ingewekwa wazi serikali ingeweza kuona wepi wameomba ualimu pamoja na kuwa wamechaguliwa kwenda kidato cha tano.
Kuviziana huku kunaumiza watu. Wazazi na vijana hawajui lengo la wizara ni nini. Siri imekuwa siri hakuna taarifa.........na hii saa nyingine ni kukaribisha mianya ya rushwa.......maana watu wataanza kuhonga mpeleke mwanagu huku ....mpeleke mwanagu kuleeee....yaani mkanganyiko. Ngoja posta wapige pesa then maombi yawe discarded watu waende high level basi.....ili mradi vyanzo vya mapato vitengenezwe kwa kucheza na akili za Watanzania. Inaudhi sana lakini.
Ukienda jukwaa la Elimu thread zaidi ya kumi zinauliza selection za form five lini??? Siasa na wizi uko kila mahali hata kwenye vitu visivyotarajiwa. Matokeo yake wataenda watu kwenye ualimu watakaokuja kutunga maswali yasiyokuwa na majibu. Ref : James Mbatia.