Wizara ya Elimu inatesa akili za Wazazi na Wahitimu wa form 4 mwaka 2013. Ualimu unalazimishwa

Ta Muganyizi

R I P
Joined
Oct 19, 2010
Posts
5,355
Reaction score
2,736
Nisijue walioko wizarani wanafikiria nini ila ukifuatilia mijadala mbalimbali kuhusu matokeo ya kidato cha nne, utaona wazazi na wahitimu wana sintofahamu nyingi na zenye kuumiza akili za watu.

Hoja ya kwanza inayolalamikiwa ni kuwa, mwaka huu alama zimebadilikia ukilinganisha na miaka ya nyuma. Katika tovuti ya Wizara wametangaza nafasi za masomo ya Ualimu. Kwa upande wa kidato cha nne wazazi na wahitimu wamekuwa wakiuliza mara kwa mara kuwa ina maana tukiomba ualimu hata kama una division 1,2, au 3 hutapata nafasi ya kwenda form five?

Kwa nini wizara isiweke wazi? Kama matokeo yalitangazwa february leo hii mwezi wa 5 kwa nini wizara isiweke wazi. Maana yake kuna implication mbili. Moja Shirika la Posta lineemeke kwa watu kutuma maombi japokuwa hawataenda ualimu au Watu walazimike kuomba ualimu na kupelekwa kwa nguvu ili hali nia yao ni kwenda form five ili wapelekwe ualimu wasichaguliwe kwenda kidato cha tano, wazazi wapeleke vijana wao shule binafsi serikali ikwepe majukumu au lengo ni nini?

Watu wamefaulu vizuri ila wamelazimika tu kuomba ualimu lakini si kwa kupenda bali ni kujaribu kukabiliana na usiri wa Serikali yetu hii. Inakuwaje serikali inashindwa kustrategize kuvutia watu waende ualimu hata kama wana alama nzuri ili wapatikane walimu wenye kupenda kazi hiyo na badala yake tuache kuviziana?

Mtu ataingia gharama atume kuomba ualimu then anyimwe nafasi apelekwe form five hata kama hawezi kumudu gharama yake hasa kwa wale ambao wao na wazazi wao wamepanga asome ualimu apate kazi kwanza aisaidie familia yake. Mtu huyu kuna hatari ya kukosa vyote. Kama ingewekwa wazi serikali ingeweza kuona wepi wameomba ualimu pamoja na kuwa wamechaguliwa kwenda kidato cha tano.

Kuviziana huku kunaumiza watu. Wazazi na vijana hawajui lengo la wizara ni nini. Siri imekuwa siri hakuna taarifa.........na hii saa nyingine ni kukaribisha mianya ya rushwa.......maana watu wataanza kuhonga mpeleke mwanagu huku ....mpeleke mwanagu kuleeee....yaani mkanganyiko. Ngoja posta wapige pesa then maombi yawe discarded watu waende high level basi.....ili mradi vyanzo vya mapato vitengenezwe kwa kucheza na akili za Watanzania. Inaudhi sana lakini.

Ukienda jukwaa la Elimu thread zaidi ya kumi zinauliza selection za form five lini??? Siasa na wizi uko kila mahali hata kwenye vitu visivyotarajiwa. Matokeo yake wataenda watu kwenye ualimu watakaokuja kutunga maswali yasiyokuwa na majibu. Ref : James Mbatia.
 
Watanzania kweli tunafanywa watu watakavyo. Hata kuhoji tunashindwa???!!!
 
Tatizo nyinyi UKAWA hamkosi kuchokonoa,serikali yetu sikivu ina nia njema.Vuteni subira.
 
Tatizo nyinyi UKAWA hamkosi kuchokonoa,serikali yetu sikivu ina nia njema.Vuteni subira.

Hahahaa..... uko serious mkuu??!!! Ina maana wahitimu wooooote ni watoto wa the so called UKAWA?
 
Nimerudia kusoma sijaelewa unachokimaanisha
 
Nimerudia kusoma sijaelewa unachokimaanisha

Watu wamefaulu vizuri ila wamelazimika tu kuomba ualimu lakini si kwa kupenda bali ni kujaribu kukabiliana na usiri wa Serikali yetu hii. Inakuwaje serikali inashindwa kustrategize kuvutia watu waende ualimu hata kama wana alama nzuri ili wapatikane walimu wenye kupenda kazi hiyo na badala yake tuache kuviziana?

Labda hii paragraph itakusaidia. Ila ndo sasa natambua kuwa najibizana na Jini "Shamsa" wewe binafsi ulishakufa kitambo. Maana tabia zako ni za jini shamsa....hata kitu muhimu na shida kwa watanzania unaona tabu.
 
Kama hauko Tanzania habari ndo hiyo.....ila wametangaza nafasi za kwenda ualimu.
Mbona watapoteza pesa bure, mtu ana division 1, 2 au 3 akienda grade A? Halafu kwa mawazo yao wanategemea ndo iwe basi? kwamba mtu huyo aridhike na hiyo grade A au ualimu kwa ujumla? Basi kama hao maprofessa walioko wizarani ndo wanawaza hivyo basi wote makanjanja tu. Kwanza primary education ni elimu inayoweza kufundishwa na valantias tu, na wazazi nyumbani.
 
Heri mimi juha-mtendaji kamanda kuliko hayo majuha mengine yaliyoko ndani ya chama cha jembe na nyundo.Au wewe unasemaje Mfalme?
 
Hii nchi yetu inakatisha tamaa mkuu TA Muganyizi.Pamoja na madudu yote bado Watanzania wanaambiwa sisiemu ni chama makini,bado ati watu wanaenda kwa wingi kumsikiliza Kinana.Hizi TA Muganyizi sio nyakati za kulalamika,ni kuking'oa chama cha ccm madarakani mara moja.Hata jeshi likiona vema kama walivyopendekeza wakubwa ni kheri kabisa.Nafikiri umenielewa mkuu.
Hahahaa..... uko serious mkuu??!!! Ina maana wahitimu wooooote ni watoto wa the so called UKAWA?
 

Sana mkuuuuuuuuuu
 
hii nchi kila kitu ni siri ma ccm kila kitu wanafanya n biashara
 

Acha kukurupuka ndg yng,
ulitaka wachaguliwe wapelekwe wapi km form six walikuwa hawajamaliza mitihani yao??

Wewe umesoma kweli?
au ulipata div.3 ya mwisho ukaenda private so hujui form five wanachaguliwa lini?

Majina ya form 5 hutangazwa baada ya form 6 kumaliza ndivyo inavyokua miaka yote,hivyo tarajia kuyasikia yakitangazwa muda wowote kuanzia leo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…