KERO Wizara ya Elimu, ingilieni kati kuhusu Utendaji wa NACTVET

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na changamoto katika usimamizi na uchakataji wa taarifa za wanafunzi, kuanzia hatua ya usajili hadi utoaji wa namba za AVN. Ucheleweshaji huu umekuwa ukivunja matumaini ya wanafunzi wanaohitaji kuendelea na masomo ya elimu ya juu.

Hadi sasa, vyuo mbalimbali, ikiwemo DIT, Tengeru, IAA na vingine, vinakabiliwa na changamoto ya taarifa za wanafunzi wao wa Diploma ambao wanahitaji kuendelea na masomo ya Shahada (Bachelor Degree).

Muda wa udahili umebaki mchache, lakini hadi sasa hakuna suluhisho la wazi la changamoto hii. Hali hii inaweza kuwanyima baadhi ya wanafunzi fursa ya kuendelea na masomo kwa wakati kutokana na ucheleweshaji wa taratibu ambazo ziko nje ya uwezo wao.

Tunaomba Wizara ya Elimu iingilie kati kwa haraka ili kuhakikisha changamoto hii inatatuliwa na wanafunzi wanapata huduma zinazohitajika kwa wakati.

Tunaamini hatua za haraka zitasaidia kulinda haki na fursa za wanafunzi kuendelea na elimu ya juu, pamoja na kuimarisha ufanisi na uaminifu katika mifumo ya elimu nchini.

Soma:
 
Wizara ya Elimu Ingilieni Kati Juu ya Utendaji NACTVET

Suala la usimamizi wa taarifa za Wanafunzi Kuanzia Usajili na hadi utoaji wa AVN number umekuwa ni wakuchelewa na kuvunja matumaini kwa wanafunzi wanao hitaji kuendelea na Elimu ya Juu.

Hadi muda huu Vyuo Kama DIT, Tengeru, IAA na vingine vingi vipo kwenye mkwamo wa taarifa za wanafunzi wao Wa Diploma wanao hitaji kuendelea na masomo ya Elimu ya Juu yaan Bachelor Degree.

Muda wa udahili umebaki Mchache sana na hadi muda huu hakuna suluhisho la tatizo hilo.

Wizara ya Elimu ingilieni suala hili kwani likiendelea hivi hivi inaendelea kushusha ari na thamani ya Elimu yetu.

Punguzeni siasa kwenye usimamizi wa Elimu
 
Mpaka muda huu website yao inaishia njiani unapojaribu kufanya application ya Kozi za afya za Diploma.

Ukijaza taarifa hizi: Namba ya mtihani wa kidato cha Nne, Mwaka uliomaliza, Baruapepe, Namba ya simu, na ngazi ya elimu unayoomba (Certificate/Diploma) na kubonyeza CONTINUE hakuna kingine kinachoendelea.
 
Kumekuwa na changamoto katika usimamizi na uchakataji wa taarifa za wanafunzi, kuanzia hatua ya usajili hadi utoaji wa namba za AVN. Ucheleweshaji huu umekuwa ukivunja matumaini ya wanafunzi wanaohitaji kuendelea na masomo ya elimu ya juu.

Hadi sasa, vyuo mbalimbali, ikiwemo DIT, Tengeru, IAA na vingine, vinakabiliwa na changamoto ya taarifa za wanafunzi wao wa Diploma ambao wanahitaji kuendelea na masomo ya Shahada (Bachelor Degree).

Muda wa udahili umebaki mchache, lakini hadi sasa hakuna suluhisho la wazi la changamoto hii. Hali hii inaweza kuwanyima baadhi ya wanafunzi fursa ya kuendelea na masomo kwa wakati kutokana na ucheleweshaji wa taratibu ambazo ziko nje ya uwezo wao.

Tunaomba Wizara ya Elimu iingilie kati kwa haraka ili kuhakikisha changamoto hii inatatuliwa na wanafunzi wanapata huduma zinazohitajika kwa wakati.

Tunaamini hatua za haraka zitasaidia kulinda haki na fursa za wanafunzi kuendelea na elimu ya juu, pamoja na kuimarisha ufanisi na uaminifu katika mifumo ya elimu nchini.

Soma:
NACTVET kwa hatua hii mtoe hata tamko basi
 
Back
Top Bottom