Wizara ya Elimu iweke vitabu vipya vya fasihi andishi katika shule za Sekondari

Wizara ya Elimu iweke vitabu vipya vya fasihi andishi katika shule za Sekondari

Dede 01

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2024
Posts
1,182
Reaction score
2,248
Tangu zamani vitabu vya fasihi andishi vinavyotumika ni vilevile si kwenye somo la kiswahili wala English.

Vitabu kama 'The black hermit' na vyakina Ngoswe na kilio chetu ni vya zamani sana. Serikali ibadilishe vitabu na ilete vitabu vipya.

Haiwezekani mimi nisome vitabu hivyo na wajukuu zangu nao wasome vitabu hivyo hivyo, competence inakuwa zero.

Au ninyi mnasemaje wakuu?
 
Kilio chetu, ngoswe penzi kitovu cha uzembe mafunzo yake bado yanafaa labda kama waongeze vingine
Ndio yanamafunzo mazuri lakini waongeze vitabu vingine vitavyogusia masuala yanayoendelea sasa hivi kama vile mapenzi ya jinsia moja.
 
Ndio yanamafunzo mazuri lakini waongeze vitabu vingine vitavyogusia masuala yanayoendelea sasa hivi kama vile mapenzi ya jinsia moja.
Hivyo vitabu vipya vitatoka wapi wakati watu hawaandiki vitabu wanekalia kushabikia mipira ya Yanga ha Simba tu?
 
Waandishi wenyewe wako wapi siku hizi?
Naona waandishi wa fasihi bongo hawana competence yaani shule za tz tunasoma vitabu wa wakenya vilivyoandikwa na kina Ngugi wa Thiong'o
 
Hivyo vitabu vipya vitatoka wapi wakati watu hawaandiki vitabu wanekalia kushabikia mipira ya Yanga ha Simba tu?
Hivi kuna hata chama cha waandishi wa fasihi hapa bongo?
Hivi kuna mwandishi wa fasihi hapa Jf?
 
Hii inaonesha wahitimu wa Sasa hawana maarifa makubwa kama ya wasomi wa zamani.Maana hawaandiki vitabi vipya ambavyo vingetumika Kwa Sasa.
 
Naunga mkono ✋ 1000%
Tatizo wahusika wenyewe sio wapenzi wa hivyo vitu (kusoma) wakishakaa ofsini wanasubiri watoto wa field tu wawanyooshe.
Bado enough watunzi wazuri kuwahi kutokea tz, Elvis Misiba na Ben R. Mtobwa wametuachia vitabu vingi lakini hakuna hata kimoja kilichotumika wakati wa uhai wao na hakuna dalili ya kuvitumia hata baada ya uhai wao😣😣💔❤️‍🩹
 
ndio mana nakwambia ni vipya kijana
Sawa basi na vitabu vilivyoandikwa na watz vitumike sio kila miaka tunatumia Takadini iliyoandikwa na mzimbabwe hasa kwenye somo la English vitabu vingi hatujaandika sisi.
 
Naunga mkono ✋ 1000%
Tatizo wahusika wenyewe sio wapenzi wa hivyo vitu (kusoma) wakishakaa ofsini wanasubiri watoto wa field tu wawanyooshe.
Bado enough watunzi wazuri kuwahi kutokea tz, Elvis Misiba na Ben R. Mtobwa wametuachia vitabu vingi lakini hakuna hata kimoja kilichotumika wakati wa uhai wao na hakuna dalili ya kuvitumia hata baada ya uhai wao😣😣💔❤️‍🩹
Shida wanafunzi wengi wanaosoma language unakuta physics na mathe zilishambaka ndo wanaamua kusoma language.
Hawasomi kwa mapenzi yao wenyewe.
 
Back
Top Bottom