Wizara ya Elimu iweke vitabu vipya vya fasihi andishi katika shule za Sekondari

" The oldest pumpkin in a home steady should not be uprooted" Song of Lawino by P. Obiteck
"Ocol is no longer in love with the old type"
Tukiachana na hayo fasihi inayotumika mashuleni lazima iendane na content ya dunia ya sasa.
 
Vitabu bado vina manufaa mfano ORODHA na PASSED LIKE A SHADOW vinaongelea maudhui ya virusi vya UKIMWI ambalo bado ni janga kwenye taifa letu
 
Vitabu bado vina manufaa mfano ORODHA na passed like a shadow vinaongelea maudhui ya virusi vya UKIMWI ambalo bado ni janga kwenye taifa letu
Nakubaliana na wewe ila lazima tuongelee majanga mengine yanayotukumba kama vile kutekwa kwa watoto na viongozi wa siasa na pia masuala ya kulawiti.
 
"Ocol is no longer in love with the old type"
Tukiachana na hayo fasihi inayotumika mashuleni lazima iendane na content ya dunia ya sasa.
Ni sawa but our identity as African must be highlighted.
 
Hivi kuna hata chama cha waandishi wa fasihi hapa bongo?
Hivi kuna mwandishi wa fasihi hapa Jf?
Hakuna hata mmoja mkuu. Kulikuwa na chama cha waandishi wa vitabu lakini kimejifia. Hapa tunatokaje sasa? Hatutoboi.
 
Unatakiwa uandike kitabu kingine kipya ili waone tija ya kuvibadilisha.
 
Siyo kweli

Njama cha Elvis Musiba kilishatumika sana kwa kidato cha sita upande wa riwaya pendwa dhati. Na Zawadi ya Ushindi cha Ben Mtobwa pia kilishatumika kwa kidato cha nne.

Shida ya riwaya kama za Elvis Musiba, fani yake haijaiva sawa sawa. Willy Gamba ni kopi dhaifu sana ya Daboloo seven James Bond... na hata atingwe namna gani atachomoka tu hata mahali pasipowezekana. Hata kimaudhui nyingi zilijikita katika kuunga mkono juhudi za kupinga makaburu na kuunga juhudi za kupigania uhuru kusini mwa jangwa la sahara, mambo ambayo kwa Gen Z sidhani kama wanamaindi sana!
 
Gen Z wa tz hawajui kuhusu fasihi na wengi wao wanasoma fasihi kwa kulazimishwa ndo maana vijana wanashindwa kutunga kazi bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…