Kuna tatizo kubwa kwenye ubora wa elimu yetu, mimi siyo muandishi mzuri ila nimeona mfumo wetu wa elimu unajenga watu kukariri ili ufaulu mtihani na siyo kujifunza au kuelimisha
Hii imepelekea mashule yamejikita kufanya njia yoyote hata ya haramu ili mradi wanafunzi wao wapate ufaulu wa juu na hili linachochewa na elimu kuwekwa sana kama biashara na si kwenye ubora
Leo nimeshangaa rafiki yangu mmoja nimemkuta analala kazini kumuuliza eti mtoto wake yupo shule fulani hapa Dar ambayo wameambiwa wanaanza masomo saa kumi na mbili kamili asubuhi na kutoka saa tatu usiku
Sasa nikajiuliza huyu mwanafunzi anaenda kupata elimu au kukaririshwa? Atapumzika saa ngapi? Ina maana kwa hali ya kawaida mzazi wa huyu mwanafunzi na yeye anakuwa kama anasoma
Wizara ya elimu embu jitahidini ili kufanya elimu iwe bora siyo kukariroshana