Ni jambo la kusikitisha na la kushangaza kuona jinsi ambavyo Wizara ya Elimu na baadhi ya taasisi zake zimeanza kuingilia kwa nguvu na pupa maandalizi ya mitaala ya vyuo vikuu, ikiwemo hatua ya kufungia baadhi ya fani au programu kwa kutoa maagizo ya ghafla yasiyozingatia muda wa kitaaluma unaohitajika ili kuandaa mabadiliko yenye ubora na tija. Hili ni kosa kubwa na la hatari kwa mustakabali wa elimu yetu kama taifa.
Sera ya elimu huandaliwa kwa muda mrefu kupitia tafiti, mijadala ya kina, na michakato thabiti ya kitaalamu. Lakini kwa kusikitisha, leo hii vyuo vikuu vinaamrishwa kufanya mabadiliko ya mitaala kwa muda mfupi sana, bila tafakuri ya kina wala maandalizi ya kisayansi. Hili ni uzembe wa kimfumo unaowaweka wahadhiri na taasisi katika presha kubwa ya kisiasa au ya watu wachache wanaotaka kuonekana wanafanya kazi, ilhali wanavuruga msingi wa elimu bora.
Vyuo vikuu si majukwaa ya kisiasa, wala taasisi za kuandaa wataalamu wa kuhudumia soko la ndani pekee. Elimu ya vyuo vikuu ni ya kimataifa (universal education valued with critical thinking grounded on moral values), inayomwandaa mwanafunzi kuwa na uwezo wa kushindana duniani kote, siyo kwenye kata, mkoa, au taifa pekee.
Sera na maagizo haya ya haraka yanaifanya elimu ya juu kuwa ya ndani (particular education), jambo linalodumaza taifa kiakili, kielimu, na kiuchumi, na kushindwa kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa, ikiwemo maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Mwelekeo huu wa kupanga kila kitu kutoka juu na kulazimisha vyuo vikuu kufuata kama taasisi zisizo na tafakuri ni kinyume cha misingi ya uhuru wa taaluma (academic freedom) na heshima ya taasisi za elimu ya juu duniani kote. Kazi ya Wizara ni kusimamia na kudhibiti viwango (regulation) kwa haki na weledi, siyo kuamrisha kama watawala wa kidikteta. Vyuo vikuu vina wataalamu waliobobea, wenye uwezo wa kuandaa mitaala bora bila kuhitaji mashinikizo ya kisiasa au maagizo ya dharura yasiyo na tafakari ya kina.
TAHADHARI KUBWA
Msipokuwa waangalifu, mtasababisha taifa kuzalisha maelfu ya wahitimu wasio na uwezo wa kushindana duniani, wenye elimu ya kubahatisha, wasiokidhi viwango vya kimataifa. Hili litakuwa janga kubwa zaidi kuliko changamoto za elimu tulizonazo sasa. Na baada ya muda mfupi, taifa hili litaendelea kulaumiana kwamba elimu imeharibika au haina tija.
ILI KULINDA HADHI YA ELIMU YETU, ZINGATIENI HAYA:
MFANO HAI
Zamani tuliwahi kuwa na combination muhimu kama Kilimo, Uchumi, Ufundi n.k., lakini zilitoweka bila tafakari ya kina. Nani aliyezifuta?
Au nani aliyeamua kuunganisha masomo ya Fizikia na Kemia bila kujali mantiki ya taaluma hizo? Ni maamuzi ya juu yasiyo na ushirikishwaji wa vyuo!
Kumbukeni kuwa kila chuo kikuu kina misheni na maono (vision) zake. Kuwapangia vyuo vikuu kufundishe hiki na hiki, kwa kuchora masomo ya kufundisha bila kujali muktadha na malengo yao ya muda mrefu, ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi yetu.
Mtu mmoja au kikundi kidogo cha watu wachache kukaa na kuamua kwa niaba ya vyuo vikuu ni kuvunja misingi ya utawala bora wa elimu.
WITO WA HESHIMA
Watendaji wa Wizara na taasisi husika, heshimuni taaluma za watu na kazi ya kitaalamu ya vyuo vikuu. Acheni elimu ifuate misingi ya tafakuri ya kina, siyo matakwa ya haraka ya kisiasa au kibinafsi.
WITO KWA WAZIRI HUSIKA
Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, tunaomba uingilie kati jambo hili kwa haraka na busara. Uongozi wako unahitajika sasa ili kulinda misingi ya taaluma, kuhakikisha vyuo vikuu vinaheshimiwa na kuachwa vifanye kazi yao ya kitaalamu kwa mujibu wa taratibu rasmi.
Hatua za ghafla kama kufungia programu bila tafakari ya kina na bila ushirikishwaji wa wataalamu ni hatari kwa uthabiti wa elimu ya juu na mustakabali wa taifa. Tunaomba uongozi wako uwe chachu ya majadiliano ya kina, ushirikishwaji, uwazi wa maamuzi, na uimarishaji wa mifumo endelevu ya elimu.
Mwisho, ni Seneti ya Chuo Kikuu yenye mamlaka ya kuidhinisha na kupitisha programu au mitaala yoyote kulingana na mahitaji ya kitaaluma na ya soko la ajira. Acheni Seneti zifanye kazi yake kwa mujibu wa taratibu rasmi, siyo kikundi kidogo cha watu kujiamulia kwa niaba ya Seneti. Huku ni kuingilia mfumo rasmi wa vyuo vikuu, jambo linalohatarisha uthabiti wa elimu ya juu nchini.
Elimu ni uti wa mgongo wa taifa. Mheshimiwa Waziri, tafadhali simama kidete kulinda heshima, uhuru, na ubora wa elimu ya juu nchini.

- Acheni vyuo vikuu vifanye kazi yao ya kitaaluma kwa uhuru.
- Acheni kuwabana vyuo, wahadhiri na wataalamu kwa maagizo ya haraka haraka yasiyo na tafakari ya kitaalamu.
- Elimu siyo siasa; haipaswi kuendeshwa kama kampeni ya kuonyesha mafanikio ya muda mfupi.
- Toeni muda wa kutosha kwa maandalizi ya mitaala ili taifa lipate elimu bora inayotambulika kimataifa, siyo elimu ya dharura ya kukidhi matakwa ya muda mfupi.