Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Nimesoma Rasimu ya Mitaala inayopendekezwa, kufuatia kile kinachoitwa mabadiliko ya mitaala ya Elimu nchini
Nilichokiona katika mabadiliko hayo naweza kusema kuwa bado hakikidhi mahitaji ya Watanzania katika kupata Elimu bora ya kuwakomboa.
Katika Rasimu hiyo inayoelezea mitaala ya Elimu kuanzia Elimu ya awali hadi sekondari nimeona mapungufu tafuatayo.
1. Rasimu inawajaza watoto wetu kujua Lugha nyingi sana za Kigeni bila sababu za msingi.
Katika rasimu hii , watoto watatakiwa tangu shule za msingi kujifunza kiingereza, Kifaransa, Kiarabu na Kichina. Hizi lugha zote za kazi gani ili iweje?.
Kwa maoni yangu watoto wanatakiwa wajifunze lugha moja tu ya Kigeni, nayo ni kiingereza. Wajifunze vuzuri lugha moja, waimudu vyema.
Hii hoja eti Wachina wanakuja juu kiuchumi kwa hiyo lazima watu wetu wajue kichina ni Nonsense. Kwa maendeleo ya sasa ya tekinolojia na AI, Ukijua lugha moja ya Kigeni vizuri unaweza kuwasiliana na yeyote duniani kwa msaada wa Wa Tehama hasa Artificial Intelligence. Siku hizi kuna vifaa mtu anaongea lugha moja kifaa kinatafsiri lugha nyingine
Pili muda ambao Watoto wetu watapoteza kujifunza lugha za kichina, Kifaransa na Kiarabu wautumie kujifunza mambo mengine ya maana zaidi kama vile stadi za kazi na Kilimo
2. Rasimu haizungumzii chochote juu ya Elimu ya Ujasiriamali katika elimu ya msingi.
Nimeisoma rasimu, nimeirudia lakini hakuna mahali wala msisitizo wa kufundisha watoto wetu elimu fedha au biashara katika ngazi hii ya Elimu. Sasa kama huwezi kufundisha skills za Enterpreneurship watoto tangu wakiwa wadogo unadhani huko mbeleni utaweza kumudu kutengeneza wajasiriamali wa maana hata kama utafubdisha elimu hii baadae?
3. Rasimu haizungumzii popote namna ya kujenga Critical thinking kwa watoto wetu. Haielezi utaratibu wa midahalo tangu wakiwa wadogo. Nashangaa Rasimu imezipa lugha za kigeni nafasi kubwa lakini haitoi nafasi ya kuwajengea uwezo watoto kudanya fikra tunduizi.
4. Rasimu imekwepa kabisa kufundisha watoto wa shule za msingi Haki zao, na Wajibu wao kwa Jamii na Taifa. Sijaona popote haki za binadamu zikitajwa, Haki ya kupata viongozi wanaotokana na wao ikitajwa. Haki nyingine za kiraia na wajibu wa raia kwa Taifa havijatajwa. Kiufupi Rasimu haimjengi mtoto kujitambua kama raia.
5. Rasimu imekwepa Kufundisha watoto kuhusu Stadi za msingi za maisha za kuwaondia watu katika umasikini kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi na ufundi. Nashangaa Rasimu inazungumzia habari za kufundisha watoto kuchonga vinyago ba kucheza ngoma lakini haifundishi hata kidogo SAYANSI KIMU, KILIMO, UFUNDI n.k
6. Hii Rasimu imeshindwa kufundisha watoto vivutio vya Utalii, watoto wajue wana vivutio gani, viko wapi n.k
7. Hii Rasimu haiinstill values kwa watoto.
Values kama vile Uchapakazi, Ukweli, Kuchukia rushwa, kukataa uzembe, Kulinda mali ya jamii na umma, kuchukia uonevu, rushwa n.k
Kiufupi, Hii Rasimu haikidhi mahitaji, na matakwa ya Watanzania wa sasa hata wa kesho. Wizara ya Elimu, na Taasisi ya Elimu jipangeni upya mje na vitu vya msingi. Hayo mambo ya kutuletea Lugha za Kigeni tupu wakati utajiri wa Utamaduni uliomo katika Makabila yetu mkiacha kabisa kuugusia hauwezi kutusaidia.
Rasimu yenyewe hii hapa chini: