Wizara ya Elimu, Taasisi ya Elimu. Mapendekezo yenu ya Rasimu ya mabadiliko ya Mitaala bado yana mapungufu mengi

Hapana, shule gani hizo za "kimataifa"?

Na hizo za "kimataifa" wameona tu lugha, je humo hawakuona vitu vingine kama stadi za maisha, ujasiriamali, moral and ethical values, kilimo, Sanaa, innovation ?
 
Soma kwa kutulia mkuu, yote unayoyasema hapo siyo ya kweli! Lugha za kigeni ni muhimu kwaajili ya biashara na mataifa mengine na watachagua lugha ya kusoma

Kuhusu kujua maeneo ya utalii watayapata kwenye somo lipo hapo la shule za msingi, Kuna mambo ya maadili yatafundishwa, chakusema ni kupongeza hatua na kusubiria utekelezaji angalau kwa 80% itapendeza!

Mkakati ni mzuri na unavutia kwa macho, Sasa utekelezaji wake lazima uwe na weledi na umakini wa hali ya juu.

Soma rasimu ukiwa na mtazamo chanya Mkuu, utashukuru.
 
Mambo mengi yametajwa kwenye historia ya Tz na maadili....pale ndo pana kila kitu..hzo mbuga nk
 
Mambo mengi yametajwa kwenye historia ya Tz na maadili....pale ndo pana kila kitu..hzo mbuga nk
Historia na mbuga za wanyama wapi na wapi?

Au wanatuletea habari kama za Waziri wa elimu wa zamani Mungai sliyeunganisha physics na chemistry na biology kuwa somo moja!

Sasa huyu Mkenda naye anataka kuunganisha Historia, Civic education na Jiografia kuwa kitu kimoja?
 
Tafuta usome tena huo mtaala mpya mkuu mambo mengi yapo mule hata Yale unayodai hayamo
 
Mtoto wa std 3 Kenya ana self awereness, confidence,anaweza kukuchambulia kitu,au ata ukapiga nae story kama kijana wa chuo...nashindwaga kuelewa kwanini wako tofauti na wakwetu huku..ata Rwanda elimu yao iko vizuri.
 
Mkuu nadhani umesoma ila hujaelewa.

Kuhusu lugha ni kwamba lugha zinafundishwa ni Kiingereza na kiswahili. Wanaotumia mitaala ya kiswahili watasoma lugha ya kiingereza kama lugha ya kigeni na wanaotumia mitaala ya kiingereza watosoma lugha ya kiswahili kama ligja ya Taifa. Hizo lugha nyingine ni optional na mwanafunzi anaweza kuchagua lugha moja kati ya hizo zingine.

Mengine yooote uliyosema yamezingatiwa. Kumbuka Hiyo ni sera na mitaala, Sylubus ndo itachambua in detail katika kila somo ni nini watosma. Ila yote uliyoyaandika yamezingatiwa

Naona umepanikisha watu tu hapa.
 
Kwanza nikwambie hivi,hii nimrasimu na imetolewa kwa ajili ya kuchambuliwa na kutolewa maoni sasa kila mtu ikiwemo wewe ni kutoa maoni sio kukimbilia kutoa lawama, hata hivyo hujaisoma vizuri, soma vizuri kwa utulivu ndipo utoe hayo maoni yako
 
Bro hiyo ni rasimu sio sera kamili na imetolewa ili watu watoe maoni yao,ndipo itatengenezwa muswada upelekwe bungeni kwa mjalada,hivyo kwa sasa sjo muda wa lawama ni muda wa kutoa maoni
 
Sasa bro unalaumu nini kwa rasimu? rasimu ipo kwa ajili ya kutolewa maoni, isome na utoe maoni yako
 
Hebu toa maoni yako unataka nini kiwekwe kwenye rasimu?
 
Afadhali wewe japo umetoa maoni yako, japo hayo uliyoyasema yamo kwenye rasimu
 
Japo sikuisoma yote hiyo rasmu, lakini hapo kwenye lugha nne za kigeni, naona haijakaa sawa. Kama tu kwa sasa tunatumia lugha mbili, yaani Kiswahili na Kiingereza, na Watanzania wengi hata wanapofika chuoni Kiingereza inakuwa changamoto. Je, itawezekana kweli kuongeza lugha nne kama Kiingereza, Kifaransa, Kichina, na Kiarabu?
 
Nakumbuka mwanzoni mwa mchakato kulikuwa na fursa kutoa maoni kwa Watanzania wote, vipi wakati ule ulitoa maoni yako na hayakuzingatiwa???

Mda mwingine inawezekana tunalaumu lakini katika tunayoyalaumu na sisi tulichangia.
 
Nakumbuka mwanzoni mwa mchakato kulikuwa na fursa kutoa maoni kwa Watanzania wote, vipi wakati ule ulitoa maoni yako na hayakuzingatiwa???

Mda mwingine inawezekana tunalaumu lakini katika tunayoyalaumu na sisi tulichangia.
Hatulaumu, tunaonyesha mapungufu na mapendekezo ili kuboresha.

Na huo ni wajibu wetu kama raia.
Si kila mtu alikuwa na access , taarifa au muda wa habari za mchakato wa awali.
 
Sasa bro unalaumu nini kwa rasimu?rasimu ipo kwa ajili ya kutolewa maoni,isome na utoe maoni yako
Tatizo ni kuwa, maoni yanayoletwa kwa taifa, yaendane na uhalisia! Sio kwasababu ni rasimu basi iende kinyume kabisa kisa kuna nafasi ya kurekebisha! Huwezi tengeneza skeleton ya mjusi kisha utegemee kumpata kuku kwa marekebisho, ni upotevu wa muda na rasilimali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…