Katika shule nyingi, hasa za msingi, kumeanzishwa utaratibu wa kutoza michango ya kila siku kwa ajili ya mitihani. Kila siku michango hiyo hutozwa kuanzia Shilingi 300 hadi 1,000 kwa kila Mwanafunzi.
Mtindo huu kwa sasa umekuwa kama fasheni katika shule nyingi, hasa kwenye madarasa yenye mitihani ya kitaifa. Nimefuatilia kwa karibu baadhi ya shule ambazo huita vikao vya wazazi, ambapo walimu huwaeleza wazazi kuwa utaratibu wa mitihani ya kila siku huwasaidia Wanafunzi kufaulu mitihani kwa kuwa wanazoea mazingira ya mitihani.
Hili nililishuhudia juzikati katika Shule ya Msingi Ndumbwi iliyopo Mbezi Juu, na pia niliwahi kuliona katika Shule ya Msingi Kitonga iliyopo Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam (Ilala), Kata ya Msongola.
Mitihani hiyo imekuwa ikitolewa kila siku ndani ya muda wa ratiba za kawaida za masomo. Najiuliza: inakuwaje katika ratiba ya kawaida pawekwe utaratibu wa kupachika mitihani ya kulipiwa?
Lakini pia, wanafunzi wanaoshindwa kuchangia wamekuwa wakitolewa nje, hali inayowapelekea kukosa kufanya mitihani hiyo. Jambo hili linazalisha utabaka bila sababu za msingi.
Ingawa utaratibu huu unatajwa kuwa na tija kwa kuwasaidia wanafunzi kuzoea mitihani, umekuwa ukipelekea wanafunzi kukosa fursa ya kufundishwa kwa kina baadhi ya mada muhimu, kwani muda mwingi hutumika kuandaa na kusahihisha mitihani hiyo ya kila siku. Zaidi ya hapo, katika baadhi ya shule mitihani hiyo haisahihishwi ipasavyo au inasahihishwa na wanafunzi kutoka madarasa ya juu.
Pia soma:
- Shule ya Sekondari Bugene inakusanya michango ya Bima ya Afya bila kuwapatia Wanafunzi bima mpaka wanamaliza
- Shuleni kwa mwanangu wanatozwa Tsh. 300 ya usafi kwa mwezi, kwa shule nzima ni pesa nyingi
Kwa mfano, katika Shule ya Msingi Kitonga darasa lina wanafunzi zaidi ya 300. Je, walimu wanapata wapi muda wa kusahihisha mitihani ya wanafunzi wote hao kila siku? Kinachofanyika ni kuwa wanafunzi ndio husahihishiana, huku walimu wakikusanya fedha pekee. Kibaya zaidi, wakati mwingine hakuna masahihisho yanayofanywa hata na walimu.
Tunapenda sana watoto wetu wasome, lakini kwa mtindo huu hatuwasaidii. Ndiyo maana kuna watoto wanamaliza darasa lakini mambo mengi hawayajui, ingawa wamefaulu mitihani. Tunawaandaa zaidi kukariri badala ya kuelewa.
Lakini pia jambo hili linafanyika katika kipindi ambacho wanafunzi wamekuwa wakichangia pesa ya chakula (lishe) kwa wastani wa Shilingi 1,000 kila siku. Jambo hili limekuwa ni mtihani kwa wazazi wengi wenye hali duni kiuchumi. Sasa tunapoongeza na pesa ya mitihani kila siku, tunatarajia nini kama siyo kuzidi kuzikandamiza familia hizo kiuchumi?
Nimepata muda wa kutafakari na kujiuliza kama utaratibu huu umehalalishwa na Wizara ya Elimu au TAMISEMI. Kama wizara haijatoa ridhaa hiyo na bado ipo kimya, basi kuna haja ya kutafakari kwa kina kuhusu uwajibikaji katika ufuatiliaji na usimamizi wa sekta ya elimu.
Wito wangu kwa mamlaka tulizozipa dhamana ya kusimamia miongozo na kufuatilia utendaji ni kwamba ni muhimu kutoka maofisini na kwenda mashuleni kufuatilia suala hili na kuchukua hatua stahiki.
Kama kuna haja ya kuwepo kwa mitihani, basi uandaliwe utaratibu rafiki na shirikishi, tofauti na huu unaotumika katika shule nyingi kwa sasa.
Pia soma:
- Waziri Mkuu Majaliwa: Michango ya ovyo ovyo shuleni ambayo haina maelezo ikome
- Kukithiri kwa michango ya ovyo shule ya sekondari Itega jijini Dodoma
- Kuna wimbi la michango Shuleni hasa Shule za Msingi
- Michango imekuwa mingi Shule ya Msingi Njelela iliyopo Ludewa - Njombe, Mzazi ambaye hatatoa anakamatwa