Wizara ya Habari/Idara ya Habari Maelezo: inakuwaje channel/mitandao ya habari ya serikali inafikia miaka mitano haina habari mpya? Mnawapimaje?

Wizara ya Habari/Idara ya Habari Maelezo: inakuwaje channel/mitandao ya habari ya serikali inafikia miaka mitano haina habari mpya? Mnawapimaje?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Maafisa Habari waliajiriwa kwa ajili ya kuunga daraja la mawasiliano kati ya serikali na wananchi. Inafikia miaka mitano mtandao rasmi hauna habari yoyote mpya.

Nadhani Sasa wawekewe malengo ya habari zisizopungua 15 kwa mwezi kwa Kila halmashauri au Ofisi ya RAS.

Kila Mkoa una maafisa hawa, lakini wamelala tu.
Vijana wengi wako mitandaoni, hawanunua magazeti, hawa maafisa Habari walitakiwa kuhakikisha serikali pia iko mitandaoni ikiwapa habari za mikopo ya vijana, wanawake, maendeleo yanayoletwa na Serikali, katika Kata zao fedha imekuja kwa ajili ya nini, na nini kifanyike.

Yaani inatakiwa Rais anafika, anakutana na watu wenye habari zote, sio aanze kuelezea kana kwamba pale alipo hakuna watu wake.
Hili Jeshi la habari limelewa chakari, limelala, halipigani vita ambayo limepewa.
Kama Afisa Habari hajaweka habari miaka miwili, anasubiri nini ofisini? Humo halmashauri pamejaa maafisa kedekede, ustawi wa jamii, uchumi, kilimo, sheria, uhandisi, hao ndio vyanzo vikuu vya habari.
Yaani waandishi wa ITV wanapata habari mbele ya macho yako wanatuma, wewe huna Cha kutumia wananchi?

Ndugu yetu Njaidi, Katibu wa chama Cha wanamawasiliano serikalini, kwenye vikao mnavyofanya, Kila Mkoa uwe unafanya presentation ya kilichofanyika kwa Kila muda mnaokutana, watu wasije kula bata tu.

Na maonyo makali yatolewe kwa walio legelege, na next time waje na jinsi walivyoboresha.

MAELEZO wajigawe katika Kanda kwa urahisi wa ufuatiliaji, na Kila habari ikitumwa, maelezo waipate siku hiyo hiyo


Msigwa, fanya mapitio ya jinsi ya kuwawajibisha hawa watu.
Screenshot_20221231-104406.jpg
Screenshot_20221231-104318.jpg
 
Hiyo ndio maana halisi ya kuwa muajiriwa wa serikali Tanzania, kigezo cha kwanza ni uvivu na uzembe kupitiliza.
 
Back
Top Bottom