Wizara ya katiba na sheria imejizindulia utaratibu wa kula pesa za walipa kodi kwa kampeni ya elimu ya katiba mpya 2024/2026; waanza kuandaa mikutano

kiufupi wameamua kutumia gharama kuchelewesha upatikanaji wa katiba, pesa ilishatumika sana sana enzi za JK, sasa wanarudia nini, kumbukumbuku zipo, sema hii nchi kila mtu akipata nafasi lazima apige na asepe, ndio kinachofanyika,

changa la macho hakuna katiba, wala nini? Wananchi mtasubiri sana
 
Chawa mzee
 
Aah Paskali, tuijue katiba, katiba ipi wakati ile ya midabwada CCM hawaitumii na hawataki nchi iendeshwe kikatiba! Tanzania mpaka sasa hatujui kama ni nchi inayofuata mfumo wa vyama vingi au kimoja kwani katiba ya sasa ni atakavyoamka mwenyekiti wa CCM ambaye ni Head Prefect wa wenyeviti wa vyama vingine.
"VIONGOZI MKIJIINGIZA KWENYE KUFANYA BIASHARA, MTAWASAHAU WANANCHI", J. K. Nyerere.
Eee Mungu tusaidie.
 
Katiba si kila kitu, katiba haimlazimishi mtu kuijua na kuifuata, "atakuja rais ambaye atatawala bila kufuata katiba" J. M. Kikwete, hili lilitokea baada ya JK.
Tulishuhudia viongozi wakijipa kinga ya kutoshitakiwa kinyume na katiba, kwa kifupi katiba ipo kwenye kitabu na haifuatwi nchi inakwenda kwa utashi wa CCM( Tanzania ina wenyewe na wenyewe ni CCM).
 
Haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma na ujinga, kikosi kazi kilifanya kazi gani?
 
Tanzania tulilaaniwa kabla ya kuumbwa
 
Paskal hili hapana ni matumizi mabaya ya muda miaka mitatu ni mingi sana, kuna social media zinafikia watu wengi sana na kama sensa imesema nusu ya watanzania ni vijana na watoto sasa miaka mitatu ya nini nyie watu, mmeshakaa miaka zaidi ya 60 mmeshindwa kufundisha katiba hiyo miaka 3 ndio mtaongeza nini.
Tunataka kujifunza katiba mpya ya zamani hata tukijua haina tija. yapo yale ya msingi na yakawaida kila mtu anajua. kama kuiba, kuua, kubaka mbona yanaeleweka.
Nyie wazee kama hamtaki kusikia itabidi mpinduliwe tu
 
Kwanza ni mawazo ya kipumbavu sn kutoea elimu kwa miaka 3, kwanini isiwe kwa miezi 2? kikosi kazi kilifanya kazi gani miezi 6 yote?
 
Tunaendeshwa kwa matakwa ya Rais na siyo kwa katiba ya sheria
 
Watanzania hadi leo sijui nini mnataka maana ni kitambo kirefu mmekuwa mkipiga kelele kuhusu Kariba mpya na mama akaridhia Kwa kutoa go ahead!. Leo vikao na mipango kuhusu upatikanaji wa Katiba mpya vimeanza mmerudi tena kupiga kelele kwamba ni ufujaji wa pesa. Tuwaeleweje sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…