majata
JF-Expert Member
- Oct 7, 2010
- 431
- 180
Mfumo wa ukodishaji wa wafanyakazi umeshika kasi sana hususani kwa makampuni Mengi makubwa hapa nchini, hili lipo sana sana kwa yale makampuni yaliyo na chimbuko la nje ya nchi.
Mfumo huu unaviashiria vya ukwepaji wa mambo fulani ikiwemo kodi kwa Serikali, utakatishaji wa fedha na kunyonga maslahi ya wafanyakazi hasa wafanyakazi Raia wa ndani sababu makampuni yenye kupendelea sana mfumo huu ni yale yasio na uasili wa hapa nchini na ukifatilia kwa undani utabaini makampuni haya yana uhusiano fulani nnje ya Tanzania, na hata mipango ya utekelezaji wa ukodishaji huo huipanga huko nnje kabla kwa kusudi zima la kukwepa vitu fulani na kujiongezea faida.
Viongozi wa wizara ya kazi na ajira waandae utaratibu utakao linda heshima na ujira wa watanzania kwa kuweka utaratibu mzuri katika hili swala, maana wapo wafanyakazi huko sector binafsi ambao ili wao walipwe zipo kampuni mpaka 5 juu yake yeye akiwa mtekelezaji (hayo makampuni ma4 ni madalali wa mshahara wake)
Huu ni unyonyaji mbaya kama ukiendelea nakama hamtauwekea utaratibu mzuri utakao heshimiwa, uwepo wa makampuni mengi juu ya huyu muajiriwa hupelekea akose vitu mhimu kama Bima za Afya, na mshahara mzuri unaoweza kukidhi mahitaji na mhusika kupiga hatua katika maisha na kuukosesha umma wa Watanzania mzunguko mzuri wa pesa unaoweza kuchangiwa na pato zuri la huyu muajiriwa.