Wizara ya Kazi na Ajira angalieni mfumo wa makampuni kukodisha wafanyakazi

majata

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2010
Posts
431
Reaction score
180
Mfumo wa ukodishaji wa wafanyakazi umeshika kasi sana hususani kwa makampuni Mengi makubwa hapa nchini, hili lipo sana sana kwa yale makampuni yaliyo na chimbuko la nje ya nchi.

Mfumo huu unaviashiria vya ukwepaji wa mambo fulani ikiwemo kodi kwa Serikali, utakatishaji wa fedha na kunyonga maslahi ya wafanyakazi hasa wafanyakazi Raia wa ndani sababu makampuni yenye kupendelea sana mfumo huu ni yale yasio na uasili wa hapa nchini na ukifatilia kwa undani utabaini makampuni haya yana uhusiano fulani nnje ya Tanzania, na hata mipango ya utekelezaji wa ukodishaji huo huipanga huko nnje kabla kwa kusudi zima la kukwepa vitu fulani na kujiongezea faida.

Viongozi wa wizara ya kazi na ajira waandae utaratibu utakao linda heshima na ujira wa watanzania kwa kuweka utaratibu mzuri katika hili swala, maana wapo wafanyakazi huko sector binafsi ambao ili wao walipwe zipo kampuni mpaka 5 juu yake yeye akiwa mtekelezaji (hayo makampuni ma4 ni madalali wa mshahara wake)

Huu ni unyonyaji mbaya kama ukiendelea nakama hamtauwekea utaratibu mzuri utakao heshimiwa, uwepo wa makampuni mengi juu ya huyu muajiriwa hupelekea akose vitu mhimu kama Bima za Afya, na mshahara mzuri unaoweza kukidhi mahitaji na mhusika kupiga hatua katika maisha na kuukosesha umma wa Watanzania mzunguko mzuri wa pesa unaoweza kuchangiwa na pato zuri la huyu muajiriwa.
 
Kodi zinakwepwa vip? Hela zinatakatishwa vip?

Hayo makampuni makubwa sehemu nyingine wanaofanya kazi wanatumia taratibu zip?
 
Kodi zinakwepwa vip? Hela zinatakatishwa vip?
Hayo makampuni makubwa sehemu nyingine wanaofanya kazi wanatumia taratibu zip?
Maswali mazito, lakini ukisoma vizuri hapo juu nimesema kunaviashiria, hivi kama makampuni mfano yote mawili kampuni Mama na makampuni mengine yaliyojuu ya mnufaika wa mwisho ambaye ni mtanzania yote yanapata faida(udalali) kutoka katika jasho lako wewe kwanini basi isiwe wewe uajiri we na hiyo kampuni moja kwa moja au angalau uajiriwe na kampuni ya pili tu badala ya mlolongo wa makampuni kuwa juu yako!?.

Ukwepaji kodi na utakatishaji wa pesa upo kwenye mahusiano ya hizo kampuni na zinakotokea ni jukumu la serikali kuhakikisha lengo hili la makampuni makubwa kujiepusha na kuajiri wafanyakazi moja kwa moja halina lengo la kukimbia kulipa malipo halali kwa serikali.
 
Hebu toa mfano specific ili uekeweke kwa urahisi, isije kuwa ni majungu tuu...
 

Wenzetu wamapenda sana kufocus kwenye main areas of their businesses. Mambo mengine wanatoa kwa third parties with expertise in the subject matter
It works everywhere. Mfano, Total inajenga pipeline. Kuajiri contract workers inaweza kuwa sio ideal.
Wanatafuta watu wenye uwezo huo. Wanawalipa. That is normal. Na hao watu wanaajiri kutoka popote wanapotaka. Unazuiaje wasifanye hivyo? Maana akiajiriwa kutoka US na akalipwa kule, hata kama yuko hapa, how do you stop?
Kutakatisha fedha ni suala la kuangalia sana. Yes inawezekana na pia kuna ugumu pia, kama sheria zinafuatwa.

Katika Dunia ambayo pengine tunahitaji transfer of knowledge and technology, itakuwa ngumu sana kuzuia kampuni za aina hiyo kufanya kazi zake
 
Mkuu outsourcing functions ama parts za functions za department ya taasisi ni kitu cha kawaida sana.

TANESCO waliwahi ku outsource management functions kutoka South Afrika ya Net Group Solutions.

Kikubwa hapa ni kuhakikisha organs zetu za ndani ziko na ufahamu wa kutosha kwenye hayo mambo ya yanafuata taratibu zote za kisheria.

Nakumbuka kuna kampuni ya yule binti wa Makamba ilikua inatumika kama recruitment agency halafu inapewa tender ya outsourcing na akatuhumiwa kukwepa kodi ya zaidi ya bilioni 3, baadae hatukusikia chochote kumhusu(mtu kama huyo hata umwambie kwa bunduki kua ccm ni wabaya hawezi kukuelewa).

Ukifuatilia makampuni mengi ambayo yanapewa tender za ku outsource yanamilikiwa na watu wa ccm. Hao ndio wanafaidi hii nchi.
 
Kuna hao kampuni za ulinzi pia..
 

Wanakwepa vipi kodi na kutakatisha fedha mkuu?
 
Makampun mengi ya kenya yanatupiga sana kwenye hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…