Wizara ya Kilimo Ianzishe Dawati la Kusikiliza Kero za Wafanya Biashara

Wizara ya Kilimo Ianzishe Dawati la Kusikiliza Kero za Wafanya Biashara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. EDWIN SWALLE - WIZARA YA KILIMO IANZISHE DAWATI LA KUSIKILIZA KERO ZA WAFANYABIASHARA MAGETINI

Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mkoa wa Njombe, Mhe. Edwin Enosy Swalle ameshauri Wizara ya Kilimo kuanzisha dawati maalum la kusikiliza na kushughulikia kero za wafanyabiashara kutokana na changamoto wanazokutana nazo wanaposafirisha mazao yao hususani magetini.

"Nikuombe Mhe. Waziri (Bashe) kwasababu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum wanalo dawati maalum la kushughulikia maswala ya jinsia, ninakushauri anzisha dawati maalum la wafanyabiashara kwenye wizara hii ili wapate fursa ya kutoa kero zao moja kwa moja kwako Wizarani" - Mhe. Edwin Enosy Swalle, Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mkoa wa Njombe

"Kumekuwa na kero kubwa sana kwa wafanyabiashara, wengi wanasumbuliwa sana na maofisa wa TRA, mageti kama ya Migori, Mikumi kuna usumbufu mkubwa sana kwa wafanyabiashara mpaka wabunge tupige simu ndio watu waachiwe" - Mhe. Edwin Enosy Swalle, Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mkoa wa Njombe

"Niipongeze Serikali, imetambua umuhimu wa kukuza sekta binafsi kwasababu inalipa kodi kubwa sana,tumemsikia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwaambia wanaoanza biashara mpya kupewa muda angalau mwaka mmoja ndipo waanze kulipa kodi,huu ni uamuzi mzuri sana" - Mhe. Edwin Enosy Swalle, Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mkoa wa Njombe
 

Attachments

  • FzPdwI6XwAoA-Zr.jpg
    FzPdwI6XwAoA-Zr.jpg
    47.8 KB · Views: 4
Back
Top Bottom