Wizara ya Kilimo yaomba kuidhinishiwa Bajeti ya TSh Tril. 1.24 kwa Mwaka wa Fedha 2025/26

Wizara ya Kilimo yaomba kuidhinishiwa Bajeti ya TSh Tril. 1.24 kwa Mwaka wa Fedha 2025/26

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akiwasilisha Bajeti ya mwaka 2025/26 amesema;
​
"Ukuaji wa Sekta ya Kilimo umeongezeka kutoka asilimia 2.6 mwaka 2021 hadi asilimia 4.2 mwaka 2023. Aidha, ukuaji wa Sekta ya Kilimo unatarajiwa kufikia asilimia 5 mwaka 2025 na asilimia 10 mwaka 2030"

"Thamani ya mauzo ya kilimo nje ya nchi imeongezeka kutoka Dola za Marekani Bilioni 1.2 mwaka 2019/2020 hadi Dola za Marekani Bilioni 3.54 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 195"

"Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani Milioni 17.14 mwaka 2021/2022 hadi tani Milioni 22.80 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 33 na kufanya utoshelevu wa chakula nchini kufikia asilimia 128 dhidi ya lengo la asilimia 130"

"Uzalishaji wa Mahindi umeongezeka kutoka tani Milioni 6.41 msimu wa 2021/2022 hadi tani Milioni 12.26 msimu wa 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 91.06 na kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa pili Afrika"

"Uzalishaji wa Mchele umeongezeka kutoka tani Milioni 1.76 msimu wa 2020/2021 hadi tani Milioni 3.04 msimu wa 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 72.27"

"Uzalishaji wa mazao asilia ya biashara umeongezeka kutoka tani 898,967 mwaka 2020/2021 hadi tani Milioni 1.45 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 61.5"

"Uzalishaji wa Korosho umeongezeka kutoka tani 210,786 msimu wa 2020/2021 hadi tani 528,263.82 msimu wa 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 150.61"

"Uzalishaji wa Tumbaku umeongezeka kutoka tani 58,508 msimu wa 2020/2021 hadi tani 160,000 msimu wa 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 173.47 na kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa pili Afrika"

"Uzalishaji wa Mkonge umeongezeka kutoka tani 36,170 mwaka 2020/2021 hadi tani 61,215.55 mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 69.24"

"Uzalishaji wa kahawa umeongezeka kutoka tani 59,318 hadi tani 81,366 msimu wa 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 37.17 na kuifanya kuwa ya nne (4) kwa uzalishaji barani Afrika"

"Uzalishaji wa mbegu bora ndani ya nchi umeongezeka kutoka tani 30,167.11 mwaka 2020/2021 hadi tani 63,526.54 mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 110.58. Uzalishaji huo umechangia kuongezeka kwa upatikanaji wa mbegu bora kutoka tani 44,581.08 mwaka 2020/2021 hadi tani 79,700.62 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 78.78"

"Uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta umeongezeka kutoka tani Milioni 1.71 mwaka 2020/2021 hadi tani Milioni 2.14 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 25.1. Aidha, uzalishaji wa alizeti umeongezeka kutoka tani 478,900 mwaka 2020/2021 hadi tani Milioni 1.21 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 154.13"

"Wizara katika kipindi cha miaka mitatu (3) imewezesha ruzuku ya mbolea tani Milioni 1.45 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 708.62 kwa mazao yote. Hatua hiyo, imewezesha kuongezeka kwa matumizi ya mbolea kutoka tani 363,599 mwaka 2021/2022 hadi tani 848,884 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 133.47"

"Uzalishaji wa ndani wa mbolea umeongezeka kutoka tani 32,239 mwaka 2020/2021 hadi tani 158,628 mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 392"

"Tumenunua na kusambaza vitendea kazi ikiwemo magari 44, pikipiki 6,444, vipima afya ya udongo 143, vishikwambi 5,426, visanduku vya ugani 1,662 na kujenga nyumba za Maafisa Ugani 50"

"Wizara imeongeza uwezo wa miundombinu ya Hifadhi ya Chakula ya Taifa kutoka tani 251,000 mwaka 2020/2021 hadi tani 776,000 mwaka 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 209.16"

"Tumenunua matrekta makubwa 500 na matrekta madogo (power tiller) 800 kwa ajili ya kutoa huduma za kilimo"

"Wizara imezalisha ajira za kudumu na za muda mfupi Milioni 1.08 kupitia programu na miradi mbalimbali ya maendeleo ya kilimo ikiwemo miradi ya uzalishaji na utafiti; ujenzi, ukarabati na usanifu wa miradi ya umwagiliaji, programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora na Vyama vya Ushirika"

"Serikali ya Awamu ya Sita imewezesha upatikanaji na usambazaji wa viuatilifu vya korosho vya unga tani 109,083 na vya maji lita Milioni 8.82 na mabomba ya kunyunyuzia viuatilifu 6,337 vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 556.71 kwa mpango wa ruzuku"

"Serikali ya Awamu ya Sita imewezesha upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za zao la tumbaku zikiwemo mbolea, viuatilifu na vifungashio vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 607.29"

"Serikali ya Awamu ya Sita imewezesha upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za zao la pamba zikiwemo mbolea, mbegu na viuatilifu yenye thamani ya Shilingi Bilioni 325.36"

"Serikali ya Awamu ya Sita imeongeza miradi ya umwagiliaji inayotekelezwa kutoka 13 mwaka 2020/2021 hadi 780 mwaka 2024/2025"

"Serikali ya Awamu ya Sita imeanzisha Benki ya Ushirika Tanzania kwa mtaji wa Shilingi Bilioni 58, kufungua matawi manne katika mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro, Tabora na Mtwara na kusajili vyama vikuu vya ushirika 58 kuwa mawakala"

"Upatikanaji wa mbegu bora kutoka tani 44,581.08 mwaka 2020/2021 hadi tani 79,700.62 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 78.78"

"Uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta umeongezeka kutoka tani 1,713,178 mwaka 2020/2021 hadi tani 2,143,098.70 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 25.1."
 

Attachments

Back
Top Bottom