Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo wa mbunge Mkinga, Dastan Kitandula ameuliza bungeni kuhusu jiwe la Tanzania linalopigwa mnada Dubai, Uarabuni. Naibu waziri wa madini amesema nao waliona mtandaoni na wanafatilia.
=====
Dansatan Kitandula: Mheshimiwa spika, jiwe la ruby lenye uzito wa kilo 2.8 lipo kwenye maonesho kwasasa Dubai na jiwe hili linasadikika linatoka Tanzania na kwamba siku chache zijazo kutakuwa na mnada wa kuuza jiwe hili. Je kama nchi tunanufaika vipi na mnada huo?
Naibu waziri wa Madini: Ni kweli mnamo tarehe 13 April mwaka huu wizara ya madini ilipata taarifa kupitia mitandao ya kijamii kwamba kuna jiwe la madini ya ruby lenye uzito wa kilo 2.8 na ambalo linadaiwa kuwa na thamani ya dola milioni 120 sawa na zaidi ya bilioni 240 ambalo limepewa jina la bald al hamal na ambalo linakwenda kuwekwa mnadani ndani ya siku 30 baada ya mfungo na jiwe hilo kudaiwa limetoka Tanzania.
Mara baada ya kupata habari hizi, wizara ya Maliasili imechukua hatua za haraka kutafuta kama habari ni za kweli na kama jiwe hili limetoka Tanzania na kwasababu jiwe hili limeshavuka mipaka lipo kwenye nchi nyingine.
Taarifa hizi sasa ambazo tunazikusanya zinahusisha nchi za Dubai na tayari tunafanya mawasiliano na ubalozi wetu kufuatilia ukweli, pia tumebaini mmiliki wa sasa wa jiwe hilo yuko nchini Marekani na mawasiliano naye tumeshafanya tangu jana.
Tutapopata nyaraka za usafirishaji kama kweli limetoka Tanzania, thamani na asili, nyaraka za mauzo tutaleta taarifa bungeni na kama ni la kwetu niwahakikishie watanzania haki yao haitapotea.
Pia, soma=> Ruby yenye thamani ya bil 276 ilisafirishwa kimagendo huko Dubai? Serikali haina taarifa ilifikaje
=> Mali yetu inauzwa mnada wa Dubai Madini ya Ruby