Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Wizara ya Maliasili na Utalii imeomba Bunge liidhinishe jumla ya Shilingi 359.9 ili iweze kutekeleza
malengo na vipaumbele iliyojiwekea kwa mwaka 2025-2026.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana Wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 amesema Kati ya fedha hizo, Shilingi Bilioni 254.2 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi Bilioni 105.7 ni za Miradi ya Maendeleo.
"Fedha za Matumizi ya Kawaida zinajumuisha Shilingi 130.7 za Mishahara na Shilingi 123.5 za Matumizi Mengineyo"
"Fedha za Miradi ya Maendeleo zinajumuisha Shilingi 32.5 fedha za ndani na Shilingi 73.3 fedha za nje"
Balozi Dkt. Pindi Chana amesema mapato yatokanayo na shughuli za utalii yameongezeka nchini kutoka Dola za Marekani bilioni 1.3 mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.9 mwaka 2024 sawa na ongezeko la 200% kwa Watalii wa kimataifa.
"Filamu ya Amaizing Tanzania baada ya kuzinduliwa mwezi Mei, 2024 Beijing China na kuzinduliwa tena hapa nchini jijini Dar es Salaam Novemba mwaka 2024, Tayari filamu hiyo imesababisha watalii kutoka China kuongezeka kutoka watalii 45,463 kwa mwaka 2023 hadi kufikia watalii 71,140 mwaka 2024 ikiwa ni ongezeko la asilimia 56.5"
"Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UN Tourism), limeitaja Tanzania kuwa nchi iliyoongoza Afrika kwa mwaka 2024 kwa kuwa na ongezeko kubwa la watalii ikilinganishwa na kabla ya janga la UVIKO-19 ambapo utalii Tanzania ulikua kwa asimilia 48, Ethiopia (40%), Morocco (35%), Kenya (11%) na Tunisia (9%). Haya ni matokeo yaliyochagizwa na maono na kujitoa kwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika filamu za Tanzania: The Royal Tour na ile ya Amazing Tanzania"
"Mhe. Spika, ninaomba kutambua mchango wa dhati wa Askari na Maafisa wa Jeshi la Uhifadhi ambao wameendelea kutekeleza majukumu yao kwa ujasiri na weledi katika kulinda na kuhifadhi maliasili za Taifa letu zikiwemo wanyamapori, misitu, nyuki na malikale."
"Idadi ya watalii wa kimataifa imeongezeka kwa asilimia 132.1 kutoka watalii 922,692 Mwaka 2021 hadi watalii 2,141,895 Mwaka 2024. Aidha, idadi ya watalii wa ndani waliotembelea vivutio vya utalii imeongezeka kwa asilimia 307.9 kutoka watalii 788,933 Mwaka 2021 hadi kufikia watalii 3,218,352 mwaka 2024. Hatua hii imewezesha idadi ya watalii kufikia 5,360,247 sawa na asilimia 107.2 ya lengo la watalii 5,000,000 kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2020."
"Mapato yatokanayo na shughuli za utalii yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.3 Mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.9 Mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 200 kwa watalii wa kimataifa. Hatua hii imeifanya Tanzania, kwa mujibu wa UN Tourism, kushika nafasi ya tisa (9) duniani na ya tatu (3) Barani Afrika kwa ongezeko la mapato ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya UVIKO-19."
"Maduhuli ya Serikali yaliongezeka kutoka Shilingi bilioni 397.42 Mwaka 2020/2021 hadi Shilingi bilioni 901.08 Mwaka 2023/2024. Mwaka wa Fedha 2024/2025 kuanzia Julai 2024, hadi kufikia Aprili 2025, Wizara imekusanya jumla ya Shilingi bilioni 912.90 sawa na asilimia 94.2 ya lengo la makusanyo, kiwango ambacho ni kikubwa kuliko wakati wowote kuwahi kupatikana katika historia ya sekta hii."