Wizara ya mambo ya ndani iwaangalie graduates kwa jicho la huruma

Moshie

Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
33
Reaction score
19
Mtaani kuna graduates wengi sana
wenye elimu ya vyuo vikuu.Kinachouma na kuumiza ni pale hizi ajira za wizara ya mambo ya ndani(polisi,magereza ,uhamiaji na zimamoto) kuwabagua vijana wenye elimu za shahada.Vijana wadogo wenye elimu za kidato cha NNE wanaajiriwa wenye shahada wanaachwa hii inapelekea vijana wenye shahada kudhalaurika kupelekea kushuka thamani ya elimu hapa tanzania.

Naiomba wizara ya mambo ya ndani na serikali ya Tanzania iwaajiri hata hawa graduates kwani wapo tayari hata kulipwa mishahara ya constable/private. Kwani kuna nini mukiwaajiri na kuwaacha wawe na vyeo vya chini kabisa( constable)

Maana Leo 21/09/2021 nimeona mh waziri akishukuru kwa kupewa nafasi za magereza , uhamiaji , zimamoto na fire ila nafasi karibu zote ni za kada ya constable !! Jamani kwani hakuna wenye degree wanaopenda kuwa constable was polisi , fire , magereza au uhamiaji ?? Msitenge wenye degree miaka inazidi kwenda wanazeeka na kupoteza sifa za kuajiriw kwenye sekta za ulinzi na usalama ukizingatia ni miaka mingi ajira hazijatoka. Kuna vijana wapo JKT ni mwaka wa 4 sasa wanajitolea.vijana hao wameingia jkt na elimu za shahada waende wapi??

NAPENDA NCHI YANGU , NAWAPENDA VIONGOZI WANGU ,,, MUNGU AWABARIKI NA KUENDELEZA VEMA TAIFA
LETU
 
Daaah kwaio unamaanisha uhamiaji,fire na magereza nao wanaweza kutoa post afu kingine ht kwa elimu ya form4 na form6 wanawabagua wenye ufaulu wa juu
 
Yan hapo LA kwa magereza kwakuwa post zao huwa zipo general ila uhamiaji na fire constable Mara nyingi huwa n form4 aise
 
Mshara wa graduate MMOJA wastani unalipa form four wa wili na CHENJI inabaki.
je, ukiajiri graduate 500_ hapo unanguvu kazi ya Form four wangapi?

Kusoma Sana siyo kuajiriwa. Bali kusoma Sana ni fursa ya Msomi kutengeneza ajira Kwa wachini yake.
 
Mshara wa graduate MMOJA wastani unalipa form four wa wili na CHENJI inabaki.
je, ukiajiri graduate 500_ hapo unanguvu kazi ya Form four wangapi?

Kusoma Sana siyo kuajiriwa. Bali kusoma Sana ni fursa ya Msomi kutengeneza ajira Kwa wachini yake.
Tatizo hujaelewa alichouliza mwenzako elewa kinachozungumziwa ndo ukoment
 
Divide and Rule.....

Yaani wote Watanzania mnaanza kubaguana ni nani apate kipato na nani asipate na sio kufikiria ni vipi kila mtu atapata kipato ?

Kweli Things have Fallen Apart... The Center is no Longer Holding
 
CCM na watawala madiktekta hawataki kuajiri wenye uwezo wa kureason jambo na kufuata sheria, Form four waliofeli kwao hakuna jambo kama hilo, wao wanapelekwa kama nyumbu na hakuna anayewajibika!

Mageuzi ya TanPol liwe jeshi linaloheshimika yatafanywa na kundi kubwa la wasomi na wale wenye elimu ya kati.
Sanuka!
 
Tatizo vijana hawajui kutafuta ajira. Mtu anataka form 4 na wewe una degree, tatizo liko wapi? Si unaonesha cheti cha form four tu. Kwanini kuji aggrandise kuwa una degree ambayo itakutupa nje ya ulingo.
 
Tatizo wakihitaji form for four , watakwambia eliemaliza kuanzia 2016, 2017, 2018, 2019 ,2020 sasa wewe ukitoa cheti chako cha form 4 utakuta umemaliza 2012 au 2013.
Hapa ndo changamoto
 
Mshara wa graduate MMOJA wastani unalipa form four wa wili na CHENJI inabaki.
je, ukiajiri graduate 500_ hapo unanguvu kazi ya Form four wangapi?

Kusoma Sana siyo kuajiriwa. Bali kusoma Sana ni fursa ya Msomi kutengeneza ajira Kwa wachini yake.
Kwani mshahara wa graduate polisi ni kias gan had wanawakwepa degree holders
 
G Graduate yoyote akiingia jeshi lazima aanzie level ya constable, je mshahara wake unakuw ni wa level hiyo au kwa kuw ni graduate analipwa mshahara tofauti?
 
G
Graduate yoyote akiingia jeshi lazima aanzie level ya constable, je mshahara wake unakuw ni wa level hiyo au kwa kuw ni graduate analipwa mshahara tofauti?
Graduate yeyote wa polisi anamshahara wake na pia wamegawanyika kuna tofauti ya mshahara kwa waliosoma kozi za science na walio soma kozi zingine
 
G
Graduate yoyote akiingia jeshi lazima aanzie level ya constable, je mshahara wake unakuw ni wa level hiyo au kwa kuw ni graduate analipwa mshahara tofauti?
Huwa wanawalipa kulingana na elimu uliyonayo wote mnaweza kuwa n constable lkn mshahara wa form4 na graduate mwenye degree uko tofauti hii n kwa majeshi yote yaliyo ndan ya wuzara ya mambo ya ndani
 
Hii n jumla na professional allowance mn graduate lazima alipwe na professional allowance.
Samahan kwa kuuliza tena boss, hiyo 960k umesema ni pamoja na professional allowance, my qn is professional allowance inakuwa sawa kwa wote au ina vary? Na kuna ambao wanapata zaidi ya hiyo?

Pili sina uzoefu sana kwa polisi ila Kwa nnavyoona pia naona kuna utofauti mkubwa kati ya JWTZ na majeshi mengine kwenye upandaji wa vyeo..naona kama JWTZ kupanda vyeo ni haraka zaidi ila polisi hata kama una elimu nzuri unaweza sota miaka au inakuaje hapo?Kama unaufahamu tafadhali nielimishe kwa hili

Tatu, kwa jeshi kama polisi, kuna nafasi ya kuendeleza professional yako ukiingia huko yan wakakuruhusu kwenda kusoma au itategemea na uhitaj wao zaidi?
 
acha kulia lia jeshi lipeleke wapi wasomi.wasomi mkawe mainjinia huko mjenge mabarabar ambuni miradi mjiajiri si mmesoma nyie .acheni majeshi ni ya wasiosoma
 
Nchi yetu sera nyingi sanaa alafu siasa nyingi....hii nchi kuja kuendelea mpaka millennium elfu 10 zipite serious jamani....unakaa mtwara intaview dodoma na Mia nyekundu huna mfukoni..hii serikali inaenda resi sana
 
Hapa dawa n kuomba kwa cheti cha form4 tu au form6 yani degree pressure tupu nafasi za police hz degree wanahitajika watu 50 na wameitwa kweny usail watu 700
 
Hii n jumla na professional allowance mn graduate lazima alipwe na professional allowance.
Kaka nimekwambia kabisa mshahara unatofautiana kaka kama wewe ni doctor yaani MD unalipwa 1.5 milioni ,kwa aliesoma IT au Engineering 990000 na kwa degree za art ni 860000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…