barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,880
Kuna uzi uliletwa humu JF siku kadhaa zilizopita ukieleza kuwa Idara ya Uhamiaji imesimamisha utoaji wa hati ya kusafiria(Passport) kwa sababu ya upungufu/ukosefu wa karatasi za kuandalia passport hiyo.Hii ilikuwa hata ukituma maombi kwenye ofisi za mikoa kuja makao makuu,majibu ilikuwa kwa sasa zoezi la kutoa "passport" limesimamishwa mpaka hapo Idara itakapopata karatasi za kuandalia passport hizo.
Hata wale "vishoka" wenye kujua mbinu za kupenyeza mpaka kitengo cha kuandalia passport Makao Makuu ya Uhamiaji Kurasini wanasema hata kwa dau lolote kwa sasa passport ni ngumu kupatikana.Wenye njia za mkato waliokuwa na uwezo wa kupenyeza "rupia" ili kufanyiwa msaada wa haraka nao wamegonga mwamba kuwa hata kwa "hela ya kiwi" kwa sasa passport ni ngumu sbb "zoezi la utengenezwaji" limesamamishwa kwa sbb ya uhaba wa "malighafi" za kutengenezea.
Tetesi za ndani ya Idara hiyo zinasema ni agizo toka "juu" kuwa zoezi hilo limatakiwa kusimama kwa muda,kwani ktk mikono ya watu wengi kwa sasa,kuna hati za kusafiria kwa watu ambao sio raia halali wa Tz na wamepata hati hizo katika mazingira ya rushwa na tatanishi.Hivyo zoezi la kutoa hati hizo limesitishwa kwa muda ili kutengeneza utaratibu mpya wa kupatikana kwa hati hizo kwa wale waombaji wa mara ya kwanza na wale wanaotaka kuhuhisha.
Maana kwa kipindi kirefu ilikuwa inawezekana kupata hati ya kusafiria ndani ya siku tano ili hali kiuhalisia zoezi huchukua wiki mbili hadi mwezi ili wenye mamlaka kujiridhisha uhalali wa muombaji.Ngawila ilikuwa ni moja ya kigezo cha kupata hati ya kusafiria ya Tz na wala si uraia wa mtu.
Tutege sikio na kusubiri juu ya "Tetesi" hizi.Muhimu ni "JF be the first to know"