Tetesi: Wizara ya Mambo ya ndani kupitia Idara ya Uhamiaji yapiga "stop" utoaji wa Passport

Tetesi: Wizara ya Mambo ya ndani kupitia Idara ya Uhamiaji yapiga "stop" utoaji wa Passport

"Asavali"maana kuna jirani yangu ilikua aende kwa Obama next month na alishaanza nyodo! Sasa acha aisome mamba tu sasa maana hakuna namna.
 
Nasikia hakuna kipindi ambacho vijana walikua wanakimbia na kutokomea zao nje kama kipindi cha miezi 6 iloisha (Mwenyewe nikiwemo) sasa Jikoni wameona vijana wataisha!
 
Nasikia hakuna kipindi ambacho vijana walikua wanakimbia na kutokomea zao nje kama kipindi cha miezi 6 iloisha (Mwenyewe nikiwemo) sasa Jikoni wameona vijana wataisha!
Duuh!!ni kweli?
 
Duh haya sasa majanga yaani sijui kwanini tumefika hapa.
Mkuu ndiyo maana ninarudia kusema kuwa matunda ya serikali ya AWAMU YA TANO tutaanza kuyaona baada ya miaka kati ya 2 mpaka 3 hivi. Sasa hivi ni kusafisha UUZO tu na hii itachukua mda mwingi. hongera Mhs Rais kwa kuanza vizuri. ninaomba wananchi waelezwe kuwa matunda yatakuja baada ya mda kwa sababu sasa hivi ni kusafisha SITE.
 
Hakuna lolote wameishiwa vitabu vya passport ndio vinasubiriwa kutoka nje ya nchi
 
Siyo pass port tu hata Salary slip hazitoki sasa hivi, sijui hii serikali inatupeleka wapi? Toka mwezi June, mapaka leo hii Tunaambiwa Wizara ya Fedha imekosa Materials kuprint. So bad.
 
MSIJALI SOON SERIKALI HII SIKIVU ITAWAPATIA PPORT...

OVA
 
Tatizo la watu wakishakula ugali wa bure ikul na familia zao ziko well off on taxpayers hawajali watanzania wenzao. Shibe mbaya sana.

Paspoti ni haki ya kila MTANZANIA kupata bila bughudha.
Umeona best,hii nchi majanga kwa kweli
 
Siyo pass port tu hata Salary slip hazitoki sasa hivi, sijui hii serikali inatupeleka wapi? Toka mwezi June, mapaka leo hii Tunaambiwa Wizara ya Fedha imekosa Materials kuprint. So bad.
Mkuu hii nchi haijawahi kuishiwa dawa za chanjo ya watoto zaidi ya kipindi hiki! wanafunzi field wa vyuo vikuu wanalia njaa tu wamepewa pesa nusu, nusu haijulikani itakuja lini? si cha walimu wala madaktari waliokwisha ajiriwa tangu bwana huyu aingie madarakani! yaani nchi imerudi nyuma mno
 
Ila uhamiaji pale bhasi tu toka July mpaka Leo sijapata passport, lakini pipoz znakuja nyuma zinapata within a week
 
Kwhaiooowote tubakii dar hakuna safarii

Mpwa hakuna safari mpaka wajulikane wale wote walioidhinisha matoleo ya passport baada ya issue ya Benard kujulikana.

Pia kuna uzi niliweka humu wa kuishauri idara kuhusu fomu za maombi hasa ya visa kwamba inabidi ziboreshwe kidogo maana zipo kienyeji mno. Na pia fomu za maombi ya passport nazo zinaangaliwa upya.

Hivyo kuna tetesi pia kwamba fomu za maombi zitakuwa na maswali ya ziada.

Nafikiri waziri amechukua wazo la busara kabisa, maana ukikutana na baadhi ya watu wameshika passport halafu lugha ya Kiswahili inakuwa shida, basi hiyo ni dalili za kuharibika system ya utoaji passport.
 
Umenena....Lkn Bernard si jamaa yako yule?au mnamkana na mwenzio yule mpare wa HQ kisa kimenuka?
 
Umenena....Lkn Bernard si jamaa yako yule?au mnamkana na mwenzio yule mpare wa HQ kisa kimenuka?

Hapana mkuu, binafsi simfahamu Bernard.

Ila watu walokuwa karibu nae wanafahamu mihangaiko yake.

Hiyo mihangaiko imegonga ukuta.

Lol.
 
Back
Top Bottom