Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ianze kuboresha vigezo vya usajili wa taasisi za dini, hasa makanisa

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ianze kuboresha vigezo vya usajili wa taasisi za dini, hasa makanisa

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Sijui kama wizara Ina maono gani kuhusu usajili wa taasisi za dini, hasa makanisa. Kwa upande wangu naona ni muda muafaka Sasa kupitia upya vigezo vya usajili wa makanisa kabla hatujachelewa.

Naona kabisa matapeli wote wa mjini wamevamia usajili wa makanisa. Nashauri kwamba kwa kuanzia Sasa, mtu anayetaka kusajili kanisa, walau awe na digrii ya theolojia au diploma kutoka chup kinachotambulika, awe na eneo la kanisa ambalo litakaguliwa kama linakidhi vigezo, na awe na Bodi ya wadhamini ambayo itakuwa na watu wenye weledi kutoka vyuo vinavyotambulika.

Katiba inatoa Uhuru wa kuabudu, lakini serikali Ina wajibu wa kuilinda jamii dhidi ya makanjanja wa kiimani/dini. Uhuru wa kuabudu uwepo, lakini ukitaka kuanzisha taasisi ya kuabudia,uwe na vigezo kadhaa wa kadhaa. Minimum requirements.



Kwa hali ilivyo, wamejaa wahuni wengi sana wanajiita wachungaji.

 
Serikali ikiendelea kufumbia macho punde patazuka McKenzie au Kibwetere wa Tanzania
Nchi kuna majuha wa imani wengi sana, angalia ule upuuzi wa Babu wa Loliondo.
 
Back
Top Bottom