Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAOMBA BILIONI 295.9 BAJETI MWAKA MPYA WA FEDHA 2023/2024
Waziri wa Wizara Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Hamis Ulega ameliomba Bunge likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi na mapato katika mwaka 2023/2024 ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya jumla ya Shilingi 295,920,933,000.00.
Akizungumza leo Bungeni wakati akiwasilisha Makadirio hayo ya mapato ambapo Mhe. Ulega amesema kuwa Kati ya fedha hizo, Shilingi 112,046,777,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Mifugo (Fungu 99) na Shilingi 183,874,156,000.00 kwa ajili ya Sekta ya Uvuvi
Aidha Mhe. Ulega amesemam Wizara inaomba kutumia jumla ya Shilingi 112,046,777,000 kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya Sekta ya Mifugo ambapo Kati ya fedha hizo, Shilingi 50,122,670,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 61,924,107,000 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo.
Mhe. Ulega ameongeza kwa kusema kuwa Fedha za Matumizi ya Kawaida Shilingi 50,122,670,000,Mishahara Shilingi 23,939,807,000,Matumizi Mengineyo (OC) Shilingi 26,182,863,000 na Fedha za Matumizi ya Maendeleo Shilingi 61,924,107,000 wakati Fedha za Ndani, Shilingi 56,592,173,000 146 huku Fedha za Nje, Shilingi 5,331,934,00