Wizara ya Mifugo yaanza kampeni ya kunywa maziwa shuleni Wilayani Rungwe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Dkt. Mackrina Nombo, Mtaalamu wa Lishe
​
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi ulio chini ya Wizara hiyo unaofadhiliwa na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) imeanza kampeni ya unywaji wa maziwa shuleni ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha lishe kwa wanafunzi, kuondoa utapiamlo na udumavu sambamba na kupandisha kiwango cha ufaulu shuleni.

Kampeni hiyo imejumuisha mikoa 8 kati ya 26 huku Mbeya/Rungwe ikiwa ni kati ya wanufaika wa programu hiyo ya maziwa shuleni.

Kampeni imeanza Julai 15, 2026 katika Shule ya Msingi Kisa iliyopo Kata ya Kisondela ambapo wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wameanza kwa kutoa elimu na kuzijengea uwezo kamati za shule, walimu, wasindikaji wa maziwa dhidi ya namna bora ya utekelezaji wa zoezi hilo.

Taarifa ya Halmashauri ya Rungwe imeeleza kuwa shule zitakazonufaika ni pamoja na Kisa, Lufingo na Ikuti kwa hatua ya kwanza.

Imeeleza kuwa katika kampeni hiyo serikali itajenga miundombinu ya kuhifadhia maziwa (ATM za Maziwa n.k) katika shule hizi huku mzazi akimuwezesha mwanaye kupata maziwa kwa gharama nafuu.

Imeelezwa kuwa hatua hiyo itaongeza lishe bora baada ya hatua ya wanafunzi wote kupata chakula cha mchana kila siku kufanikiwa katika shule zote za msingi na sekondari.

Kwa wastani Halmashauri ya Rungwe huzalisha lita za maziwa 180,000 kila siku, maziwa ambayo hutumiwa na wakazi kama chakuka lishe na mengine husafirishwa katika masoko mbalimbali nchini.
 
Safi sana!
 
View attachment 3630041

Ni Mradi mzuri sana. Naomba kudodosa kama ifuatavyokwa maboresho:
1. Kampeni itaana au ilianza lini na Hitimisho litakuwa ni lini ili Shule ziendelee zikiwa zinajisimami zenyewe badala ya kuwa ni Kampeni (Issue ni sustainability)
2. Huenda kukawepo na watoto watakaoshindwa hata kuchangia/kununua maziwa kutokana na hali ya Familia au Mazingira yao e.g. watoto wanaojitegemea( ref. TASAF -Vulnarable groups) Watasaidiwaje?
3. Huenda wakawepo watoto wenye mzio(Allergy) kwa maziwa fresh e.g. Lactose intolerance watasaidiwaje?
4. Mwisho; Kama Mpango ukawa na ufanisi mkubwa kiasi kwamba hata wasiokuwa wanafunzi lakini ni watoto wataweza kujiunga/kunufaika ndani ya Kampeni hiyo?
Ila hiyo kampeni ni nzuri kaza buti :ClapHD:
 
Back
Top Bottom