saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Waziri wa Nishati, Januari Makamba ametangaza kuajiri vijana 139 watakaosambazwa katika Halmashauri zote nchini ili wawe waratibu wa Miradi ya REA katika maeneo yao.
Makamba amesema hayo Julai 13, 2022 akizingumza Bariadi Simiyu
“Vijana hawa 139 kazi yao ni kufuatilia miradi imefikia hatua gani, mfano kama vifaa vya umeme vimefika katika maeneo yao, kama nguzo zimechimbiwa mashimo, kama zimesimamishwa na kama nyaya zimevutwa, vijana hawa watakuwa pia kiungo cha mawasiliano kati ya Wizara, Tanesco, viongozi wa Serikali na kisiasa pamoja na wadau wengine wanaohusika na miradi hii” amesema Makamba
Chanzo: Instagram ya Wizara ya Nishati Tanzania