SoC04 Wizara ya ujenzi na Wizara ya Madini zishirikiane kikamilifu ili kurahisisha upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa miundombinu ya barabara

SoC04 Wizara ya ujenzi na Wizara ya Madini zishirikiane kikamilifu ili kurahisisha upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa miundombinu ya barabara

Tanzania Tuitakayo competition threads

HARUNI IDDI

Member
Joined
May 31, 2024
Posts
8
Reaction score
3
Wizara ya ujenzi inatakiwa kufanya kazi bega kwa bega na wizara ya madini ilikurahisha upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa miundombinu ya barabara ili ujenzi uweze kukamilika kwa wakati na wananchi kuanza kupata huduma kupitia miundombinu iliyopo katika maeneo Yao.

Kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yameleta uharibifu mkubwa wa miundombinu katika maeneo mbalimbali hasa kwenye mikoa kama Mbeya, Tabora, manyara Kilimanjaro, ambayo ulipata mvua nyingi zilizo haribu miundombinu ya barabara na usafirishaji kwa ujumla.

Upatikanaji wa malighafi za ujenzi kama vile mchanga, mawe, kokoto, na malighafi nyingine za viwandani kama vile lami, saruji, na vyuma iliviweze kupatikana kwa wepesi ni muhimu kuwepo na ushirikiano wa karibu kati ya wizara ya ujenzi kupitia wakala wa barabara ( Tanroads) na wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA ). na wizara ya madini ili madini ya ujenzi uweze kupatikana kwa wepesi na kurahisisha ukamiliahaji wa miradi miundombinu kwa wakati.

UShirikano huu unaweza kuleta faida mbalimbali kama ifuatavyo;
1. Kupunguza urasimu; wizara hizi zikifanya kazi kwa ukaribu zaidi itapunguza urasimu katika kupata vibali vya kutumia rasilmali za madini katika ujenzi wa miundombinu ya barabara hivyo kusaidia ukamlishaji wa miradi kwa wakati.

2. Miradi ya ujenzi kumalizika kwa wakati; kutokana na upatanaji wa malighafi za ujenzi wa miundombinu ya barabara inaweza kumalizika kwa wakati kulingana na mahitaji ya jamii husika kwani miradi ya ujenzi huchochea uwepo wa ukuaji wa uchumi wa jamii kwa ujumla.

Pia kutokana na uhitaji mkubwa wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara kutokana na uharibifu mkubwa ulioletwa na mabadiliko ya tabia ya nchi ni vyema serekali kubuni vyanzo vipya kupata mapato ilikugharamikia ujenzi wa miundombinu kupitia Mfuko wa barabara (Road funds).

Pia Kuna haja ya serekali kushirikiana na sekta binafsi katika kuchangia gharama za ujenzi, matengenezo, na uboreshaji wa miundombinu ya barabara.

Kwa kuwa suala la ujenzi wa miundombinu ya barabara ni mtambuka ni muhimu kuwepo kwa ushirikiano wa karibu wa wizara na taasisi zake kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na wizara nyingine kama wizara ya madini, fedha, na wadau wengine.
 
Upvote 4
Wizara ya ujenzi inatakiwa kufanya kazi bega kwa bega na wizara ya madini ilikurahisha upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa miundombinu ya barabara ili ujenzi uweze kukamilika kwa wakati na wananchi kuanza kupata huduma kupitia miundombinu iliyopo katika maeneo Yao.
NA ingependeza hata zaidi, wizara zote, na taasisi zote kushirikiana nchi ikatenda na kuenenda kama kiumbe mmoja bro.

Pia Kuna haja ya serekali kushirikiana na sekta binafsi katika kuchangia gharama za ujenzi, matengenezo, na uboreshaji wa miundombinu ya barabara.

Kwa kuwa suala la ujenzi wa miundombinu ya barabara ni mtambuka ni muhimu kuwepo kwa ushirikiano wa karibu wa wizara na taasisi zake kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na wizara nyingine kama wizara ya madini, fedha, na wadau wengine.
Hakika, kama kiumbe mmoja. Single organism.
 
Back
Top Bottom