Wizara yafafanua taarifa ya kuonekana kwa FARU MWEUSI katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu taarifa iliyotolewa na mtandao wa Tanzania Times, tarehe 3 Machi, 2022 ikieleza kuonekana kwa faru mweusi katika Hifadhi ya Taifa Nyerere.

Wizara imeeleza kuwa taarifa hiyo ambayo inaendelea kusambaa katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii siyo sahihi na wanaomba ipuuzwe. Ukweli ni kwamba hakuna Faru mweusi aliyeonekana katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere kama ilivyoripotiwa na mtandao huo.

Aidha, Wizara imesisitiza kuwa Msemaji Mkuu wa masuala ya wanyampori hapa nchini ikiwemo utoaji wa takwimu na taarifa za wanyamapori kwa umma ni Wizara ya Maliasili na Utalii na si vinginevyo.

 
Kwani Faru mweusi ni Ishara gani!? Nuksi balaa au mkosi!? Au heri!?
 
Ana faida gani hasaa..!??
Ni kivutio kikubwa Cha utalii kwa Afrika inasemekana wapo kwetu tu na kenya. Kutokana na umaalum wake Kuna msanii amewahi kujiita "black rhino" kumaanisha hakuna Kama yeye duniani yupo Tanzania pekee. Kwahiyo kutokana na hili Ni kivutio kikubwa Cha watalii na wanalindwa Sana Kama ingekua serikalini tungesema ulinzi wao Ni Kama wa Rais.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ili mumpige bei kimya kimya
 
πŸ‘πŸ»πŸ‘πŸ»πŸ’―πŸ’―
 
Sijaelewa sababu za kukanusha, si yupo kwenye hifadhi? Au wizara ina ugomvi na huyo faru mweusi?
 
Ukweli ni kwamba hakuna Faru mweusi aliyeonekana katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere kama ilivyoripotiwa na mtandao huo.
Ili kuuthibitishia umma kuwa ni uzushi basi wafungulieni kesi mahakamani kama mlivyoofanya kwa wazushi wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…