Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Na sasa watu wanampongeza ndugu aliyeshinda Marathon na kuleta medali nchini. Miaka kadhaa iliyopita Ramadhani Brother walifanya maajabu, Mwakinyo naye alileta ushindi na watu wengine mbalimbali.
Hawa watu wakihojiwa wanaweka wazi kuwa hawajapata msaada mkubwa kutoka kwa serikali na mara nyingine hata passport huwa mtihani kuipata.
Wapo vijana wengi wana uwezo mkubwa wakuleta medali mbalimbali nchini, swali ni je wizara zina mikakati gani ya kuhakikisha kuwa watu wenye vipaji wanapata support kubwa ili kuleta medali nchini.
Mara nyingi wanasiasa hujitokeza kupongeza bila kuwa sehemu ya mchakato. Suala la kupongeza mbali na kuwa halina ubaya lakini mara nyingi huonekana ni mikosi. Mathalani watu hushauri watu wengi wanaong'ara kimataifa wasiende bungeni au kuonana na viongozi wa kisiasa nchini ili wasizime nyota zao.
Hii sio tu chuki kwa viongozi bali ni kutoona ushiriki wa viongozi katika mchakato wa kuwakilisha taifa kimataifa.
Narudia swali, wizara zinamikakati gani ya kukuza vipaji vya watu?