Mkuu huo hauwezi kuita uporaji, tambua kuna sheria inayosimamia uendeshaji wa maduka hayo. Sasa ikiwa walikiuka lazima wakumbane na adhabu. Mfano tu nikupe, mtaji uliosajili wewe ni dola 300,000 wakaja kukagua na kufanya hesabu za usuluhishi ( accounts reconciliation) ukakutwa una ziada inafikisha mzunguko wako hadi dola 500,000. Moja kwa moja wewe ni mtakatisha fedha haramu ( money launder) na adhabu yake unaijua, hizo pess sio zako zinabebwa zote pamoja na kila kitu kilichokutwa humo.
Sasa hapo mtu asiyejua anaita uporaji wakati ni uhalifu wa kiuchumi umedhibitiwa.