Wizi huu wa Benki sio mzuri kwa Taifa

Hivi kwa nini wengi wanajifanya wana pesa nyingi sana humu JF? Wangekuwa na pesa ndefu wasingekuwa wanashinda JF kwa kueneza umbeya. Hebu endeleeni kusafisha vibibi vya kithungu kama BAK.

Hivi baba yako au babu yako akiizeeka na kutojiweza hiyo kazi ya kumuogesha hua anaifanya nani? Au wewe ukizeeka nani atakusafisha na kukusitiri? Acha kudhalau kazi za watu ndugu yangu... duniani humu, sote tunategemeana kwa namna moja au nyingine.

Hata ungekuwa Ginimbi wa Zimbabwe au Bill Gates, lazima tu utasafishwa muda wako ukifika... mfano , wewe ugua tu Malaria, hata mtu wa kukupa uji utamuona wa maana sana na mahela yako... kwa ufupi.

Humu JF watu wanatoa tu kero zao na najua wakubwa wanasomaga na kuzipatia kero majobu mujarabu.
 
Hapa ndio namkumbuka marehemu Dr Shika.
Inawezekana ni kweli ukawa na pesa benki ila ukafa njaa.
 
Mwaka jana mwezi wa 9 nilitumiwa $250,000 kutoka Canada na kampuni ya vmedia kwa njia ya bank [emoji542] transfer sikukatwa hata cent Zaid yeye ndio alikatwa. Bank ni NMB. Card ni Platinum, sms ilivyolia tu nikaenda kupakuwa mzigo nikakuta imo.
 
Nakuunga mkono kwa 100/%
 
Mwaka jana mwezi wa 9 nilitumiwa $250,000 kutoka Canada na kampuni ya vmedia kwa njia ya bank [emoji542] transfer sikukatwa hata cent Zaid yeye ndio alikatwa. Bank ni NMB. Card ni Platinum, sms ilivyolia tu nikaenda kupakuwa mzigo nikakuta imo.
Mungu wako ni mkubwa na pengine wakati unatumiwa pesa wahusika BOT walisinzia wakakusahau wenye bahati kama zako mpo wachache mno lakini wengi huteseka mno kupata pesa zao pindi zikitumwa tokea nje ya Nchi.
 
Hapa ndio namkumbuka marehemu Dr Shika.
Inawezekana ni kweli ukawa na pesa benki ila ukafa njaa.
Wengi wamekufa na wengine wetelekeza pesa zao huko baada ya kufuatilia kwa mda mrefu pasipo mafanikio
 
Sijaelewa kwa nini umemquote Pascal Mayalla

... au ndio wewe Pascal umekuja kivingine, ili usionekane umeigeuka serikali ya chama chako?
 
Sasa kama husemi Bank yenyewe sasa hapa umeleta malalamiko ya nini, tutathibitishaje?
 
Wengi hupigiwa hesabu kihuni huni kisha kubambikiwa kesi za utakatishaji fedha na uhujumu uchumi ambayo sasa ni fimbo inayotumika vibaya kuwaonea wengi kienyeji kwa njia haramu za kishetani
Sina uhakika sana na unachokisema na siwezi kukukatalia ila mimi ninachokijua na kile nina uzoefu nacho ni kuwa kwa hesabu za kihasibu na mtaalamu wa kitengo cha FIU ni rahisi mno kwake kubaini money laundering akiingia kukukagua.

Hata hawa wenye utajili usioelezeka sema serikali inawafumbia macho tu ila ukweli wakiamua kukufuatilia hauponi. Wanaanzia kwenye yaarifa zako za kodi TRA. Kwa urahisi tu, una mali ya milioni 500,000,000 TZS, lakini TIN yako inaonyesha mpaka muda huo kodi uliyolipa ni milioni 20 kwa mfano. Sasa hapo kuna mawili.

1. Ulikuwa unakwepa kodi. Utapigiwa hesabu ya kodi toka kipindi ulipozipata hizo mali na adhabu yake. Unajikuta unadaiwa bilioni 1 zaidi ya mali ulizonazo. Kwanini usiwaachie zote? Ndugu, hii ipo kwenye sheria za kodi sema jamaa wanapotezea mambo yaende lakini wakikomaa wengi wanaumia. Na ndio maana Serikali ikiamua kukutafuta kukumaliza hapa hauponi.

2. Ulikuwa unajihusisha na utakatishaji fedha haramu ndio maana fedha zako hazikupita kwenye mfumo sahihi zikatozwa kodi. Hapa kwa nchi kama hizi za kwetu kuna changamoto tofauti na nchi za wenzetu walioendelea mtu hujikadiria kodi mwenyewe na kulipa pale anapogundua amezidisha hudai na kurudishiwa. Zidisha sasa hapa kwetu uone. Sasa kilichopo hapa ndio changamoto ilipo, nimeuza ng'ombe, mahindi nyumbani, nafanya hivyo miaka nenda rudi na utaratibu wetu sisi huku ni mpaka TRA wakutafute ndipo ulipe kodi, hapo ndio hili suala hushindikana kidogo.

Anyway cha mambo ni mengi na yana changamoto zake pale yanapotumika vibaya.
 
Vinginevyo,kama hawselezi hiyo ni benki gani hii stori ni ya uongo
 
Hapa kuna maswala mawili!!! Swala wako porini, sema masuala!
 
we chawa wa mhindi acha kuchafua taasisi za fedha...ela yoyote inayokuja juu ya dola 10,000 lazima iwe na kielelezo cha kuja hapa....usije tuletea fedha ya ugaidi au madawa..unakuja nunua magari hata invoice ya kununulia hujaipeleka bank unategemea nn nenda basi huko india na hiyo dolla laki 1 uone ka utaitoa tu kama maembe...ushasikia kitu kinaitwa ANTI-MONEY LAUNDERING LAWS lakini
 
Pesa ni yako ikiwa mikononi mwako,tofauti na hapo inaweza isiwe yako
Zamani Serikali Ilikuwa Inafanywa Chochote Na Wenye Pesa
Lakini Utawala Wangu Mwenye Pesa Anaweza Kufanyiziwa Lolote!!
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜…πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Unaogopaje kuitaja kama pesa ni halali yako? Au ni Money Launders?
Atutajie Bank Vinginevyo Ni Ujanjaujanja Tu
Unataka Kuichonganisha Serikali Yetu Na Wananchi Wake
Hatutakubali!! Maalim Anakula Boflo Huko Zanzibar
 
Lete Jina La Bank
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…