Wizi mita za maji Dodoma: Yabainika zatumika kutengenezea bangili na pete

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph amesema imebainika mita zinaziibiwa zinakwenda kutengenezea bangili na pete

"Katika vitu ambavyo vinatoka changamoto hapa kwa sasa hivi katika jirodoma ni wizi wa mita. Wananchi wengi wanalalamika kuibiwa mita katika maeneo yao hasa wale ambao mita zao ziko nje au hawana fens."

"Na tunazozungumza leo mpaka nakuja hapa ndani ya kipindi cha miezi mitatu takwimu zinanionyesha kwamba mita 103 zimeibiwa. Kwa hiyo ni kama wastani wa zaidi ya 30 hivi kwa kila mwezi. Hilo ni jambo la hatari."

Hao wanaoiba mita wanaenda kuzifanyia nini? Kwa ambao tumeweza kufanya uchunguzi wengi wanaenda kuyeyusha na kutengeneza bangili, pete... au kwa ajili ya chuma cha kavu."

Soma Pia: Waziri wa Maji Ingilia Kati Wizi wa Mita za maji Iringa mjini

"Sasa hivi atakayekamatika tunatakiwa tumshtaki kwa ile sheria ya uchumi."

Hapo DUWASA Kuna mfanyakazi wao anakatakata mita Kwa fundi kuchomelea anaitwa Big pembeni ya ofisi Yao. Vyombo vya Sheria viwaulize machalii WA hapo kistaarabu watawatajia jina la mwamba anaendaga kukatakata mita Kila mwezi hapo
 
Ngozi nyeusi kama laana, huyo Big akamatwe haraka yaan anawapa tabu wateja

Hongera kwa kuwa mzalendo kwa kutoa taarifa
 
Hapo DUWASA Kuna mfanyakazi wao anakatakata mita Kwa fundi kuchomelea anaitwa Big pembeni ya ofisi Yao. Vyombo vya Sheria viwaulize machalii WA hapo kistaarabu watawatajia jina la mwamba anaendaga kukatakata mita Kila mwezi hapo
Wenyewe Kwa Wenyewe
Ntu' Wa Dili, Kataa
 
Sasa hapo mnategemea nchi iendelee?
Mara wameiba Transfoma na sasa haya tena
Hata kama kuna njaa na shida, hapana kwa kweli

Hawa ni wa kunyonga tu
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph amesema imebainika mita zinaziibiwa zinakwenda kutengenezea bangili na pete

Hao wanaoiba mita wanaenda kuzifanyia nini? Kwa ambao tumeweza kufanya uchunguzi wengi wanaenda kuyeyusha na kutengeneza bangili, pete... au kwa ajili ya chuma cha kavu."
Hii nchi imekithiri kwa vituko, sasa huyu anauliza swali wakati alishajijibu mwenyewe mwanzoni mwa maelezo yake
 
Sasa hapo mnategemea nchi iendelee?
Mara wameiba Transfoma na sasa haya tena
Hata kama kuna njaa na shida, hapana kwa kweli

Hawa ni wa kunyonga tu
Unaweza kukuta na hao wezi nao pia hua wanalaumu mitandaoni kuhusu maendeleo na kulaani wizi wa mali za umma.
 
Hapo DUWASA Kuna mfanyakazi wao anakatakata mita Kwa fundi kuchomelea anaitwa Big pembeni ya ofisi Yao. Vyombo vya Sheria viwaulize machalii WA hapo kistaarabu watawatajia jina la mwamba anaendaga kukatakata mita Kila mwezi hapo
DUWASA ya wapi?
 
Back
Top Bottom