Wizi unaofanywa na makampuni ya kusafirisha watu kwa ajili ya kazi nje ya Tanzania

Azniv Protingas

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2020
Posts
335
Reaction score
554
Habari wana JF, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, sasa hivi kutokana na uhaba wa ajira ndani ya nchi yetu ya Tanzania, kuna makampuni ambayo yanatangaza yanatoa ajira nje ya nchi, hasa nchi za uarabuni.



Makampuni hayo yameanzisha mchezo wa kutangaza kuwa kuna kazi fulani, lakini inahitajika kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya kujiandikisha. Watu wanaenda kujiandikisha lakini hakuna interview inayofanyika na pesa hazirudishwi.


Mwezi wa tatu kuna kampuni zilitangaza kuwa kuna nafasi za kazi Saudi Arabia na kujiandikisha kwa ajili ya hizo kazi ni 50,000/- hiyo pesa ni kwa ajili ya interview Tu. Kwa hiyo ukifeli au ukifeli hairudi hiyo pesa. Kuna watu walitoka sehemu mbalimbali za Tanzania lakini mpaka leo hakuna interview iliyofanyika na haijulikani ni lini hao wanaohusika na Interview kutoka kwenye kampuni ya Saudi Arabia watakuja lini.



Na pia hakuna mrejesho wowote kutoka kwa makampuni kwamba labda vumilieni tumewasiliana na hiyo kampuni na tumefikia wapi lakini hakuna. Na wahanga wakubwa wa huu utapeli ni wanaume.

Pia juzi kampuni mojawapo kati ya hizo walitangaza kuwa kuna kazi za Canada, pesa walizokula kwa ajili ya interview ya Saudia hazijawatosha wamekuja na kazi nyingine. Wanajificha kwenye kivuli cha kuwa tumesajiliwa na serikali kwa hiyo tunafanya kazi kihalali, tumepewa ruhusa na serikali.





N.b Sio kwamba hakuna ambaye amesafirishwa na hizo kampuni wapo waliobahatika kupata ajira. Lakini hii ya Saudi Arabia inaonekana kama imetengenezwa ili watu watoe pesa za usajili kwa ajili ya kunufaisha matumbo yao. Watu wakilalamika kuwa pesa ya usajili ni kubwa wanajibu kwa jeuri kuwa, tutapata wapi pesa ya kodi na mishahara ya wafanyakazi.



Hizi kampuni ni mfano tu lakini zipo nyingi na kuna watu wametapeliwa zaidi ya hiyo 50000/-. Na hizi kampuni sio mara ya kwanza kushtakiwa, Kuna moja ilifungiwa lakini baadae ikafunguliwa tena.
 
kuna thread humu ya kupeleka watu poland
kam sijakosea sijawahi jua kam kuna watu walifikishwa huko poland😂
 
Inasikitisha sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kuwalaumu watanzania kwa ujinga na kutapeliwa, lazima tufahamu kuwa watu tunatofautiana kwenye kufikiri na kutatua changamoto zinazotukabili.
Serikali inabidi izifuatilie hizo kampuni zinazolalamikiwa kwa utapeli!!
 
Ngoja nikisanue mwanangu, hao nao ni graduates kama nyie wamekosa kazi wametafuta namna ya kuishi wakaona ni wajinga wengine wenye tamaa, si ajanu hata kenya hawapajui... jiongezeni😀😀😀
 
Pole sana
 
kuna thread humu ya kupeleka watu poland
kam sijakosea sijawahi jua kam kuna watu walifikishwa huko poland😂
Hakuna ukweli wowote kikubwa utaambiwa utoe pesa kwa ajili ya visa na agent fee, halafu imeisha hivyo.
 
Huwezi kuwalaumu watanzania kwa ujinga na kutapeliwa, lazima tufahamu kuwa watu tunatofautiana kwenye kufikiri na kutatua changamoto zinazotukabili.
Serikali inabidi izifuatilie hizo kampuni zinazolalamikiwa kwa utapeli!!
Itakuwa vizuri Lkn hata zikifuatiliwa wataachiwa wataendelea kupiga watu wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…