Zinedine
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 1,187
- 694
Mkuu hiyo kwenye red wako wapi hao mkuu maana nami najiandaa kuanza ujenzi.
Hao Yemen wako Buguruni ukipita Kobil (Maarufu shell), lakini kabla hujaenda ujiandae kunywa dawa za kuzuia hasira. Maana sijaona wadada wa kiarab ambao wana dharau kuliko wao, infact siku ya kwanza nilivumilia nikanunua, lakini siku yapili nilishindwa bana ilibidi niwaambie ukweli then nikatimua zangu. Huwa najiuliza sana hali ya wafanyabiashara wetu katika hili soko la Pamoja la East Afrika! kusema ukweli kenya watatuburuza sana, hawana ujanjaujanja huo, wana lugha nzuri ya biashara, atakachokwambia ndio chenyewe/fake atakwambia fake, china atakwambia china, Japan Japan, Gage atakwambia kwa usahihi wake. Nakushauri badala ya Yemen au Wahenga nendeni Tabata ukivuka daraja la baada ya Njia panda ya tabata ukiwa unaenda Ubungo, then turn right utaona wako jamaa pale nadhani ni warusi au sjui kina nani-Wanauza bei poa saaaana na hawako kwa ajili ya kutangaza utukufu wao kama hao yemen, usalama ni wa kutosha, they have each an everything katika ujenzi.