Wizi wa cover za nyuma za side mirror unakuwa kwa kasi unazaminiwa na wauza spea (used) wa magari

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau.

Kuna wizi wa ajabu sana kwenye magari.

Wanaiba cover ya nyuma ya side mirror tu sababu ni rahisi kuzichomoa. Hawachukui side mirror nzima. Na wanaiba sababu wanajua mwenye gari lazima ukanunue tena hicho ki cover.

Wezi wanaenda kuwauzia wauza spea hivyo vi cover vya wizi na wauza spea wanatuuzia tena tulioibiwa

Wizi huu umetamalaki sana kwenye gari aina ya IST, PASSO, SUBARU, etc.

Unapopaki gari yako sehemu kuwa makini sana. Maana hivyo vi cover wanavichomoa dakika tu
 
Piga libiti sijui kama spelling nimepatia ila zinaitwa ivyo. Ile cover ikishakua na shimo la libiti haliuziki.
Yesss upo sahihi kabisa...Ila wabongo wanazingua sana unakuta gari ikifika TANZANIA tunaanza kuchora vioo,tunapiga libiti kila sehemu hii yote Kwaajili kuzuia wizi Hadi gari inakuwa kama Banda la chipsi kila sehemu imegongewa misumari
 
Yesss upo sahihi kabisa...Ila wabongo wanazingua sana unakuta gari ikifika TANZANIA tunaanza kuchora vioo,tunapiga libiti kila sehemu hii yote Kwaajili kuzuia wizi Hadi gari inakuwa kama Banda la chipsi kila sehemu imegongewa misumari
Hahaha na kweli mkuu maana bila kufanya ivyo kila siku utakua unanunua spare udokozi bongo ni mwingi sana.
 
Mimi sijaibiwa ila niligonga sehem, sikuweka rivet vikatoka. Hii ni ya subaru forester 2011 hapo imenitoka 150,000 kuagiza vyote vitatu online aliexpress( cover kubwa dogo na kitaa) hapa bongo nimekosa wanasema ninunue sidemirror complete inauzwa 750,000View attachment 2335079
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…