DOKEZO Wizi wa Fedha NHIF unaofanywa na Meneja wa Mkoa wa Dodoma (Fidelis Shauritanga) na baadhi ya Watumishi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

boneagain2022

New Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
3
Reaction score
4
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, naomba kuwasilisha tuhuma za WIZI wa fedha za Umma katika Ofisi ya Mkoa wa Dodoma kwa miaka minne tangu 2018 mpaka 2022. Ninaamini taarifa hii itavifikia vyombo vinavyoshughulikia Maadili ya Viongozi wa Umma pamoja na Utawala Bora kwa ajili ya kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.

Ofisi ya NHIF Mkoa Dodoma kwa muda wa miaka minne imekua inaadaa mipango kazi za nje ya Ofisi kwa ajili ya kwenda kutafuta Wanachama wapya na kusajili Vituo vya Huduma za Afya. Hata hivyo, Meneja wa Mkoa Fidelis Shauritanga kwa kushirikiana na Maafisa Wanachama wafuatao; Linus Kaana, Sunday Matoi, Emmanuel Magese, Zuena Hassan na Ashiel Faustine wamekuwa wanagawana fedha za safari za kikazi lakini hawasafiri bali wanabaki Ofisini. Hivyo, Ofisi hii imekuwa ikijilipa malipo hewa na kubaki Ofisini jambo ambalo ni kosa na wizi wa fedha za umma.

Ubadhirifu huu uliripotiwa kwa vyombo vya uchunguzi. Uchunguzi ulithibitisha matumizi haya ya fedha ambapo wahusika walikiri na kuandika barua za kuomba kurudisha fedha hizo. Hata hivyo uchunguzi ulifanywa kwa mwaka mmoja tu lakini ubadhirifu huu umekuwa ukifanyika kwa miaka minne. Kitendo cha kukiri kugawana fedha za Umma na kuomba kurudisha fedha hizo hakuondoi jinai kwa Meneja wa Mkoa Dodoma na Watumishi waliotajwa. Ziko taratibu za Mwajiri kuchukua kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Kanuni za Utumishi.

Jambo la kushangaza, Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala inayokaimiwa na Ndg. Lameck Kabeho ilipewa taarifa ya uchunguzi huu uliothibitishwa na taasisi ya Uchunguzi lakini Mwajiri amekaa kimya na kuwalinda. Meneja wa Mkoa Dodoma na Watumishi waliotajwa hawajawahi kuchukuliwa hatua yoyote jambo ambalo linatafsiriwa kama Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya inawaslinda baadhi wa Watumishi wa Mfuko dhidi ya wizi wa mali ya umma.

Ili kulinda heshima ya Taasisi hii ya Umma, ninawasilisha taarifa hii kwa ajili ya hatua stahiki. Ninaamini Meneja huyu na Watumishi walio chini yake waliotajwa watachukuliwa hatua na Mwajiri ili kulinda taswira njema ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Naomba kuwasilisha.
 
Ni kweli umefanya jambo la kizalendo ila wewe una roho mbaya sana na ni mjinga haswa, ni kwanini usiingeenda takukuru tu moja kwa moja au polisi au wizarani moja kwa moja kupeleka malalamiko haya badala ya unavyofanya sasa kuwatangaza na kuwadhalilisha hao watu tena kwa majina yao nchi nzima?

Ni wazi wewe ni miongoni mwa wafanyakazi hapo ofisini kwao na una hasira haujawai kupata trip za safari ili na wewe upate ka kipato maana kwa akili hizi ni wazi mshaara wako sio juu ya laki tano.

Haya uliyo yaandika hapa hakuna mtu atakae yafanyia kazi ila utawapa ulaji wakubwa wengine wa kuchota mapesa toka kwa hao watu kwa njia ya kuwatisha tu.
 
Ulitaka waibe wapi ...saiz nikupiga tu. nawe ucjekuwa unataka uteuzi!! maana kama wanazipiga karipo vyombo vya sheria .huyu unaemwambia ndyo kazi yake?
 
Kwani taasisi yenu haina utaratibu wa kuwasilisha malalamiko? Wewe una roho ya KIBARUA.

Umeshindwa hata kumwandikia Mwenyekiti wenu wa Bodi mpaka uje huku. Haya ya kuwaaibisha wenzio kuna siku yatakurudi, kama si wewe basi mwanao.

Nenda kanisani ukatubu.
 
Ni kweli umefanya jambo la kizalendo ila wewe una roho mbaya sana na ni mjinga haswa, ni kwanini usiingeenda takukuru tu moja kwa moja au polisi au wizarani moja kwa moja kupeleka malalamiko haya badala ya unavyofanya sasa kuwatangaza na kuwadhalilisha hao watu tena kwa majina yao nchi nzima?

Ni wazi wewe ni miongoni mwa wafanyakazi hapo ofisini kwao na una hasira haujawai kupata trip za safari ili na wewe upate ka kipato maana kwa akili hizi ni wazi mshaara wako sio juu ya laki tano.

Haya uliyo yaandika hapa hakuna mtu atakae yafanyia kazi ila utawapa ulaji wakubwa wengine wa kuchota mapesa toka kwa hao watu kwa njia ya kuwatisha tu.

Mshaara
 
Kwani taasisi yenu haina utaratibu wa kuwasilisha malalamiko? Wewe una roho ya KIBARUA.
Umeshindwa hata kumwandikia Mwenyekiti wenu wa Bodi mpaka uje huku.Haya ya kuwahaibisha wenzio kuna siku yatakurudi, kama si wewe basi mwanao.Nenda kanisani ukatubu.
acheni upuuuuzi hakuna njia yeyote ya kiustaarbu ya kumsema mwizi hivyo muwasilishaji yuko sahihi na mi naagiza wachukuliwe hatua haraka
 
Ni kweli umefanya jambo la kizalendo ila wewe una roho mbaya sana na ni mjinga haswa, ni kwanini usiingeenda takukuru tu moja kwa moja au polisi au wizarani moja kwa moja kupeleka malalamiko haya badala ya unavyofanya sasa kuwatangaza na kuwadhalilisha hao watu tena kwa majina yao nchi nzima?

Ni wazi wewe ni miongoni mwa wafanyakazi hapo ofisini kwao na una hasira haujawai kupata trip za safari ili na wewe upate ka kipato maana kwa akili hizi ni wazi mshaara wako sio juu ya laki tano.

Haya uliyo yaandika hapa hakuna mtu atakae yafanyia kazi ila utawapa ulaji wakubwa wengine wa kuchota mapesa toka kwa hao watu kwa njia ya kuwatisha tu.
Hizo ni tuhuma nzito, sio rahisi mtumishi kujitoa muhanga kwa kwenda kurupoti suala hilo takukuru au sehemu yoyote maalumu.

Hapo amelinda kibarua chake, na usalama wake na usalama wa familia yake.

Umafia ni mwingi sana... Jifanye mzalendo tukufunze adabu.

Kama hawajaiba hakuna shida, ila kama wameiba wawajibishwe tu.
 
Kabla hii haijaisha, skendo nyingine tena!
1661693195914.jpg
 
Baada ya siku chache kila kitu kitasahaulika na maisha yataendelea.
 
Lakini atakuwa ametua mzigo ulioko kifuani kwake.Hayo mengine Ni ya wanachama watakaofia kwenye mabenchi kwa kukosa huduma.
 
mkuu hivi unajua uliowataja hapo wana familia zinawategemea? ungefikiria kwanza kuhusu familia zao ndio uje uandike hapa.
 
Ni kweli umefanya jambo la kizalendo ila wewe una roho mbaya sana na ni mjinga haswa, ni kwanini usiingeenda takukuru tu moja kwa moja au polisi au wizarani moja kwa moja kupeleka malalamiko haya badala ya unavyofanya sasa kuwatangaza na kuwadhalilisha hao watu tena kwa majina yao nchi nzima?

Ni wazi wewe ni miongoni mwa wafanyakazi hapo ofisini kwao na una hasira haujawai kupata trip za safari ili na wewe upate ka kipato maana kwa akili hizi ni wazi mshaara wako sio juu ya laki tano.

Haya uliyo yaandika hapa hakuna mtu atakae yafanyia kazi ila utawapa ulaji wakubwa wengine wa kuchota mapesa toka kwa hao watu kwa njia ya kuwatisha tu.
Kafanya kitu kizuri sana, kaleta kwa uma ili wahusika wasijesema hawakupewa taarifa. NHIF imejifia tu, huduma zake ni mbovu, huku watu wanajilipa wakiwa Ofisini.
 
Back
Top Bottom