DOKEZO Wizi wa Fedha za NHIF unaofanywa na Meneja wa Mkoa wa Dodoma na baadhi ya Watumishi

DOKEZO Wizi wa Fedha za NHIF unaofanywa na Meneja wa Mkoa wa Dodoma na baadhi ya Watumishi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Status
Not open for further replies.
A

Anonymous

Guest
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, naomba kuwasilisha tuhuma za WIZI wa fedha za Umma katika Ofisi ya Mkoa wa Dodoma kwa miaka minne tangu 2018 mpaka 2022. Ninaamini taarifa hii itavifikia vyombo vinavyoshughulikia Maadili ya Viongozi wa Umma pamoja na Utawala Bora kwa ajili ya kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.

Ofisi ya NHIF Mkoa Dodoma kwa muda wa miaka minne imekua inaadaa mipango kazi za nje ya Ofisi kwa ajili ya kwenda kutafuta Wanachama wapya na kusajili Vituo vya Huduma za Afya. Hata hivyo, Meneja wa Mkoa kwa kushirikiana na Maafisa Wanachama wamekuwa wanagawana fedha za safari za kikazi lakini hawasafiri bali wanabaki Ofisini. Hivyo, Ofisi hii imekuwa ikijilipa malipo hewa na kubaki Ofisini jambo ambalo ni kosa na wizi wa fedha za umma.

Ubadhirifu huu uliripotiwa kwa vyombo vya uchunguzi. Uchunguzi ulithibitisha matumizi haya ya fedha ambapo wahusika walikiri na kuandika barua za kuomba kurudisha fedha hizo. Hata hivyo uchunguzi ulifanywa kwa mwaka mmoja tu lakini ubadhirifu huu umekuwa ukifanyika kwa miaka minne. Kitendo cha kukiri kugawana fedha za Umma na kuomba kurudisha fedha hizo hakuondoi jinai kwa Meneja wa Mkoa Dodoma na Watumishi waliotajwa. Ziko taratibu za Mwajiri kuchukua kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma na Kanuni za Utumishi.

Jambo la kushangaza, Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala ilipewa taarifa ya uchunguzi huu uliothibitishwa na taasisi ya Uchunguzi lakini Mwajiri amekaa kimya na kuwalinda. Meneja wa Mkoa Dodoma na Watumishi hawajawahi kuchukuliwa hatua yoyote jambo ambalo linatafsiriwa kama Menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya inawaslinda baadhi wa Watumishi wa Mfuko dhidi ya wizi wa mali ya umma.

Ili kulinda heshima ya Taasisi hii ya Umma, ninawasilisha taarifa hii kwa ajili ya hatua stahiki. Ninaamini Meneja huyu na Watumishi walio chini yake waliotajwa watachukuliwa hatua na Mwajiri ili kulinda taswira njema ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Naomba kuwasilisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom