Wizi wa Karne! Benki Kuu Yaibwa Bila CCTV Kuona – Hela Zaidi ya Bilioni 180 Tsh Zimepulizwa

Wizi wa Karne! Benki Kuu Yaibwa Bila CCTV Kuona – Hela Zaidi ya Bilioni 180 Tsh Zimepulizwa

Ashampoo burning

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2023
Posts
1,299
Reaction score
3,977
Tarehe 8 Agosti 2005, Jumatatu pale Ceará, Brazil – mambo yalilipuka!
Wakati walinzi wa benki walikuwa kwenye ukaguzi wao wa kawaida ndani ya chumba cha hazina, wakakutana na kitu cha ajabu sana. Mbele yao, shimo kubwa limetobolewa sakafuni, na kumbe si mchezo – zaidi ya tani 3.5 za hela taslimu, sawa na dola milioni 70, zimeshakwanguliwa!
OIG4.jpeg




Walinzi walipatwa na butwaa, sekunde mbili tatu wakaamua: "acha tuwapigie wakubwa wa sirikali mara moja."


Polisi waliposhusha mguu eneo la tukio, macho yakawa wazi. Swali kubwa likawa: hawa watu waliwezaje kufanya hivyo bila kugongwa na CCTV wala sensa za mwendo?
Hapo polisi wakajua – hii si wizi wa kawaida, hii ni movie kabisa!


Sasa swali likabaki: hao wezi ni kina nani hadi wakapenya kwenye benki moja ya salama zaidi nchini, bila hata kufumaniwa? Na walitumia ujanja gani kuipiga jackpot hii ya kihistoria?


👉 Hapo ndipo simulizi hili la kutisha na la kusisimua linaanza..
.
 

Machi 2005 – Miezi Minne Kabla ya Wizi​


Machi 2005 kule Brazil, kabla hatujafika Augusti ya wizi mkubwa, tayari mchezo ulikuwa umeanza kupikwa. Si mchezo wa kawaida bwana, hii ilikuwa recipe ya karne. Kundi moja la majamaa walikuwa wanapanga kuvamia Benki Kuu ya Brazil (Banco Central do Brasil) – sio benki ya mshahara au ya mtaani, hii ni ile benki mama yenye hela zote zinazotembea nchini.


Boss wa operation alikuwa jamaa mmoja anaitwa kwa jina la utani Alemão. Jamaa alikuwa ni mzee wa heshima kwenye ulimwengu wa uhalifu – akitembea mtaani wezi wengine wanapiga saluti. Tayari alikuwa ameshawahi kuvunja mabenki makubwa, so jina lake lilikuwa linatisha.


Mpango wake? Kuchimba handaki refu chini kwa chini mpaka lifike moja kwa moja kwenye chumba cha hazina. Si unajua pale kwenye chuma cha chuma, milango mizito, na mifuko ya mabilioni? Ndiyo huko.


Kwa hivyo Alemão akaanza kukusanya team yake kama vile mtu anaweka Avengers:


  • Kwanza, akatafuta mkono wake wa kulia – mtu wa kumsaidia kushika kasi pale ambapo yeye hatakuwapo. Huyu alikuwa kama “second-in-command.”
  • Halafu akaingiza jamaa anaitwa Doutor – mhandisi wa majengo. Jamaa alikuwa kichwa, anachora ramani ya handaki mpaka unashangaa. Yeye ndiye alibuni design ya tunnel kutoka mwanzo hadi mwisho.
  • Next akamleta Tatuzão, fundi mwenye mikono ya dhahabu. Jamaa alikuwa ni legend wa kuchimba – akipewa mpango, anakokota wachimbaji wengine bila kusimama. Yeye ndiye captain wa ground.

Lakini kabla hata ya Alemão kuanza kuunda hiyo dream team, kulikuwa na mtu mmoja wa maana zaidi – mlinzi wa benki. Sasa huyu ndiye aliyewapa life-line. Jamaa akapiga zungu zote: akatoa ramani kamili ya jengo, alionyesha zilipo kamera za CCTV, motion sensors, ukubwa wa vyumba, na hadi zile containers za hela zilivyojipanga humo ndani.


Hapo Alemão akatabasamu, akasema:


“Mchezo huu sasa hauta-balance, tutavuna! Na jamaa huyu, nikishamaliza kazi lazima apate share yake.”

Na hapo ndipo mchezo wa karne ulipoanza kupikwa taratibu – chini ya radar, kimya kimya, lakini kwa hesabu kali.
 

Kuanzisha Biashara Feki​


Sasa basi, miezi mitatu kabla ya dili lao, jamaa mkubwa Alemão akakodisha nyumba moja ya zamani, kama base ya genge. Pale ndipo wangefanyia mikutano, kupanga hesabu, na kusuka mbinu zote. Ila haikuishia hapo – akakodisha pia nyumba nyingine jirani kabisa na Benki Kuu ya Brazil. Hapo ndipo walipopanga kuanzisha safari ya handaki lao.


Sasa unajua lazima ukicheza game kubwa lazima ujipange kuficha nyendo zako. Alemão hakuwa mjinga. Akaibuka na idea kali – akafungua kampuni feki ya landscaping, biashara ya bustani, ati wanauza nyasi bandia (artificial turf). Ujanja ulikuwa mmoja: majirani wawaone wakitoka na magunia ya udongo, wasijue chochote, wadhani tu wanafanya kazi ya bustani. Kwa macho ya jirani ilikuwa biashara halali kabisa, kumbe ndani yake ni project ya wizi wa karne.
OIG1 (1).jpeg



Doutor, yule mhandisi bingwa, akaleta mchoro wa handaki. Sasa changamoto ilikuwa kali – Brazil haina ramani nzuri za mabomba, nyaya, mifereji ya maji. Kwa hiyo kuchimba kulikuwa na hatari ya kugonga waya au bomba lolote wakati wowote. Ila Doutor hakuwa mtu wa mchezo, akafanya hesabu zake, akapiga mawe hadi akaleta ramani safi.


Alemão akapiga shangwe, akasema, “Basi hii kazi tunavunja bila stress.” Mara moja akatoa oda ya vifaa vyote – mashine za kuchimba, lori za kubeba udongo, magari yenye stika za kampuni yao ya landscaping, hadi mabango ya biashara ili ionekane legit kabisa.


Kila jamaa wa genge akapewa uniform za wafanyakazi wa bustani – overalls, gloves, viatu vya kazi. Majirani walipowaona walidhani ni watu wa landscaping wana hustle kawaida, kumbe jamaa walikuwa wanaingia ndani ya historia.


Zaidi ya hapo, Alemão akamchukua hata ndugu wa mke wake awe secretary wa kampuni. Jamaa hakuwa na clue kabisa, anadhani ni biashara genuine. Kumbe anashikilia cover ya moja ya wizi mkubwa zaidi duniani.
 
Mei 2005, Fortaleza – Brazil.
Hapo ndipo kazi ya kweli ilianza – kuchimba handaki. Wale jamaa wa Alemão walikuwa na countdown yao kali: lazima wamalize kabla ya tarehe yao ya dhahabu – Agosti 6, 2005.


Sasa unajua kwa nini waliichagua hiyo tarehe? Si bahati mbaya bwana. Hiyo siku ilikuwa ya kusafirisha ma-bundle ya noti mbovu kutoka mabenki zingine kupeleka Benki Kuu wakazipige check. Zile ambazo hazina maana zingechomwa moto. Lakini bado – zilikuwa na thamani mbichi, na mbaya zaidi (au bora kwao), hakuna rekodi ya serial numbers. Yaani ukishapata, hakuna system inaweza kufuatilia. Pesa safi kabisa, ghost money.


Sasa imagine scene. Hapo Rua 25 de Março namba 1071, nyumba ya kawaida tu, lakini ndani yake kulikuwa gateway ya pesa za ndoto. Umbali? Ni kama kuvuka barabara kuu – Avenida Dom Manuel – basi unakutana uso kwa uso na Benki Kuu.


Handaki walilochimba? Ebu sikia specs:


  • Urefu: mita 80 straight,
  • Kina: mita 4 chini ya ardhi,
  • Kipenyo: sentimita 70 tu – enough kwa mtu kujisukuma kama snake.

Sasa kazi ya kuondoa udongo? Wamepiga creative cover-up. Udongo wote waliweka magunia, waka-pack kwenye lori. Guess what? Lori limepambwa vizuri na stika za ile kampuni yao fake ya landscaping. Majirani wanawaona wakitoa tani 30 za mchanga, lakini wanadhani ni “biashara ya bustani inasonga mbele.” Yaani hakuna mtu hata mmoja alihisi kuna kitu kinaenda chini ya ardhi.


Walikuwa wameset kila kitu kama pro project:



  • Mlango wa chumba walipoanzia shimo? Waliufunga na kufunika kwa mbao na carpet – hata yule katibu wa kampuni (shemeji ya Alemão) hakushuku chochote.
  • Handaki yenyewe? Walipiga finishing safi kama site ya ghorofa: nguzo za mbao zili-support ukuta, umeme ulipigwa connection, kulikuwa na maji, simu, AC na ventilation system kali. Hapo ndani ilikuwa kama mini-office chini ya ardhi, sio shimo la kawaida.
  • Wachimbaji waligawanyika zamu tatu – yaani 24/7 shovels zikichapa, mchanga ukipigwa clearing.

Na sasa boss wa finance – Fernandinho mdogo. Jamaa ndiye alifungua wallet, akadrop zaidi ya 200,000 reais ili mradi usimame. Bila yeye, hakuna hata spade moja ingeangukia pale chini.


Kwa kifupi, Mei 2005 ilikuwa moto. Waliishi kama watu wa kawaida juu ya ardhi, lakini chini ya miguu yao – ndoto kubwa ya wizi wa karne ilikuwa inakua taratibu, mita baada ya mita.
OIG4 (1).jpeg
 
⚡ Wakati Tunaposubiri Kipande Kingine…


Wacha nikuambie kitu. Wakati jamaa walikuwa chini ya ardhi wakichimba handaki, wewe pia unaweza kujipanga kuweza kufanya business kubwa bila stress.


Kwa hiyo, wakati tunasubiri kuingia kwenye sehemu nyingine ya stori hii ya wizi, angalia hii offer ya vitabu:


📚 Jinsi ya Kuagiza Mizigo Kutoka China
📚 Jinsi ya Kuanza Biashara ya Dhahabu
📚 Machimbo ya Kariakoo – Maduka na Namba za Wajanja wa Jumla
📚 Jinsi ya Kutumia AI Kwenye Biashara


Hizi zote zipo pamoja, uki click link hii hapa https://lordnick.site/offer-kubwa/, unaweza kuzipata zote na kuanza kutumia mbinu hizi leo.
OFA YA KIPEKEE – VITABU VIWILI KWA PAMOJA! (1).png
 
Nakusapoti boss

Pichani ndo centre bank yenyewe kumbe bhana kisa cha kweli kbs
 

Attachments

  • BCB.png
    BCB.png
    2.6 MB · Views: 55

Siku ya Wizi – Agosti 6, 2005​


Hapo ndipo mambo yalipofika level kali. Baada ya miezi mitatu ya kuchimba, jamaa walifika moja kwa moja chini ya Benki Kuu, chini ya ardhi, kama wachawi wa pesa.


Challenge? Kuta za zege lenye nondo, nzito kama iron, unene wa mita 1.1 – si kitu cha kuchezea. Lakini jamaa walikuwa tayari: vifaa vizito, plan safi, na moyo . Waka-chop-chop, wakavunja kuta na hatimaye wakaingia ndani ya hazina.


Sasa hapa ndipo ingeanza action ya kweli. Kwa kuwa walikuwa na blueprint ya usalama, walijua hasa wapi pa kutembea bila kufumaniwa na kamera au sensa za mwendo. Walijua maeneo kamera hakuna (blind spots) – hakuna mtu anayeweza kusema “hapo kuna mtu” – yote ilikuwa math.


Walimata makontena matano yaliyojaa noti za 50 reais, kila moja ikiwa sawa na dola 22. Magunia mazito ya fedha, tani 3.5 kwa jumla, wakapakia kupitia handaki mpaka kwenye nyumba yao. Thamani? Reais milioni 164 – sawa na takribani dola milioni 70!
OIG1.jpeg



Lakini jamaa hawakuwa na time ya kucheka. Waliweza kufuta alama zote – walipaka chokaa na agricultural lime kila corner ya handaki na chumba walichotoka, fingerprints zilipotea. Kisha, kama ghosts, walitoweka bila ya mtu kuishi kuwa na clue yoyote.


Hii ilikuwa kama movie ya heist ya karne, hakuna script ingekuwa safi zaidi. Kila detail ilikuwa iko kwenye nafasi yake – kutoka blueprint, blind spots, magunia ya pesa, hadi lime ya kuficha alama.
 

Ugawaji wa Fedha na Mpasuko Kundi​


Hapo baada ya kugawa pesa, jamaa walikaa chini wakihesabu. Calculator? Hapo hakuna, brains tu za wizi.


Wakakubaliana hivi: kila mtu apate milioni 1.5 reais – si mbaya, ni cash kwa mtu wa mtaa. Lakini boss Alemão, yeye akabaki na zaidi ya milioni 150 – maana, yeye ndiye kingpin, yeye ndiye alicheki every detail ya operation.


Sasa unapofikiria kuwa kila mtu hatapiga kelele, hapana, moja ya jamaa aliamka na kusema:


“Eh bro, pesa hizi zilinganishwe sawa, hakuna bias!”

Alemão aka-turn, akampa look kali kali – na guess what? boom! Risasi moja ya kichwa – jamaa aka silence mara moja. 😂


Baada ya hayo, Alemão akazunguka, akatisha wengine wote, akisema:


“Sikia jamaa – usitumie hela hizi haraka! Ukienda spending sasa, polisi wataku-track. Hifadhi, jifunze kuwa smart.”

Na jamaa walibaki wakiwa silent, wote wakijua story ni serious, lakini.
OIG1 (2).jpeg
 

Ugunduzi – Agosti 8, 2005​


Jumatatu asubuhi, walinzi wa Benki Kuu walikuja kufanya check ya kawaida. Wakatoa macho… kisha boom! Shimo kubwa chini ya hazina. Noti mpya bado ziko salama, lakini zile za zamani? puff… zimetoweka


Polisi walifika haraka, wakaangalia CCTV – nothing. Sensa? Silent. Wakati wa action? Hawa jamaa walikuwa ghosts. Polisi walijua moja kwa moja – kuna mtu wa ndani alicheza game. Hii si wizi wa kawaida, bro.


Wakati walipita ndani ya handaki, macho yao hayakuamini:


  • Ngazi ikiongoza chini,
  • Mbao zenye kukashikilia walls,
  • Plastiki kufunika corner zote,
  • Nyaya za umeme na simu zikiwa safi,
  • Hata kiyoyozi kilikuwa installed!
  • OIG4 (1).jpeg

Lakini surprise ya kweli? Waliona kadi ya simu iliyodondoka chini – hiyo ilikuwa ya katibu wa kampuni feki. Bam! Hii ndio clue kubwa waliyoanza nayo.


Hiyo kadi ya simu ikawa ndo pa kuanzia – polisi wakaanza tap wire yaani kuhack simu za katibu, wakikusanya kila hint mpaka hela itakapopatikana.
 
Back
Top Bottom